Hivi ndivyo utawala wa imla(dictatorship) unavyopandikizwa

luteadam

Member
Aug 10, 2015
71
60
"Julai 2016 ulikuwa mwezi wa kuwaza sana aisee. Haya niliandika Hivi: Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla

1 Pambana na ' matajiri ' ili kuweka matajiri wako wapya watakaokuwa msaada kwako. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana. Hitler yeye aliamua kuwaua Jews kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani

2 Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya lazima uwe na watu wako. Rais Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB.

3 Kudhibiti vyombo vya habari. Rais Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali na ilikuwa marufuku DUMA kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV.

4 Kudhibiti Vyama vya Siasa. Hitler alifuta vyama vyote Ujerumani. Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka.

Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema.

Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Kagame hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Lee Kuan Yew na Mahathir ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals."- *Zitto Kabwe.*
 
The guy is so obsessed with pet construction projects only,maybe for a reason.
He always braying about airplanes,railways and construction projects
He pays absolutely no attention to the main employer....Agriculture
No attention to job creation at all unless one thinks the mythical nchi ya viwanda is a reality
[HASHTAG]#twafaa[/HASHTAG]
 
Wakati wengine tukitoa ya moyoni mapema kabisa, kuna watu walitudhihaki sana. Sasa nafahamu kwamba kuna fast learners na laggards
 
Jisahau tu..... afu uanze kuandika ukiomba msaada unaonewa....

Si ndo zeenu... km yule wa UDSM munaaanzisha harakat afu njaa kali... ukitikiswa tu uko hoi...

Ongea tu acha uoga
 
Back
Top Bottom