Hivi ndiyo kusema tumeishiwa kiasi hiki?????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ndiyo kusema tumeishiwa kiasi hiki??????

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Richardbr, Dec 5, 2011.

 1. R

  Richardbr Senior Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wapendwa nina wasalimu katika jina la yule mwenye jina lipitalo majina yote.

  Salamu kwenu wanafunzi wote mlio vyuoni na mliomaliza masomo yenu.

  Salamu kwenu kina Babalao na wengine wengi mliobahatika kuwa wataalamu wa masula ya uchumi.

  Salamu kwenu viongozi wa Taasisi mbalimbali za kijamii na nyinginezo.

  Nasikitika kusema kuwa pamoja na uwepo wenu ninyi watu bado inaniuma kuona kwamba watanzania wengi hatufaidiki na Taaluma mlizo nazo hasa katika hili jukwaa Biashara na uchumi,sasa sielewei ndo kwamba tumeishiwa ama hakuna tunachoweza kufanya kuhakikisha kwamba jukwaa hili linatoa mchango unaokusudiwa katika jamii.

  Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali lakini asilimia kubwa imekuwa ni mijadala rahisirahisi tu na zaidi sana huisha na utani.

  Kwasababu ya hali hii imepelekea mpka hofu kwa watu kuleta mambo yao humu ndani hivyo naomba wenzangu tubadilike na turejeshe heshima ya jukwaa hili.

  Wenzetu wa JE Saccos walianzia hapa na sasa wamepiga hatua,njooni tulitumie jukwaa hili kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavyo.

  Tukumbuke Nchi yetu inamuda mchache kabla ya uvamizi wa nchi zinazo unda jumuiya ya EAC haujaanza naogopa wakati ukifika tukakutwa bado tunajadili habari za kina fulani wapeana mikono,naogopa kuja kuona tunashtuka wakati tumeshakuwa wageni katika Nchi yetu wenyewewe shime wana JF tuamke tuitumie nafasi hii pekee.

  Sera ya vyama vya ushirika inasema Jenga ushirika ukujenge tuungane na tuendelee kuelimishana jamani ili tupige hatua za kimaendeleo.

  JE Saccos uwe mfano mzuri wa kuigwa na sisi sote.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Jukwaa linatumika vizuri sana, kuna watu wameungana na kufanya mambo kupitia hapa. Kuna watu wamepata mawazo hapa na wanaendelea mbele. Labda tatizo ni mrejesho/feedback. Fuatilia uzi wa jamii farm, uzi wa Mtaji wa 10M, na mfano ulioutoa mwenyewe wa JE saccos. Niliwahi kusoma mtu mmoja tu aliyerudisha shukrani hapa,wengine tunauchuna.
   
Loading...