Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Hawa ni baadhi ya wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA. Elimu ni muhimu ndio maana nimeona ni vyema mkafahamu viwango vya elimu vya viongozi ambao kesho na kesho kutwa tunatarajia wawe wawakilishi wetu katika medani za kitaifa na kimataifa:

1) Godbless Jonathan Lema -- BBA, ST Augustine --- Amevuliwa ubunge kwa sasa, kesi inaendelea.
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level, Degree bible college.
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education, Masters in theology.
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary, Certifcate from Monduli Teachers college
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

CV ya 'DR' WILBROD SLAA HII HAPA:
Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung'unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.

Kama mawaziri watatokana na wabunge, basi CHADEMA inaweza kuwa na wabunge ambao kielimu wanaweza kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yao.

Indhari:
Chanzo cha taarifa hii ni kutoka kwenye web site ya bunge. Therefore, kama kuna kosa lolote unaweza kusahihisha. Si lengo kupotosha.

UJUMBE:
Tusidharau elimu wakati wa kuteua wagombea kuwakilisha watanzania.

WITO:
Tupeleke mapendekezo katika CRC ya kutaka mawaziri wasitokane na wabunge, kwa vile inaweza kuja kuwa tatizo kupata wabunge walio na sifa za kuongoza wizara.

wewe bayana kuwa mfuatiliaji wa mambo, hata chadema ikiingia madarakan inapingana na uataratibu wa mawaziri kutokana na wabunge, hivyo hoja yako hasa cjaielewa
 
Nijuavyo elimu haipatikani darasani tu, kuna wasomi waliobobea lakini ni bure kabisa. Kuna michango na mawazo ambayo hutolewa na wenye shahada za elimu Bungeni hadi nashangaa.

Juzi juzi alipokamatwa Sheikh Ponda, msomi mmoja mbobevu na mwanasiasa, alinishangaza sana kwa maoni aliyoyatoa.
 
Unajua USA ina marais wangapi ambao hata hawakuwa na diploma?

Ok hao wenye degree zao walioko CCM na serikalini si ndio wametufikisha hapa tulipo hoi bin taaban? Je hizo elimu zao (Chenge ana digirii ya Harvad) zimelisaidiaje hii nchi mpaka sasa?

Huwezi kutumia kigezo kimoja au viwili linapokuja suala la uongozi, iwe wa jumuiya, chama au nchi.
 
Mbona mnapenda kupotosha umma Lema hajawahi kusoma ST AUGUSTINE UNIVERSITY wala Wenje naye hajawahi kusoma.
Cc to.. Ngongo,
 
Last edited by a moderator:

Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.

Kwani sifa za kupitshwa, kugombea, na hatimaye kuchaguliwa kuwa mbunge au Rais ni zipi? Ni zipi kati ya hizo ambazo wagombea wa Chadema hawakuwa nazo?

Si wanajaza mafomu kibao ya NEC na michakato mingi kufanywa na NEC kabla ya kupitishwa hawa? Hivyo basi, kama kuna wagombea waliopitishwa (na serikali chini ya NEC) kwa sifa ambazo ni batili basi hao waliowapitisha ni wa.pu.mba.vu kuliko hao waliopitishwa.

Je, unailamu serikali yako chini ya CCM kwamba ni serikali na chama cha wa.pu.mba.vu? Fikiria mara mbili mbili kabla ya kuposti hoja hapa.
 
Jamani tusitetee ujinga kwa vile wanaoguswa tunawashabikia. Mambo ya elimu haipatikani darasani US iliongozwa na marais wasio na diploma yamepitwa na wakati. Elimu ni muhimu tutake tusitake.

Hivi nani yuko tayari kwa mfano kuongozwa na rais asiyejua kusoma na kuandika katika karne ya 21? Sasa mnatetea nini hapa? Angekuwa ameandikwa Salma Kikwete kama kihiyo hapa kila mmoja angehanikiza kumtaka asome.

Mie nadhani wabunge wa CDM ambao Resumes zao haziko safi wanapaswa kwenda shule. Bila kusoma watapitwa na wakati. Mfano Mbowe aliwahi kuwa admitted Hull University. Je ni kwanini hakumaliza masomo yake? Alifeli, alikuwa na udhuru?
 
Unajua USA ina marais wangapi ambao hata hawakuwa na diploma? Ok hao wenye degree zao walioko CCM na serikalini si ndio wametufikisha hapa? Je hizo elimu zao (Chenge ana digirii ya Harvad) zimelisaidiaje hii nchi mpaka sasa?

Huwezi kutumia kigezo kimoja au viwili linapokuja suala la uongozi, iwe wa jumuiya, chama au nchi.

Chalii angu usifananishe Tanzania na Marekani hata siku moja. Bora ungefananisha Tanzania na Burundi, Malawi. Zambia.
 
Hawa ni baadhi ya wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA. Elimu ni muhimu ndio maana nimeona ni vyema mkafahamu viwango vya elimu vya viongozi ambao kesho na kesho kutwa tunatarajia wawe wawakilishi wetu katika medani za kitaifa na kimataifa:

1) Godbless Jonathan Lema -- BBA, ST Augustine --- Amevuliwa ubunge kwa sasa, kesi inaendelea.
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level, Degree bible college.
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education, Masters in theology.
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary, Certifcate from Monduli Teachers college
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.

Kama mawaziri watatokana na wabunge, basi CHADEMA inaweza kuwa na wabunge ambao kielimu wanaweza kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yao.

Indhari:
Chanzo cha taarifa hii ni kutoka kwenye web site ya bunge. Therefore, kama kuna kosa lolote unaweza kusahihisha. Si lengo kupotosha.

UJUMBE:
Tusidharau elimu wakati wa kuteua wagombea kuwakilisha watanzania.

WITO:
Tupeleke mapendekezo katika CRC ya kutaka mawaziri wasitokane na wabunge, kwa vile inaweza kuja kuwa tatizo kupata wabunge walio na sifa za kuongoza wizara.

hebu weka na cv yako ili tujue uwezo wako wa kuchambua mambo kabla hatujaukubali au kuukataa umbea wako
 
wewe bayana kuwa mfuatiliaji wa mambo, hata chadema ikiingia madarakan inapingana na uataratibu wa mawaziri kutokana na wabunge, hivyo hoja yako hasa cjaielewa

Hii itafanikiwatu kama kwenye katiba mpya kutakuwa na upeo mkubwa zaidi wa kuteua mawaziri
 
Mkuu Bayana

Unaweza Kutuwekea CV za Viongozi wa Chama chako cha ADC utakuwa umebalance Mjadala
 
Last edited by a moderator:
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom