Hivi ndivyo unavyouzwa bila hata ya wewe mwenyewe kujua

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Rafiki yangu mpendwa,

Ushauri mmoja mfupi ambao nimekuwa nautoa sana na ambao naamini kila mtu akiuelewa dunia itakuwa bora sana ni huu; HAKUNA KITU CHA BURE.

Kila kitu kina gharama ambayo inaingia katika kukiandaa. Na kwa hii dunia ya kiuchumi ambayo tunaishi, gharama hizo zinapimwa kwa muda, juhudi na fedha.

Hakuna kitu chochote kile kinachoweza kupatikana bure. Hivyo unapoona kuna kitu unapata bure, jua wazi kuna namna unalipia bila wewe kujua au kuna wengine wanalipia kwa niaba yako.

Hili linatuleta kwenye njia kuu za mawasiliano tunazotumia sana kwenye zama hizi, ambazo kuu ni mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na WhatsApp.

Mitandao hiyo imekuwa inajinadi ni ya bure kabisa, kwamba huwalipi wenye mitandao ndiyo uweze kuitumia. Ni wewe tu kujiandikisha na kuanza kutumia mitandao hiyo.



Lakini cha kushangaza sasa, mitandao hiyo hiyo unayoaminishwa ni ya bure, ndiyo imezalisha matajiri wakubwa duniani.

Mark Zuckerberg ambaye ni mkurugenzi wa kampuni inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram, WhatsApp na mingine, yupo kwenye kumi bora ya matajiri duniani.

Huyu ni mtu ambaye hajawaji kuwa na kazi au biashara ya aina nyingine nje ya mitandao hiyo ya kijamii.

Nini kinaendelea hapo?

Iweje mtu anayetoa huduma ya bure awe pia ndiye tajiri mkubwa duniani?

Unapojiuliza maswali hayo na kutafakari kwa kina, ndiyo unaona ukweli ambao umekuwa unafichwa kwa muda mrefu.

Ukweli ni kwamba, mitandao ya kijamii siyo bure kama inavyojinadi.

Na mbaya zaidi, mitandao hiyo imekugeuza wewe mtumiaji kuwa bidhaa ambayo inauzwa.

Ndiyo, utajiri mkubwa ambao mitandao ya kijamii imetengeneza, unatokana na kuuza umakini wa watumiaji wa mitandao hiyo.

Hivyo dili liko hivi;
Wanasema kutumia mtandao wao ni bure, na watu wanakimbilia kwa sababu wanapenda vya bure.
Wanateka umakini wa watumiaji hao kwa kuhakikisha wanatumia mitandao hiyo kwa muda mrefu.
Wanakusanya taarifa za watumiaji hao na kuziuza kwa wale wanaotaka kutangaza biashara zao.

Unajionea hapo mwenyewe, kwamba kwa matumizi yako ya mitandao ya kijamii, umegeuzwa kuwa bidhaa ambayo inauzwa, bila ya wewe kujua.

Inapokuja kwenye swala la fedha, watu hutumia kila mbinu ili kuzipata nyingi zaidi. Na moja ya mbinu hizo ni kuuza zaidi.
Makampuni ya mitandao ya kijamii yanapotaka kupata fedha zaidi, yanateka umakini wako zaidi na kuuza kwa wengi zaidi.

Ufanye nini kwenye hili?​

Nilichokueleza hapa ni tone tu kutoka kwenye bahari ya mengi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ambayo hayana manufaa kwako.

Kwenye kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI nimekushirikisha kwa kina mbinu zote ambazo mitandao ya kijamii imekuwa inatumia kukuchukua mateka na kisha kukuuza kwa namna ambayo mitandao hiyo inataka yenyewe.


Kitabu hicho pia kina suluhisho la namna ya kuondoka kwenye huo utumwa ambao umetekwa na kuweza kuwa huru tena.

Ninachoweza kukuambia na kukuhakikishia ni kwamba kama umekuwa unatumia mitandao ya kijamii kwa muda sasa, akili yako haiko sawa tena.
Kuna namna mitandao hiyo imeshaharibu na kuteka akili yako bila ya wewe mwenyewe kujua.

Moja ya dalili za namna mitandao ya kijamii imeharibu akili yako ni kitu kinaitwa FOMO (Fear Of Missing Out). Hii ni hali inayotokea pale ambapo unakuwa hujatumia mtandao wa kijamii kwa muda, unaona kama unapitwa hivi. Hivyo unakimbilia kutumia kila mara ili usipitwe na chochote.

Hiyo ni dalili moja, lakini zipo nyingi ambazo zinaonyesha jinsi mitandao ya kijamii imekuteka na kukuuza bila wewe mwenyewe kujua.
Pata leo na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili uweze kupata uelewa na kuchukua hatua sahihi za kurudisha uhuru wako.

Wasiliana sasa na 0752 977 170 ili kupata kitabu hiki kizuri cha kukuondoa kwenye mateka na gereza ambalo mitandao ya kijamii imekushikilia.

Kama unatumia simu janja (smartphone) na mtandao wowote wa kijamii, hiki ni kitabu unachopaswa kusoma, maana wenzako wamejipanga kweli kweli kukuteka na kukuuza.

Kama huna maarifa sahihi ya kukwepa mitego yao, wataendelea kukutumia watakavyo wao.

Mimi kama rafiki yako nataka uwe huru kuyaishi maisha yako kwa namna ambayo ni sahihi kwako.

Ndiyo maana mara zote nimekuwa nakushirikisha maarifa ya kukuwezesha kuwa na uhuru huo.

Kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ni moja ya zana muhimu mno unazopaswa kuwa nazo ili kuvuka vyema kwenye zama hizi tunazoishi sasa. Kipate kitabu sasa kwa kuwasiliana na 0752 977 170 uletewe au kutumiwa ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,

Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
 
Kuna namna mitandao hiyo imeshaharibu na kuteka akili yako bila ya wewe mwenyewe kujua.

Moja ya dalili za namna mitandao ya kijamii imeharibu akili yako ni kitu kinaitwa FOMO (Fear Of Missing Out). Hii ni hali inayotokea pale ambapo unakuwa hujatumia mtandao wa kijamii kwa muda, unaona kama unapitwa hivi. Hivyo unakimbilia kutumia kila mara ili usipitwe na chochote.
Hii hatari Sana tumegeuzwa misukule bila kujijua ...
 
Dah tangazo limekaza nganganga, ndio maana umeshindwa kufikiri upande wa pili wa shilingi ukoje...

Ninavyofahamu Instagram wanauza taarifa zako kwa makampuni ya ki biashara ikiwa na maana kwamba... Utakua ukiona post za sponsored / Reels ya kile unacho LIKE kwa Sana.

Mfano : Ikiwa wewe unapenda Sana mavazi, na una LIKE post nyingi za mavazi basi INSTAGRAM watakua wakikuletea Sana post za mavazi, hii inamaana kwamba Kuna mfanyabiashara amelipia sponsored ad tangazo lake la mavazi kwahiyo INSTAGRAM wanalielekeza kwako wewe mpenzi wa fasion / mavazi.

Hivyohivyo ukiwa unapenda Sana misosi na una LIKE Sana post za misosi, basi utakua ukiona Sana post za misosi, INSTAGRAM watakua wanakuletea kile unachopenda na kuki LIKE kwa sana.

Kwa mantiki hiyo, hatuwezi kutumia neno INAKUUZA Kama ambavyo umesema kwenye tangazo lako, ulioaswa kutumia neno INAKUPELEKA kwa mfanyabiashara anaeuza kile unachokitaka / DEMAND.

Baba tangazo lako limekaza Sana, weka grease kidogo... Kwa tangazo hili hutoweza ku meet your AUDIENCE hapa, utakua ni Kama wale wafanyabiashara ambao kwenye Instagram wana post post nyingi za bidhaa na mauzo hakuna
 
Labda tu unawaingiza kwenye biashara yako. Nimesoma kwa makini ili kuona madhara ya hiyo mitandao,hasa pale uliposema inaharibu akili,lakini nimeishia tu kuona unamaanisha utumiaji sana,kuwa addicted na mitandao. Sijaona madhara.

Eleza madhara yake,labda nitakuwa kichaa baadae,labda ubongo utavimba. Umekwepa pia kueleza kwa uwazi jinsi mitandao hiyo ilivyowapatia pesa,biashara watuamiaji wengi. Wengi wanafanya biashara kwenye mitandao hiyo.

Wachache itawaingia hiyo hoja yako,labda tu utuambie tuache kutumia vifaa vya digital kama simu na computer ambazo nawe unatumia
 
Kwahiyo wasiotumia mitandao ndio wajanja au ndio sio bidhaa?

Wewe pia umetumia mtandao kufikisha ujumbe wa kuuza kitabu
 
Kwa logic ulizotumia kuandika ni wazi kuwa nawe unatafuta mateka wa kitabu chako. Kwani hapa jamiiforums umelipia?

Angalia na upande wa pili pia, labda kama unafungua hiyo mitandao na kulala fofofo bila cha kufanya.
 
Jifunze Copywriting skills... Hiki kitabu ungekiuza vizuri sana ila story uliyoiandika haishawishi mtu kununua hiki kitabu. Mpe mtu solution baada ya kua mtumwa atumie mitandao kwa faida kwa maana huwezi acha kutumia mitandao ya Kijamii kwa zama hizi.
 
Back
Top Bottom