Hivi ndiyo tumefika hapa ? Kweli jamani ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Wadau habari zenu.
Post hii nimesugua kichwa niiweke jukwaa gani , iwe muafaka.
Mwisho wa yote nikaona niitupe hapa ambapo hubeba vitu cocktail .
Wadau naandika post hii nikiwa na UCHUNGU mithili yake sijauchungika kiivi about 10 years past.
Nimefika Bugando (Hospitali ya Rufaa) mida si mirefu, ambapo nimemleta Mama yangu mzazi, kuja kufunguliwa Plaster of Paris (P.O.P)
Mwezi jana Mama yangu aliteleza nyumbani na kuanguka na akavunjika. Tukamleta Hosp akafungwa hogo na leo ndiyo siku ya kufunguliwa hogo.
Kilichojitokeza hapa mara baada ya kufika mapokezi, kwa kua bi. Mkubwa umri umeshakua arijojo, hakuwa amepewa magongo kwani yanamshinda kutembelea.
Tukaomba Wheelchair, jibu tukaambiwa hapa tuna wheelchair moja tu! Najibiwa na wahudumu hayo maneno. Mbele yetu tunakiona ki'wheelchair kimoja ambacho tayari kimebeba mgonjwa, na mtu ambae amemleta mgonjwa yule, lakini hawaoneshi kama wanadalili ya kwenda popote.
Kwa kua mimi mgonjwa wangu nilihitaji nimpeleke 3rd flr, nikamuomba yule mtu, muhudumu awaombe wale wenzetu ambao tayari walikua wanaimiliki wheelchair, kama wao watakua wanasubiri kitu, basi watuachie once mie nipelekee mgonjwa wangu then niwarejeshee.
Muhudumu akanijibu "cha kufanya we wasubirie wakija kupanda na wewe upande nao, wanaenda 9th flr wakiachia wewe ndiyo urudi nayo!"
Kwa wanaoijua Bugando kutoka mapokezi hadi ghorofa ya 9 si shghl ndogo, pamoja na lift zilizopo.
Nisiwachoshe my fellow members mengi yanatia uchungu nikomee hapa .
Bt niwaachie quiz MIAKA 50 YA UHURU TZ , HOSPITAL YA RUFAA WHEELCHAIR 1 ya kupokezana
Kweli ?
 
pole sana itabidi mumbebe tu hamna jinsi hiyo ndio hali halisi ya hosp zetu full uchungu na hasira..
 
pole sana....ndio maana tuko busy kuleta mabadiliko....vumilia kwani yote yana mwisho....freedom is coming kesho.....
 
Pole Judgement wheelchair zipo mkuu ungeuliza naweza pata wapi wheelchair ndio ungeona mziki wake...ungekipata ila kwa kuomba kama vile sio haki yako bungando naifahamu vizuri...ghorofa ya 9 ni mbali sio mchezo.
 
Wadau habari zenu.
Post hii nimesugua kichwa niiweke jukwaa gani , iwe muafaka.
Mwisho wa yote nikaona niitupe hapa ambapo hubeba vitu cocktail .
Wadau naandika post hii nikiwa na UCHUNGU mithili yake sijauchungika kiivi about 10 years past.
Nimefika Bugando (Hospitali ya Rufaa) mida si mirefu, ambapo nimemleta Mama yangu mzazi, kuja kufunguliwa Plaster of Paris (P.O.P)
Mwezi jana Mama yangu aliteleza nyumbani na kuanguka na akavunjika. Tukamleta Hosp akafungwa hogo na leo ndiyo siku ya kufunguliwa hogo.
Kilichojitokeza hapa mara baada ya kufika mapokezi, kwa kua bi. Mkubwa umri umeshakua arijojo, hakuwa amepewa magongo kwani yanamshinda kutembelea.
Tukaomba Wheelchair, jibu tukaambiwa hapa tuna wheelchair moja tu! Najibiwa na wahudumu hayo maneno. Mbele yetu tunakiona ki'wheelchair kimoja ambacho tayari kimebeba mgonjwa, na mtu ambae amemleta mgonjwa yule, lakini hawaoneshi kama wanadalili ya kwenda popote.
Kwa kua mimi mgonjwa wangu nilihitaji nimpeleke 3rd flr, nikamuomba yule mtu, muhudumu awaombe wale wenzetu ambao tayari walikua wanaimiliki wheelchair, kama wao watakua wanasubiri kitu, basi watuachie once mie nipelekee mgonjwa wangu then niwarejeshee.
Muhudumu akanijibu "cha kufanya we wasubirie wakija kupanda na wewe upande nao, wanaenda 9th flr wakiachia wewe ndiyo urudi nayo!"
Kwa wanaoijua Bugando kutoka mapokezi hadi ghorofa ya 9 si shghl ndogo, pamoja na lift zilizopo.
Nisiwachoshe my fellow members mengi yanatia uchungu nikomee hapa .
Bt niwaachie quiz MIAKA 50 YA UHURU TZ , HOSPITAL YA RUFAA WHEELCHAIR 1 ya kupokezana
Kweli ?

Mbwa'ko asipobweka unabweka mwenyewe.
Ungebeba maza mgongoni afu mdogo mdogo mpaka ghorofa ya 9.
BTW: Serikali ina magari worth Sh.T 5,000,000,000,000/=
 
Haki ya Mungu nakiomba vile vimbunga na masunami aliyoahidi Mh. Ezekia Wenje na vije fasta!
Nchi imepiga tiktaka huku imevaa msuli chukuchuku!
 
Pole mkuu, nadhani tumekosa uzalendo na uungwana lakin sio kwamba hicho kititorori kilibakia kimoja hosp kubwa kama hiyo...
 
Pole mkuu Judgment..

Ila hili si jukwaa sahihi... Ungepeleka kule HHM..
 
Pole mkuu, nadhani tumekosa uzalendo na uungwana lakin sio kwamba hicho kititorori kilibakia kimoja hosp kubwa kama hiyo...

Mtaly! Kadhia niliyoiandika hapo ndivyo ilivyonitokea jana, na sikuimalizia.
Kwani wakati naandika Sredi nilikua still yet sijapata kitoroli, hatimae kuna raia mmoja akanitonya nikatafute mawodini, na huko ndipo nilipokwenda gundua baadhi ya ma'nurse wanavificha na unapewa kwa kuwaachia senti, nilitoa buku 3 ndiyo nikapewa kitoroli tena kwa msisitizo mkubwa kukirejesha.
Na kesho Friday natakiwa nimrejeshe tena mgonjwa so mbali ya gharama za tiba ya mgonjwa nalazimika na budget ya kitoroli iwe budgeted already.
 
Pole sana mkuu BMC imeoza kuazia juu mpaka chini bora irudishwe kwenye utawala wa warumi wale labda adabu itapatikana.
 
pole sana, wahusika wenye dhamana wanajua kufanya sherehe tu ,miaka 50, muungano, kuwapa makaburu dhahabu, kusafirisha twiga, kutoa ardhi kwa wawekezaji, kuuza mashirika kama uda......mengine hawana habari nayo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom