Hivi ndivyo vigezo vya udahili wa wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2015

CompaQ

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
281
250
WARAKA WA ELIMU NA. 3 WA MWAKA 2015 KUHUSU VIGEZO VYA UDAHILI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO


1.0. Utangulizi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatoa Waraka kuhusu vigezo vya kudahili wanafunzi wa Kidato cha Tano iii kuwaongoza wamiliki wa Shule za Sekondari zenye Kidato cha Tano katika kudahili wanafunzi wa Kidato cha Tano, mwaka 2015. Waraka huu utatumika kwa shule zote, yaani za Serikali na zile zisizokuwa za Serikali.

2.0. Vigezo vya Jumla ya Udahili wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Tano (K5) Katika kudahili wanafunzi wa Kidato cha Tano, vigezo vifuatavyo vya jumla vitatumika:


i. Ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha 'Credit', (yaani A, B+, B au C) katika Mtihani wa Kidato cha Nne, na ii. Ufaulu usiopungua Daraja la 'Credit' au 'GPA' ya 1.6 katika Mtihani wa Kidato cha Nne, na iii. Ufaulu usiopungua Gredi D kwenye masomo yote ya tahasusi.

AU
iv. Ufaulu wa masomo matatu (3) ya tahasusi kwa kiwango cha 'Credit' bila kujali daraja alilopata mtahiniwa kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne.

3.0. Taratibu za Udahili
i. Wanafunzi watadahiliwa kwa ushindani kulingana na nafasi zilizopo katika shule. Hata hivyo, wakati wa zoezi la udahili, kipaumbele kitolewe kwa: a. wanafunzi wa kike; b. wanafunzi wenye mahitaji maalum, na c. michepuo ya Sayansi, Teknolojia na Hisabati

ii Udahili katika shule za umma utaanza na wanafunzi wa kujiunga na shule za sekondari za Kitaifa na watakaobaki watachaguliwa kulingana na uwezo wa shule nyingine zilizopo.

iii. Udahili kwa shule zote za umma utafanywa katika kikao kitakachoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.

iv. Wanafunzi wenye sifa linganishi (ambao matokeo ya mitihani yao siyo ya Baraza la Mitihani la Tanzania) wataomba udahili kwa kutumia matokeo ambayo yamehakikiwa na kukubaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwamba alama za mwanafunzi alizopata zinalingana na alama zilizotamkwa katika Waraka huu kwa ajili ya udahili.

Waraka huu unafuta Waraka Namba 1 wa mwaka 2014 na unaanza kutumika kuanzia tarehe 01/03/ 2015.

Prof. Eustella P. Bhalalusesa KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani Tanzania,
S.L.P. 2624, DAR ES SALAAM.
 

Mnyalu Junior

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
572
225
Thank you very much. Ila kuna kitu najiuliza, wenzangu mmepataje hiyo link? Coz ukiingia kwenye website ya wizara ya elimu na ukadownload attachment waliyoweka unakuta ni barua ya mwaka 2013 kuhusu uchangiaji wa gharama za ukaguzi wa shule. Asiyeamini aingie kwenye website ya wizara ya elimu na adownload hiyo attachment aone
 

Mnyalu Junior

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
572
225
Thank you very much. Ila kuna kitu najiuliza, wenzangu mmepataje hiyo link? Coz ukiingia kwenye website ya wizara ya elimu na ukadownload attachment waliyoweka unakuta ni barua ya mwaka 2013 kuhusu uchangiaji wa gharama za ukaguzi wa shule. Asiyeamini aingie kwenye website ya wizara ya elimu na adownload hiyo attachment aone

Thanks, washarekebisha na kuweka attachment sahihi
 

moghasa

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,018
2,000
wakuu vipi kuhusu wanafunz waliorisiti mwakajana ambao wanavyet vya zaman je, wanaruhisiwa kuunganisha vyeti vyenye mifumo miwili tofaut!!?
 

john watson

Senior Member
Apr 28, 2015
152
225
jaman sasa kama me nimepasi masomo ya sayansi kwa sana lakini upande wa kombination zimesumbua nina gpa 1.6 naweza kuchukuliwa hapo kweli.
 

Hillscka

New Member
Jun 16, 2017
1
20
Jamani naomba kuuliza, ivi unaweza ukasoma combination ya science kwamfano CBG bila ya uwepo wa physics katika cheti chako cha frm4????
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom