Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Humble African

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Messages
4,776
Points
2,000
Humble African

Humble African

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2013
4,776 2,000
Kuna watu kibao humu JF walituasa kwamba Forex ni utapeli hilo kwanza napingana nalo kwa nguvu zote sababu sio kweli kwamba forex ni utapeli kabla sijafunguka mengine niwathibitishie nimejiridhisha bila hata lepe la mashaka kwamba Forex is real and its my future lifestyle na binafsi sijioni nikikoma kufanya Forex licha ya haya magumu ninayopitia bali mawazo yao ninayachukuliaga kama catalyst ya kutaka kuzidi kuijua hii biashara kwa mapana zaidi kujua weakness na strength zake na kujua potential scammer, wezi na matapeli wakoje maana wametawala hii biashara kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na money liquidity kubwa kuliko soko lolote duniani..more than 6 trillion USD is traded daily on the Global financial exchange market..hiki ni kiasi kikubwa sana hivyo matapeli huwa wanazengea zengea kwenye magap Kama haya yenye mkwanja mrefu..my economic cake pie is in Forex that's why I wont quit it easily.

But changamoto kubwa ya Forex ni hawa brokers na trainers..ninaposema trainers nazungumzia mtu kama Ontario hawa waliochungulia fursa mapema na kuintroduce kwa watu nchini kwa kigezo cha kuitoa elimu kwa bei sawa na bure tusijue wana agenda yao ya siri na Wasauzi ya kutaka kuwaliza watanzania wenzao.

Ontario ni mtunzi mzuri wa story na ana kipawa cha kusimulia na kushawishi kwa ufasha na ni mtu mwenye uelewa mpana wa mambo but anakosa kitu muhimu sana katika maisha uwezo wa kusocialize na watu in harmony..he is not a leader he is a boss na ukiangalia there is a thin line between a leader and a Boss..Ontario ana dharau, kiburi, na kejeli mbaya sana bila kujalisha umri wa anaeongea nae. Hana attentive listening ukiongea nae anakuangalia kama Choo cha shimo na hajali lolote najua wengi waliokutana nae watakiri huu ukweli mchungu kwake ukiona mtu ana urafiki na Ontario ujue huyo mtu analazimika kujishusha sana kwa huyu dogo ili waende along. Huwa nashangaa ni rafiki sana na Bold. Pole sana Bold..I know what you going through.

Wahenga humu walituhasa kwamba ukiitwa kwenye fursa tafakari mara mbili yaweza kuwa wewe ndio fursa.anyways tulipoitwa kwenye fursa mwanzoni mambo yalienda vizuri na humu tulikuwa tunavurumusha screenshot za profit tu kwa maelekezo ya Ontario ili tuwakoge haters hadi haters wakafyata but kadri siku zilivyoenda mambo yakawa kimya ikawa ni loss daily tu watu wamechukua viinua mgongo vyote vikafyekwa sokoni. Hakyamungu!

Saga lilianza around mwezi wa kumi baada ya Ontario kula njama ya siri na broker awe anampa pips 2 kwa kila kichwa na zikiwa zinatoka calls kibao kombo kwa siku na zote zilikuwa sio accurate hivyo na watu kutengenezewa mazingira ya kutrade more often inamaanisha wakitrade watu 1000 wakafungua position 7 kila mmoja na idadi ya spreads pips anazopewa kutoka kwa broker kwa mtu mmoja ni 2..kimahesabu anapata 1000×7×2= 14,000 pips hizi ni dola kibao kwa siku ..wandugu wanojua mahesabu zaidi wanajua ni madola kiasi gani jamaa kavuta, hili suala alituficha but aliwahi kusema "Bob Marley you can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time"... Tukashtuka..tukamuuliza..akakubali ila akakiri alituficha na hayo mamilion yanayopatikana ni kwa ajili ya kuendeshea ofisi ya TMT co Ltd iliyoko pale Jangid plaza.. Watoto wa maskini tukakubali tu kwa shingo upande ila tukawa tumeghafilishwa na kusikitishwa sana na hizi njama zao..hili likapita na tukajilazimisha kulimeza maana ukipenda boga upende na ua lake.

Tamaa ni mbaya sana..licha ya kuchukua mamilion kutokana na hizo pips hawakuridhika..bado tena walikuwa wanachukua pesa kibao kwa siri kwa ajili ya IB link kwa affiliate program waliotuunga nayo siku tunamaliza mafunzo bila ridhaa yetu kutoka kwa broker kwa sisi tukipata loss sokoni wao wanapata chochote maana broker wao ni market marker. Hakyamungu! People are heartless.

Kama ilivyo asili ya watu wenye tamaa mbaya wakivurugana basi wao hukimbilia kutafuta sympathy ya Wateja..juzi wakavurugana broker na TMT kama ilivyo tabia ya wezi na matapeli kugeukana.. Majuzi wenyewe wanakuja na habari kwamba yule Broker ni market Maker na mwizi..kweli? Wakati wewe mentor umeishi South afrika na umekuwa Trader kwa miaka kibao bado hujui status ya broker unae trade nae? Na inakuwaje mrecomend broker mwenye walakini na competency na efficiency yake? Broker nae anajitetea kwa kutuma texts kwa Wateja privately akimtuhumu huyo mentor kuwa ni batili na mbabaishaji na kuwasihi watu wamuignore!? Blalifuli!

Tangu mwanzo mchakato uligubikwa na walakini mkubwa uliokuwa unaendelea..kwanza kumlazimisha mtu afungue real account baada ya siku tano tu za kumaliza mafunzo na aweke laki tano kuanza kutrade ilikuwa ni ishara ya wizi wa wazi sema tulikuwa na trust na maneno sukari ya Ontario, thus we were blinded and we had fear of missing out easy Money.. Hatukujua!

Kutoa calls zaidi ya 7 kwa siku ni ishara mbaya ya kuwafanya clients waovetrade then wao wapige hela. Wizi huu.

Kuwaambia watu waongeze position ilhali wako in deep red ilikuwa ishara ya wizi, kuwataka watu waburn account zao wao wanufaike.

Kudiscourage matumizi ya stop loss ilhali ndio silaha ya kukinga mtaji wako kwenye Forex ilikuwa ishara ya wizi.

Watu wapoteze zaidi ili mpate zaidi maana kila ijumaa ilikuwa tunapunwa hela yote ya wiki nzima.

Mungu sio Sholo Mwamba, Yule broker market maker aliekuwa anatupiga sisi kwa tamaa kapitiliza kawafanyia mtimanyongo hadi kampuni ya TMT kaipuna zaidi ya nusu billion mapema mwezi wa kwanza. Imagine kampuni hii Changa ya huyu dogo imewazaje kupata nusu billion kwa muda mfupi hivi? Ni mikwanja aliyotuibia sisi misukule wake. But in life! "easy come..easy go"..ukikipata kiwepesi..kitaondoka kiwepesi pia. Nusu billion gone in a single month. Kweli JP Market broker ni hayawani!

Nitoe Rai kwa Ontario...sio kwamba namchukia hapana Bali naamini biashara inayohusisha watu moja kwa moja haiwezi kutokana na tabia yake mbaya ya asili..biashara na dharau, kebehi, utapeli na matusi havichangamani milele. Ni vyema akaendela na kilimo apate mil 19 zake kwa siku. Ameharibu kitu muhimu sana katika maisha yake ya biashara "Brand" and trust ya watu wengi aliowavuta kwa maandishi matamu humu JF..Trust ya watu pekee ni mtaji mkubwa kuliko hata mtaji wa fedha.

Fid Q aliwahi kusema neno lenye utamu siku zote halina ukweli na neno lisilo na utamu ndio lenye ukweli ndani yake. Tuwe makini sana na maneno matamu ya watu wa kariba ya Ontario.

Kwenye ile thread yake ya Namna alivyopiga milion 19 alipata kusema hivi "shika akili zao waachie mioyo yao" ndio kauli mbiu yake guys tuwe makini dogo asishike akili zetu kirahisi.

Namshukuru kwa kutuletea fursa hii adhimu lakini isiwe sababu ya kutuibia, kututapeli na kutunyanyasa economically and emotionally.

Rai kwa traders waliopigwa za uso na ndugu yao.."if you want to be strong learn how to fight alone" kwa kuwekeza Kwenye skills and self learning tunaweza kuwa self consistency profitable traders..let's ignore TMT they are scammer and predators and I don't recommend anyone to trust them.

Don't hate the game, hate the player.

Oooooopsiiii! Finally misukule wa Ontario tuko huru but tuko nyang'anyang'a kiuchumi. But it feels good kuwa huru.

Forex sio utapeli, matapeli ni mawakala wake.

Ni bora walimkavu...kuliko walimwengu!

Freedom!.
 
The Monk

The Monk

Platinum Member
Joined
Oct 12, 2012
Messages
12,982
Points
2,000
The Monk

The Monk

Platinum Member
Joined Oct 12, 2012
12,982 2,000
Mbona hayo yote uliyoyasema yalishaletwa na watu tofauti tofauti wakaweka hadi screenshot za malalamiko?

Sasa hivi watu wapo kwenye hatua ya lessons learned. Walishavuka hii stage kitambo sana. Kuna wakati ilikua hatupumui kwa nyuzi za Forex, mtifuano mithili ya ukanda wa gaza kama sio Syria Aleppo.
 
Humble African

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Messages
4,776
Points
2,000
Humble African

Humble African

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2013
4,776 2,000
D9,forex nilizitilia shaka tangu mwanzo
D9 ni zengwe Forex haina shida kama nikivyoeleza tatizo ni kwa wale ma agents wake ndio wamejaa ukatili na tamaa mbaya.

Nakushauri jifunze Forex Sio mbaya...D9 kitaalamu inaitwa ponzi scheme huu ndio utapeli mkubwa.
 
mjingamimi

mjingamimi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2015
Messages
17,385
Points
2,000
mjingamimi

mjingamimi

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2015
17,385 2,000
Mkuu sio ya kucheka haya! Tafadhali tupe hata pole tu inatosha.
Pole haitasaidia kitu.mngetusikiliza tangu mwanzo.ndo ingesaidia.kama forex ni rahisi kwa nini alikuwa anahangaika na ada zenu.?si angetulia tu.apige mahela mwenyewe.hela NGUMU.
 

Forum statistics

Threads 1,325,452
Members 509,127
Posts 32,192,987
Top