Elections 2010 Hivi ndivyo wizi wa kura ulivyofanyika!

Siyo lazima NEC wasubiri matokeo ya miji midogo kutangaza matokeo. Kama population ni ndogo, na namba za watu waliopiga kura haziwezi kufikia zile ambazo tayari zimeshapigwa, NEC wanao uwezo kutangaza matokeo bila ya kusubiri hayo matokeo. Is all about Mathematics.

I thought it was about procedures and following the constitution! I did not know that is all about mathematics... and what kind of mathematics were applied!? 2+3=10? or?!! explain to pipo please.
 
Superman, unafikiri hata kama Chadema ingeweza kutoa matokeo yote na ushahidi wote basi watu wangekubaliana kuwa ushindi wa CCM una mashaka? Tarehe 3 Novemba wakati Dr. Slaa ametoa wito kuwa kuna tofauti za kura na akatolea mfano wa jimbo moja tu la Geita isingetosha kuwafanya Tume wasitishe na kusikiliza? Leo hii yametolewa majimbo mengi zaidi na baadaye yatatolewa zaidi unafikiri wana CCM na mashabiki wao watakuja na kusema "tupitie kura zote ili Rais wetu asionekane kabebwa"? Really?


Hapa the only point is to make NEC better ready for 2015 "Thats why nashauri wacompile evidence zote na story A to Z na kitungwe kitabu kigawiwe bure Tanzania na Nje ya Tanzania Mwanakijiji with your journalistic background am sure you can compile a book kwa kuhihusisha chedema and with proper evidence ofcourse
 
Hapa the only point is to make NEC better ready for 2015 "Thats why nashauri wacompile evidence zote na story A to Z na kitungwe kitabu kigawiwe bure Tanzania na Nje ya Tanzania Mwanakijiji with your journalistic background am sure you can compile a book kwa kuhihusisha chedema and with proper evidence ofcourse

Wabongo kwa kupangia kazi wenzetu tu hatujambo. Utafikiri Mwanakijiji nchi ndiyo yake sisi wengine ni watakia heri tusio raia ambao haturuhusiwi kushiriki.

Basi hivi hivi hata mabadiliko tutaachia watu fulani tu kutokana na "backgrounds" zao. Ndiyo maana mabadiliko yanakuwa magumu, kila mtu anamtegemea fulani. Vipi kama tungekuwa na wanavijiji kadhaa wanatokea kila mwezi ?
 
Wabongo kwa kupangia kazi wenzetu tu hatujambo. Utafikiri Mwanakijiji nchi ndiyo yake sisi wengine ni watakia heri tusio raia ambao haturuhusiwi kushiriki.

Basi hivi hivi hata mabadiliko tutaachia watu fulani tu kutokana na "backgrounds" zao. Ndiyo maana mabadiliko yanakuwa magumu, kila mtu anamtegemea fulani. Vipi kama tungekuwa na wanavijiji kadhaa wanatokea kila mwezi ?

Kuna kitu kinaitwa Specialization Mkuu, Kila kitu kinahitaji expertisim, am sure when it comes with journalism na uandishi MKijiji ananiacha mbali and am not talking about the IQ and thinking capacity bali his journalistic contacts and all that kwake ni rahisi kupata hizo evidence kuliko mimi and likewise it is easy kwake kuonge na dr Slaa et al . kuliko mimi.... Amigo tusipigane am sure we are fighting the same war
 
Mkuu unapoona ukweli wa aina yoyote ile unachakachuliwa lazima uuweke sawa. Uchakachuaji wa ukweli kuhusu kumlinganisha Dr. King na Dr. Slaa ilibidi usahihishwe kwanza kisha tuendelee na mjadala. Tukirudi kwenye mada kuu: Kosa moja goli moja - kosa lilifanyika siku ya kuhesabu kura ambapo watu walijikita kufuatilia na kulinda kura za Ubunge na kusahau za Urais japo walikumbushwa sana hadi humu jamvini! Kilichobaki sasa ni kutorudia kosa kwa kuanza kujenga mazingira ya kuziba mianya yote ya uchakachuaji kati ya sasa na 2015. Nawasilisha.

Nimekusoma mkuu na kweli tulijisahau..
 
Asante kwa post yako. Ingekuwa ni vyema data zote ziwekwe wazi ili watanzania wajue kilichojiri. Bila kuonyesha haya mapungufu wote tutadhania mfumo wa mwaka huu ulikuwa safi na hivyo utaendelea kutumika katika chaguzi zijazo!

Tunaamini kama mapungufu yataonyeshwa basi hata move ya kubadili katiba especially kuhusu kuhoji matokeo ya Urais itapata kuungwa mkono na watanzania wengi. Mungu ibariki Tanzania!
 
Duh! jamani hivi kweli Bongo tunatumia mfumo gani huu wa demokrasia?..Kama kuna vituo ambavyo hadi leo hesabu yake haijatolewa, inawezekana vipi NEC kumtangaza mshindi hali hawana hesabu kamili ya kura zote zilizopigwa?

Labda kwake yeye ni kuwa hadi matokeo yawe rasmi ni pale yatakapokuwa katika website ya NEC na sio yanapotangazwa kwa mdomo na NEC....Kama walivyosema...

Lakini pia kama tofauti ya kura ambazo hazijatangazwa hazifiki hata asilimia moja ya kura zote, ni jambo la ajabu ama kinyume cha katiba na sheria ama hata rationale kumtangaza mgombea kushinda uchaguzi??? Na kama huu ndio ushahidi walioweza kuupata baada ya wiki mbili sasa...something is very wrong hapa tulipo na huko tuendako


Nimesoma huu ushahidi tangia ijumaa na kuurudiarudia na ndio nikang'amua kwanini CHADEMA walisepa kuongea na waandishi wakati ule wa mwanzo na kwa nini asilimia temanini ya wabunge wazoefu wakiwemo viongozi wakuu wa chama, waasisi na hata makambanda wa kampeni hawako pamoja katika hili la kutomtambua RAIS na zaidi hili la kumsusia akifungua rasmi bunge.......
 
To Mwanakijiji; so umekubali responsibility ya ku compile kitabu kuhusu huu wizi, myself tachangia gharama na kukisambaza bure mitaani
 
Kuna kitu kinaitwa Specialization Mkuu, Kila kitu kinahitaji expertisim, am sure when it comes with journalism na uandishi MKijiji ananiacha mbali and am not talking about the IQ and thinking capacity bali his journalistic contacts and all that kwake ni rahisi kupata hizo evidence kuliko mimi and likewise it is easy kwake kuonge na dr Slaa et al . kuliko mimi.... Amigo tusipigane am sure we are fighting the same war
No, your fighting different war
 
To Mwanakijiji; so umekubali responsibility ya ku compile kitabu kuhusu huu wizi, myself tachangia gharama na kukisambaza bure mitaani

Ndg usihangaike.....

Hata ukitaka matokeo ya urais katika yale majimbo waliyoshinda tu ninawasiwasi kama sio uhakika hawatakuwa nayo............No wonder hizi disastrous moves kwani hawako tayari kuwa wanamapungufu ambayo wanapaswa kuyakubali, kuyajadili na kyatumia kama kioo cha jinsi gani wanajipanga vyema kuanzia sasa................

Mwanakijiji anajua hilo ndio maana anakwepesha jukumu hilo kama ambavyo anavyospin hapo juu...........
 
This is very sad... for what i have seen hapa Jamvini kwa muda wangu mfupi now tkribani mwezi hivi ..... we are very good at Taliking the Talk lakini when it comes to Walk the Walk ...... ..........:noidea:
 
Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kuispin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomba kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita.

Mlolongo wa maneno haya unanipa picha kuwa hii sio kauli ya Dr Slaa mwenyewe isipokuwa ni kazi ya Mwanachadema mwenye access ya ID ya Dr Slaa na ambaye amechukua tarifa iliyoandaliwa na chama na kuiweka hapa akimanisha kuwa ni maandiko ya Dr Slaa

Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi
.

Ni majimbo yapi hayo na uko wapi ushahidi wenu ikiwemo karatasi za matokeo ambazo mlipaswa kuwa nazo kutoka kwa ama wagombea wenu ama mawakala wenu……

Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.

Kama hayajahesabiwa yameathiri nini matokeo ya uchaguzi ambayo Chadema na Dr Slaa hataki kuyatambua?

Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Na kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena.

Naamini hapa NEC wana wajibu wa kutoa ufafanuzi…..

Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa. Hata hivyo, baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP.

Itakuwa vyema kuirudia taarifa hii na kufanya editing ili ieleweke hapa

Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena.

Huu ni ushahidi kuwa maamuzi ya CHADEMA yamejigubika katika predetermined assumptions kuliko collected facts….hatari kwa mustakabali wa chama na taifa kwa ujumla

Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo: Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao.

Nchi ibaki na leadership vacuum ili kuridhisha hisia na tofauti za kisiasa ama kimitazamo……..

Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo.

Wananchi waliingi mitaani kama matokeo ya kuaminishwa kuwa CHADEMA ni lazima wameshinda na CCM ni lazima wataiba hivyo mapungufu madogo yote yaliweza kutafsiriw kama jitihada za wizi. Na hisia hizo ndizo zimechangia sana wengi wanaopenda mabadiliko kutokwenda kupiga kura kwani walishaminiswa kuwa kura zao hazitakuwa na impact kwani CCM ni lazima wataiba…….

Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari.

Si kweli kuwa Chadema kama chama ama viongozi wake wote walifanya jitihada za kuwasihi wananchi ama wafuasi ama washabiki wao wasiingie mirtaani. Kuna ushahidi kuwa baadhi y viongozi wa juu wa Chadema walifurahia hilo na wengependa liendelee kwani litawafanya waendelee kuwa relevant n haswa wale walioshindwa. Lakini pia kuna ushahidi kuwa badhi ya wagombea kwa mfano kule Mwanza walitumia nyumba na viongozi wa dini kuchochea vurugu mitaani ili kuhakikisha "wanalinda" kura…..Yaleyale ya ODM kule Kenya…..

Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za

Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa).
Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000).
Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa na uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi)
Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taarifa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba).

Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137) Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu.

Moja, ni jimbo lipi kati ya haya bado matokeo ni tofauti na je uwapi ushahidi wenu yaani matokeo rasmi yaliyosainiwa na mawakala ama wagombea wenu yanayonyesha kura tofauti na zile rasmi hadi sasa??

Lakini pia ukijjumuisha kura tofauti za kura hapo juu kama mnavyodai, je zinafika ama kuongeza asilimia ngapi ambzo zinaweza kugeuza matokeo kiasi cha kufuta matokeo?

Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.
Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. (Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.

Tafadhalini, akili ya kawaida mening layman or sometimes mediocre thinking/analysis/understanding haiwezi kuwa msingi wa maamuzi makubwa kitaifa kama haya mliyochukua na mnayotaka watu kuwaunga mkono……….
 
Hata kichwa cha mada ni sehemu ya hoja vilevile......
Haswaa! Kichwa ndio kitambulisho cha kiwiliwili :teeth:

Inategemea na mfananishaji, nimeshawahi kuona mtu (hakuwa mtoto) akifananisha mbwa na kondoo!!! Hivyo basi sishangai mtu akifananisha visivofanana!! TATIZO uchakachuaji umezidi kila mmoja anavutia kwake kiasi kwamba sasa hatuelewi nini kweli na nini uongo!!!!!!

Na kote kunachakachuliwa mpaka jamvini kuna uchakachuaji wa posts! hivyo basi tuusubiri muda uamue UKWELI uliposimamia kwani kila jambo lina msimu wake. HUU NI MSIMU WA UCHAKACHUAJI :teeth::teeth:
 
Siyo lazima NEC wasubiri matokeo ya miji midogo kutangaza matokeo. Kama population ni ndogo, na namba za watu waliopiga kura haziwezi kufikia zile ambazo tayari zimeshapigwa, NEC wanao uwezo kutangaza matokeo bila ya kusubiri hayo matokeo. Is all about Mathematics.
Mkuu wangu sivyo inavyokwenda... Vituo vya habari au watabiri na hata kambi ya CCM wanaweza kutangaza ushindi pasipo hesabu iliyobakia, wakijua kwamba haiwezi kubadirisha matokeo lakini chombo cha mwisho kama NEC hakitakiwi kutangaza matokeo pasipo kuwa na uhakika kwa asilimia 100 kwa sababu mbali na hizo kura chache zilibakia inawezekana pia kuna makosa ya uhesabuji au makosa mengine yeyote yanaweza kutokea hivyo maadam chombo hiki ndicho cha mwisho na chenye kutoa tamko la mwisho ni lazima wawe na hesabu zote zilizothibitishwa.

Hawawezi kusema JK ameshinda kwa asilimia 61 wakati hizo kura zinaweza kumpa asilimia moja nyingine hivyo kufanya ushindi wake kuwa asilimia 62 au hata asilimia 70 - who knows!. Mimi nadhani swala la uchakachuaji linapingwa sii kwa sababu JK ameshinda, isipokuwa ni kupotoshwa kwa makusudi demokrasia ambayo pengine ingeonyesha JK kashinda kihalali kwa asilimia ngapi, na ni kutokana na mapungufu hayo kumepelekea wasiwasi kwamba pengine kashindwa na ndio maana kumetokea uchakachuaji.

Nakumbuka enzi zetu tukisoma mwalimu akikukata maksi inauma vibaya sana na wakati mwingine ukifanya malalamiko na karatasi yako ikapitiwa upya unaweza kutoka ktk ushindi wa pili na kuwa wa kwanza au hata kama ulikuwa wa mwisho ikakupa nafasi ya pili toka mwisho. Ni ile hali ya kujua umefika wapi ndio haki ya kipimo bora cha mtihaniwa.

Kinachotakiwa ni Uhalali wa matokeo kwani kuwapa NEC madaraka ya refa wakati refa huyo ni mwajiriwa na team inayocheza sidhani kama mpira utachezwa na inabidi wakati mwingine tuwe wakweli tusizidanganye roho zetu kwa mapenzi na ushabiki wa chama. NEC wamechemsha vibaya sana na tatizo lenu imekuwa kwamba ikisemwa NEC basi lazima inasemwa CCM, hapo mnashindwa kutofautisha.

Kifupi kama unakumbuka niliwaonya Chadema kuwa makini sana na uchaguzi huu hasa ktk hesabu za Dr.Slaa na uchakachuaji wakasema wamejizatiti kwa umakini ktk vituo vyote na watahakikisha hakuna njia ambayo NEC au CCM wataitumia kuiba kura za Dr.Slaa. well imetokea kama nilivyosema kuhusu CUF na uchaguzi wa Zanzibar, leo wameambulia Umakamu wa rais na wizara sizizokuwa na nguvu kupelekea mageuzi yeyote ya kisera.
 
Kwa kweli huwezi amini hata kura za wanachi wanazipora, maana tumeshazoea wa achukua madini, wanyama na Magogo, mafisadi kiboko.

Ila mimi naamini iko siku watatoka maana wanaoisumbua nchi hata kumi hawafiki wengine bendera fuata upepo, tunabanana kwenye daladala, foleni za hospital, Matatizo ya maji, Ukata vile vile,
 
Dr tumekuelewa asiyetaka kukueewa huyo hana uchungu na nchi yetu lakini mungu atafanaya kizazi juu ya wote waliofanya hivyo. Na atarejeshe heshima katika taifa hili
 
Changia mada achana na mambo ya ulinganisho, Martin Luther alikuwa kwa ajiri ya wamarekani na si watanzania. Changia mada iliyowekwa juu
 
Duh! jamani hivi kweli Bongo tunatumia mfumo gani huu wa demokrasia?..Kama kuna vituo ambavyo hadi leo hesabu yake haijatolewa, inawezekana vipi NEC kumtangaza mshindi hali hawana hesabu kamili ya kura zote zilizopigwa?

Mkuu Mkandara,

Matokeo kutokuingizwa kwenye website ya NEC haina maana hayajatangazwa. Matokeo ya ubunge yalikuwa yanatangazwa kwenye wilaya husika na wasimamizi wa majimbo hayo pamoja na mawakala wa vyama wanayo matokeo hayo.

Kuingizwa kwenye website ilikuwa ni kazi ya ziada kuongeza transparency na kutunza records na ilikuwa haina uhusiano na kutangazwa kwa matokeo ya ubunge.

Hivyo hivyo kwenye matokeo ya urais, matokeo yote yalishatolewa na hata hapa JF yapo ingawaje kwenye website kuna baadhi ya wilaya hawajaingiza entries zake.
 
Back
Top Bottom