Elections 2010 Hivi ndivyo wizi wa kura ulivyofanyika!

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
picture-4.jpg


Na Saed Kubenea - Imechapwa 10 November 2010

slaa_214.jpg



MATOKEO ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yamejaa utata, MwanaHALISI limegundua.

Taarifa kutoka ndani ya NEC, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautiana na kura halisi zilizopigwa.


Kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).


Matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na mitatu ya Zanzibar, hadi juzi Jumatatu, yanathibitisha kuwepo tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na NEC.


Uchaguzi mkuu nchini ulifanyika Jumapili iliyopita kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais, kwa upande wa Tanzania Bara na masheha, wawakilishi na rais Visiwani.


Katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, matokeo yaliyotangazwa na NEC yanaonyesha kuwa CCM imepata kura za urais 35,910, huku CHADEMA ikionyeshwa kupata kura 18,513.


Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa CHADEMA yanaonyesha CCM imepata kura 20,120, huku CHADEMA ikipata kura 26,724.


Katika jimbo la Karatu, mkoani Arusha, hesabu za NEC zinaonyesha CCM imepata kura za urais 24,382, huku CHADEMA ikipata kura 41 tu; angalau kwa mujibu wa matangazo ya televisheni.


Bali kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa na mawakala na ambayo yamesainiwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi katika jimboni hilo, CCM imepata kura 24,364 na CHADEMA imepata kura 43,137.


Jimbo jingine ambalo matokeo yake yamejaa utata ni Geita, mkoani Mwanza. Matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo, yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 17,792, na CHADEMA imeambulia kura 3,989.


Lakini matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 30,960 na CHADEMA kimepata kura 15, 736. NEC ilikiri kuwapo kwa kasoro katika jimbo la Geita na ilikubali kufanyia marekebisho.


Katika jimbo la Ubungo, mkoani Dar es Salaam, matokeo ya NEC yameipa CCM kura 68,727 na CHADEMA kura 65,450.


Hata hivyo, kwa mujibu wa matokeo mikononi mwa mawakala katika jimbo hilo yanaonyesha kuwa CHADEMA imepata kura 72,252 na CCM kura 70,472.


Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya NEC kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha urais.


Kwa mujibu wa NEC, Kikwete alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali zilizopigwa. Tume imesema kura zizopigwa zilikuwa 8,626,283.


Mshindani mkuu wa Kikwete, ambaye ni mgombea wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alitangazwa kuwa amepata kura 2,271,941 zilizo sawa na asilimia 26.34 ya kura zote halali zilizopigwa.


Katika mpangilio huo, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF alipewa kura 695,667 ambazo ni sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali.


Uchunguzi wa MwanaHALISI umebaini kuwa licha ya tofauti ya matokeo ya vituoni na yale ya NEC, matokeo katika baadhi ya maeneo hayakurekodiwa kwenye karatasi za tume, rasmi kwa shughuli hiyo.


Gazeti hili limeona matokeo yaliyorekodiwa kwenye karatasi za kawaida na magamba magumu ya makasha, ingawa zimegongwa mihuri inayoonekana kuwa ya tume.


Matokeo ya aina hii yanashurutisha kuwepo ujenzi wa shaka juu ya usalama wa kura na uwezekano wa matokeo kugushiwa.


Kwa mfano, katika jimbo la Segerea, mkoani Dar es Salaam, matokeo ya kura za urais yaliandikwa kwenye karatasi ya kawaida ya rangi ya khaki. Karatasi hiyo inaonyesha kuwa imetoka katika kituo Na. B – 2.


Katika kituo B – 4 ambako matokeo yameandikwa kwenye karatasi ya kawaida, CCM imepata kura 90 na CHADEMA kura 55.


Matokeo katika kituo hicho, kwa mujibu wa karatasi hiyo, yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 94 na CHADEMA kura 90.


MwanaHALISI limeelezwa kuwa mbali na kasoro hiyo ya kutokuwapo kwa fomu za kurekodia matokeo, katika baadhi ya majimbo yaliyofanya uchaguzi, majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.


Gazeti hili lilitaka kujua maoni ya Dk. Slaa juu ya taarifa kuwa kuna maeneo ambako majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.


Naye alijibu, "Wewe unazungumzia hilo; matatizo yaliyopo katika uchaguzi huu ni makubwa sana. Kuna uchafu mwingi. Ndiyo maana sisi tunasisitiza kuwa hatuwezi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa."


Amesema, "Tunaendelea kukusanya nyaraka zote za uchaguzi na si muda mrefu ujao, tutaeleza dunia ni kitu gani kilifanyika, wapi na akina nani walihusika. Tutaeleza pia hatua gani itakayofuata baada ya hapa."


Gazeti lina taarifa kuwa baadhi ya majimbo ambako matokeo ya urais hayakutangazwa, ni Kiteto, Segerea, Muheza, Kibakwe, Kinondoni, Ilala na Moshi Vijijini.


"Huku kwetu hatukupewa nafasi ya kushuhudia zoezi la kuhesabu kura. Kazi hiyo ilifanywa na msimamizi wa uchaguzi ambaye alisema kura za rais zitahesabiwa wilayani," anasema John Mrema ambaye aligombea ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia CHADEMA.


Anasema, "Lakini tulipofika katika ofisi ya mkurugenzi wa uchaguzi kule wilayani, tulimkuta msimamizi wa uchaguzi akiwa tayari na matokeo yake ya urais. Tulipomuuliza amepataje matokeo hayo wakati kura hazijajumlishwa, alikasirika na kuamua kuchana karatasi zote alizokuwa nazo."


Akiongea kwa kujiamini, Mrema amesema, kwa ufahamu wake, mpaka sasa matokeo ya urais katika jimbo la Moshi Vijijini hayajatangazwa.


Mbali na kuwapo kwa kasoro za majumuisho, taarifa zinasema zaidi ya majimbo 25 yaliyoshiriki uchaguzi hayakuwa na fomu za matokeo Na. 21 (A) na 24 (A).


Aidha, masanduku 36 yaliyosheheni kura za urais, yalikutwa yamehifadhiwa katika shule binafsi ya Biafra iliyopo katika manispaa ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.


Masanduku hayo yalikutwa yakiwa na karatasi zake halisi za kupigia kura na yalikuwa bado yamefungwa kwa lakiri. Katika orodha ya masanduku hayo kulikuwa na yale yaliyotolewa kwa Kata za Tandale, Makumbusho, Mwananyamala, Kigogo na Hananasif.


Kwa kata ya Tandale yalikuwa na namba: 162452, 162495, 1624586, 162489 na 162401. Makumbusho Na. 161330, Hananasif Na. 16871, 161051, 160958, 160165 na Kigogo Na. 160665.


Kutoka Morogoro, taarifa zinaeleza utata wa aina yake. Kati ya wapigakura 422 waliotarajiwa kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Msufini, kata ya Msufini, manispaa ya Morogoro, hakuna hata mmoja aliyekuwa na shahada ya kupigia kura.


Taarifa hizi ni kwa mujibu wa daftari la wapigakura PDF Na. 00434524.


Katika kituo cha Shule ya Msingi Misufini B – 2, Na. 00006226 kilichopo kata ya Mafinga, kati ya wapigakura 422 ni wapigakura 192 tu ambao walikuwa na sifa ya kupigakura. Hii ni kwa mujibu wa daftari la wapigakura PDF Na. 00434425.


Mbali na kasoro hizo, baadhi ya watu wanaonekana mara mbili katika daftari la wapigakura. Inaonyeshwa pia kuwa wana shahada mbili tofauti za kupigia kura.


Hapa ndipo zinachipuka taarifa zinazodai kuwa kwa kupitia majina hayo, na mengine ya ambao hawakujitokeza kupigakura, ulifanyika uchakachuaji matokeo.


Madai yamezagaa kuwa uchakachuaji kwa njia ya wale ambao hawakujitokeza kupiga kura, ama ulifanyika kupitia mawakala wa vyama vya siasa wasiowaaminifu au wasimamizi wa uchaguzi.


Katika jimbo la Babati Mjini pekee, yamekutwa majina zaidi ya 2,000 ya wapigakura wa aina hiyo. Miongoni mwao ni Ali Khera Sumaye ambaye amekutwa na shahada mbili.


Shahada ya kwanza ya Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama cha NCCR- Mageuzi kabla ya kurejea CCM, ina Na. 12539414 na nyingine ni Na. 49947458. Taarifa nyingine zote za Sumaye, ikiwamo tarehe ya kuzaliwa zinafanana.


Shahada zote mbili zinamuonyesha Sumaye kuwa amezaliwa 17 Agosti 1952. Taarifa zake zinapatikana katika PDF Na. 00400518 ya daftari la kudumu la wapiga kura.


Naye Amina Abdallah Soono anatumia shahada Na. 1255139 na Na. 12557140; Anna Yakobo Masay, shahada Na. 1255831 na 12558205; Elinake Joseah, shahada Na. 26314248 na 49716656 na Jumapili Ramadhani Moromba mwenye shahada Na. 41226061.


Katika orodha hiyo, wapigakura wengine waliokutwa na shahada mbili ni Mariam Saidi Mohamed ambaye shahada zake ni Na. 12566932 na 49773838 na Ibrahim Richard Shalua Na. 32298659 na 12557313.


Taarifa za wapigakura hawa zinapatikana katika PDF, Na.004000518, Na.004000537 na Na. 00400534.


MwanaHALISI limegundua pia kwamba kuna baadhi ya wapigakura ambao majina yao yamekutwa katika daftari la wapigakura, lakini picha zao zinakosekana.


Haijaweza kufahamika iwapo wapigakura wanaoonyeshwa kuwa na shahada mbili walifanikiwa kupiga kura mara mbili au hata zaidi katika uchaguzi uliomalizika wiki iliyopita.


Lakini katika daftari la wapigakura kunaonyesha pia kuwa katika kituo cha Serikali ya Mt. Mbuyuni – 1 Na. 00006218, kata ya Mafisa, wapigakura 57 kati ya 410 hawakuwa na shahada za kupigia kura.


Miongoni mwa ambao hawakuwa na shahada ni Abas Ali Dunda, Abdallah Ali Matoto na Abas Majemba.


Mbali na kasoro hizo, MwanaHALISI limegundua mkanganyiko katika idadi ya walioandikishwa kupiga kura. Kwa mfano, Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kilavu alinukuliwa akisema tume yake imeandikisha jumla ya watu 21,210,187.


Hata hivyo, idadi hiyo ilipungua hadi kufikia wapigakura 19,686,608. Lakini Mwenyekiti wa Tume, Jaji mstaafu Lewis Makame alisema tume yake iliandikisha wapigakura 20,137,303.


Aidha, imefahamika kuwa timu ya wataalamu wa teknoljia ya habari (IT) ya CHADEMA ilitembelea mtambo wa kupokea matokeo ya uchaguzi siku mbili kabla ya uchaguzi.


Katika ziara hiyo, wataalamu hao waligundua kuwa mtambo huo haukuwa umejaribiwa kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa.


"Tulipowaeleza kwamba ni makosa kitaalamu kutojaribu mtambo kama huu, ndipo walipoamua kuujaribu; na mara baada ya kuujaribu, ulikwama palepale," anaeleza Mashinda Mtei, mmoja wa wataalamu wa CHADEMA waliokwenda kukagua mtambo wa NEC.


Anasema wakati wanafanya majaribio waligundua kuwapo kwa kasoro kubwa ya kura za mgombea mmoja kuhamia kwa mgombea mwingine.


Mara baada ya kugundua kasoro hizo, anaeleza Mtei, NEC waliahidi kurejesha Dar es Salaam kompyuta zote zilizokuwa zimesambazwa mikoani na kwamba waliahidi kufanya kazi hiyo na kuikamilisha haraka.


Tume iliahidi kuifahamisha CHADEMA juu ya maendeleo kuhusu kompyuta hizo.


Hata hivyo, katika hali ambayo haijaeleweka, siku hiyohiyo, tarehe 28 Oktoba 2010, Kiravu alimuandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA akikiri kuwapo kwa ujumbe wake katika ofisi za NEC.


Barua ya NEC yenye Kumb. Na. EA.75/162/08/99 ya tarehe 28 Oktoba inasema, "Napenda kukujulisha kwamba jana tarehe 27/10/2010, wataalam wa chama chako wa IT walikuja na kuruhusiwa kukagua mfumo wa kujumlisha kura.


Wataalamu hao waliridhika na mfumo huo na ni matumaini yangu kwamba wamekupatia taarifa kamili."


Barua ya Kiravu ilipokelewa CHADEMA terehe 4 Novemba 2010, siku sita baada ya uchaguzi kumalizika.


Gazeti hili ambalo linaendelea kutunga taarifa za uchaguzi kwa makini zaidi, limeshindwa kumpata Kiravu kueleza mapungufu haya na kwa nini barua kutoka NEC kwenda CHADEMA ilichukua zaidi ya siku tano kuwafikia.


Wakati NEC ikisema wataalamu wa IT waliotumwa na CHADEMA wameridhika na mfumo wa kuhesabia kura, taarifa kutoka ndani ya chama hicho na ambazo zimethibitishwa na Dk. Slaa zinasema wataalamu wake waliupinga mfumo huo kwa maelezo kwamba haufahamiki kwa watendaji wa NEC.


Anasema kuthibitisha kwamba watalaamu wa chama walikuwa sahihi, zoezi la kuhesabu kura za rais na hata kumjulisha kura za wabunge ili kupata idadi ya wabunge wa viti maalum, limechukua zaidi ya wiki moja.


Gazeti toleo na. 214
 
Kweli sisi ni WADANGANYIKA. Yaani tumepokea takataka zote hizi. NAona aibu kuwa Mtanzania.
 
ningependa kujua inachoendelea baada ya ushahidi huu kutolewa, hivi kuna hatua zozote zilizochukuliwa ukiacha ile ya mheshimiwa Slaa?
 
Timing ni kitu cha muhimu sana. Sio watanzania wengi wanaamini kuwa kuna wizi wa kura umefanyika. Hata humu kwenye JF watu walitiana moyo kuwa wizi hauwezekani.
Leo watu wanapoanza kuambiwa kuwa kura zimeibiwa kwa haraka wanaona kuwa CHADEMA wanasema hayo kwa kuwa wameshindwa.

Ukiacha watu waendelee kuamini kuwa ni maneno tu hata utakapokuja na uthibisho lakini unaotolewa baada ya muda mrefu kupita wataona hata huo uthibitisho ni wa kutengeneza na huwezi kuwapata tena.

MAONI YANGU:
Dr. Slaa na CHADEMA kwa ujumla. Toeni mifano michache ya wizi kama niliyoiona kwenye gazeti la Mwanahalisi. Kisha kila mnapozungumzia kutokumtambua rais toeni mfano wa ushahidi mmojawapo kati ya mingi inayoweza kuwepo.

Endapo mtatoa mifano michache kisha mkaonyesha kuwa bado mnaendelea kukusanya takwimu na ushahidi basi watu wataamini na wao watangojea ushahidi wenu.

Katika gazeti la Mwanahalisi walipoandika juu ya wizi wa kura, wao pia hawakufafanua walitoa tu mfano wa majimbo mawili ( au vituo viwili tofauti) na matokeo yake yalikuwa yanafanana kwa wagombea wote kupata kura zinazofanana kwa kila mgombea. Alichopata Kikwete, Slaa, Lipumba. Mziray, Dovutwa, Hashim, nk

Matokeo yao yalikuwa yaleyale yaliyoonyeshwa kwenye upande mwingine.

Mwanahalisi hawakusema kama hayo maeneo yaliyotajwa yako katika mkoa mmoja au ni vipi. Pia hawakufafanua juu ya matokeo hayo yaliyoandikwa kuwa yanafanana hadi mchunguzi mwenye muda aone mwenyewe.

Wanasema ukitaka kuficha kitu kwa mwafrika kiweke kwenye maandishi. Watu wengi hawajisumbui kutafuta habari au kuchunguza kilichojificha. Ndio maana mfumo wa siasa za Tanzania haupati shida ya kuharibu mambo kwani watakaojitesa kuchunguza sio wengi.

Naomba hapa tuweke mifano michache ya kweli kutoka vyombo vya kuaminika au picha kabisa ya fomu iliyobandikwa mahali na ikatofautiana na matokeo halisi.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
MwanaJF Mtaka Haki umenena!! Ila mie nashauri data hizi zitolewe kama support facts katika hoja bungeni za CDM kudai Tume Huru, na Katiba mpya!!!!!!!!!! Hapo zitakuwa zimeingia katika Hansard na ktika mkondo wa sheria na siasa-hapa ndipo impact yake ndani na nje ya nchi itazaa matunda!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Hii kitu ifanyike very strategically! Mpambanaji Tundu Lisu na jopo lako la wanasheria huu ni ushauri kwenu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Hongera Kamanda Freeman tulikouna ukiongoza jahazi kutoka nje-JK alijikaza tu lkn ujumbe ulifika!!!!!!!!!!!!!!!!
 
I strongly support your idea. Tungependa tupewe ushahidi maana huko vijijini wanalalamika kuhusu kukaa kimya kwa Dr. Slaa. Ajitokeze awaambie wananchi jinsi alivyoibiwa kura.
 
Mnayoyasema ni ya kweli bila ya kuchukua hatua za haraka kutekeleza suala hilo ccm itauteka huo mjadala wa wizi wa kura na suala la udini kwenye uchaguzi.

Tangu JK agusie suala hilo katika hotuba yake tayari baadhi ya viongozi wa chadema wamekwisha ingizwa kwenye mkenge; leo hii nimemsikia Zito Kabwe kwenye TBC Taifa, akiunga mkono dai la JK ya kuwa uchaguzi uliopita ulighubikwa na udini. Na akuishia hapo, bali pia alipendekeza uanzishwe mjadala wa kitaifa kuzungumzia suala hilo.

Hivi tujiulize hayo ni mawazo yake Zito au ni kipaza sauti tu wa CCM?
 
Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kuispin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomba kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita.

Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi.

Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Na kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena.


Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa. Hata hivyo, baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP.

Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo: Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao.

Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari.

Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa na uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba).

Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137) Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.

148853_462188548852_533398852_5518680_3788151_n.jpg




HONGERA WABUNGE WA CHADEMA HONGERA KIUNGO MCHEZESHAJI BABA MBOWE, TUNDU LISSU, VITI MAALUMU WOTE, SHIBUDA, ZITTO, MNYIKA, AKUNAAY, PRFO KAHIGI, SUGU, VINCENT NYERER, GOD LEMA, ARFI, NA WENIGNE WOTE KWA KUWAKIRISHA VEMA PIPOZ POWER HATA KAMA BAADHI YENU HAWAKUPENDA ILA MMETUTOA KIMASOMASO SASA NEXT STEP INTERNATIONAL COMMUNITY AND WATANZANIA WOTE WAJUE -SMABAZA HII KWA WATANZANIA WOTE HATA CCMhttp://www.facebook.com/ajax/share_dialog.php?s=4&appid=2347471856&p[]=533398852&p[]=167384616627783
 
Na hata Dr. King is not all he is cracked up to be in the first place.

But you can't compare Dr. Slaa to Dr. King by any measure.....Dr. King was an intellectual giant, a philosopher, Nobel peace prize lareate, and an orator, among many other things.............

Dr. King is in a different league compared to Dr. Slaa......and I dare say it, that it is somewhat insulting to compare the two!!!!!
 
And all these do not make sense to Thito! Used to be indeffernt with this gentlemen, slowly is getting too much on me, For sur hate him
 
UFAFANUZI ZAIDI TOKA KWA DR SLAA KUHUSU MTILILIKO MZIMA WA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI NA KUSUSIA HOTUBA YA NDUGU KIKWETE


by George Maige Nhigula Jr on Saturday, November 20, 2010 at 11:18pm

Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kuispin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomba kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Na kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa. Hata hivyo, baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo: Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari. Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa na uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137) Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.

148853_462188548852_533398852_5518680_3788151_n.jpg



HONGERA WABUNGE WA CHADEMA HONGERA KIUNGO MCHEZESHAJI BABA MBOWE, TUNDU LISSU, VITI MAALUMU WOTE, SHIBUDA, ZITTO, MNYIKA, AKUNAAY, PRFO KAHIGI, SUGU, VINCENT NYERER, GOD LEMA, ARFI, NA WENIGNE WOTE KWA KUWAKIRISHA VEMA PIPOZ POWER HATA KAMA BAADHI YENU HAWAKUPENDA ILA MMETUTOA KIMASOMASO SASA NEXT STEP INTERNATIONAL COMMUNITY AND WATANZANIA WOTE WAJUE -SMABAZA HII KWA WATANZANIA WOTEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE HATA CCM Share
 
Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala.
Duh! jamani hivi kweli Bongo tunatumia mfumo gani huu wa demokrasia?..Kama kuna vituo ambavyo hadi leo hesabu yake haijatolewa, inawezekana vipi NEC kumtangaza mshindi hali hawana hesabu kamili ya kura zote zilizopigwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom