Hivi ndivyo risasi nane zilizotolewa mwilini mwa Lissu nchini Kenya, nje ya 5 zilizotolewa pale Dodoma

Inashangaza kuwa hauwezi kumwona pale Mungu alipo. Hivi haushangai risasi kutokukiona kichwa na kifua cha TL? Ni mkono wa Mungu ulikuwa umemfunika ili waovu ambao Mungu anawajua vizuri na ambao uhai wao uko mikononi mwake washindwe kutekeleza azima yao ya kuutoa uhai wa TL.
Hiyo ya begani hapo inaonesha kabisa ilielekezwa ktk moyo wa TL ili kuusamba ratisha kabisa ila Mungu hakupenda akai panch.
Eeee mwenyezimungu mnusuru mja wako huyu anayeteswa na mikono ya shetani.
 
Kwa sisi Wakristo, umaarufu wa Manabii na Watumishi wa Mungu ulipatikana baada ya mateso na kuuwawa. Hawa manabii hawakuwa na ulinzi wowote isipokuwa wa kiroho.
Kwa hiyo ni kwaida kwa mtu anayetaka kuwa maarufu na anayefikiri kuwa anatetea wanyonge kupata matatizo kama haya.
Ndiyo maana Viongozi wakuu wa Inchi wanakuwa na ulinzi mkali kwa sababu ya kuwa watetezi wa Watu.
Tundu Lissu anafanya makosa kushindana na kundi lenye nguvu bila ya kuwa na ulinzi wowote.
Apewe ulinzi ili hata kama atapata shambulio tupate pahala pa kuanzia.
"ignorance is too expensive"
Mwalimu Nyerere japokuwa amekufa lakini yu hai.
 
Imenitoa machozi...TL kama binadamu anaweza kuwa ana mapungufu yake,lakini hakustahili unyama huu.Miaka 20 iliyopita,wakati wengine wakiwa hawajaingia kwenye siasa,TL alikuwa Bulyahulu kuwatetea wananchi walibomolewa nyumba zao na Serikali ili kumpisha muwekezaji,walihamishwa kinyama bila fidia wala chochote.

Wakati akiyafanya haya,serikali ilimuita mchochezi na kumfungulia kesi kibao.Aliwatetea raia wa Nyamongo kando ya Mgodi wa North Mara bila hata kulipwa senti,zaidi ya vijana 200 walikuwa wamefungwa jela kwa kesi za kubambikiwa kwa ushirika wa DC wa Tarime na Mgodi wa North Mara.TL alifunga safari toka Dsm mpaka Tarime,aliwatetea bureee na wote wakatoka.Huyu hakustahili adhabu hii ambayo watesi wake wamemchagulia.

Wakati TL akiwa peke yake,akipambana kwa vifungu vya sheria za nchi na za kimataifa dhidi ya ubabe na uonevu wa wananchi kutoka kwa wawekezaji wa Migodi,hao wanaomuita "msaliti" walikuwa busy bungeni kupitisha sheria ambazo leo wao ndio wanaziona za kinyonyaji.

Mungu atakupa nguvu mnyampaa Tundu Lissu,utarudi tena katika pumzi na uhai wako,kama Mungu alivyomuokoa Daniel katikati la Simba wenye njaa,ndivyo atakavyotenda kwako,katikati ya watesi watakaolipwa hapahap duniani.

Ni kwanini Mungu umeyaruhusu haya kwa TL?Ni wapi alipokosea zaidi ya sisi wengine na kustahili unyama huu?Lakini wewe Mungu mwenye haki ulinena,ya kwamba hautatuacha kamwe,na wala hautaweza kutupa majaribu yashindayo imani zetu.Jaribu hili kwa TL,linaonyesha uimara na imani yake kubwa kwako.Tenda Mungu,tenda ewe mwenye haki,tenda sawasawa na fadhila zako

Upone haraka TL
I cried for him,inasikitisha Sana,kwa nini watu wengine watake kuchukua leseni ya maisha ya watu?lakini Kama Mungu aishivyo,ambaye Leo hii tunajinyenyekeza kwake,kwa kufunga na kuomba,na Kama alivyosema mwenye haki ataishi kwa imani,ambaye yeye havunji agano na watu wake,Mungu atakamilisha kusudi lake,hao watu wabaya wanaomjilia,watatawanywa kwa njia saba,maana Mungu amenena haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wameamua kuchagua kukaa upande wa shetani na kujiondolea hofu ya Mungu mioyoni mwao, madaraka yamewalevya wapo tayari kumwaga damu kisa hawataki kukosolewa.

Eee Mwenyezi Mungu mpiganie Mpendwa wetu Lissu na pigana juu ya watesi wake.

Katika Jina YESU KRISTO.
Eee Mungu Mkuu pigana na hao wanapigana na wana wa nchi hii bila huruma. Mkono wako wa nguvu Ukadhihirike ee Mungu.
 
Kutokana na huo mchoro Nmejaribu kuwaza how is it possible Mguu wa Kulia uumie zaid kuliko wa kushoto considering the fact that Mguu wa kushoto ndio ulikuwa mlangoni unapokaa kwenye gar na Pia ndio upande uliopigwa na risasi zaid kuliko upande wa dereva.
Sjui ila nmewza tu from the image.
 
Dah, inanyon'gonyeza sana! Uko wapi Mungu! Tukumbuke basi wana wako, kama kuna mahali tulikukwaza tafadhali Baba mwenyezi Tusamehe sana!
Mie tokea jana nilivyosikia ile taarifa ya akina Mashinji na Prof. Safari nilijisikia vibaya sana. Kweli Lisu amepata maumivu makali. Na imagine wakati mwingine hata nikikata kitunguu jikoni, ikitokea bahati mbaya nikajikata na kisu maumivu yake yanakuwa makali sasa sembuse risasi!
 
....laana iwe juu ya wote walio geuza maneno ya kwa kununuliwa na kumgeuzia kibao mzee wa mihogo na mchumbake

Laana haiwapati itawapata wao wenyewe kwa kuamua kuwa na bei.Pole sana usiwe unatoa laana ukadhani itawapata wasiohusika itampata aliyehusika naye ni Dr.Slaa na Mkewe.Leo wameshindwa hata kutoa pole ya kinafiki
 
Alafu unakuta watu kila wakisimama wanatumia jina LA Mungu kutafuta kuaminiwa na wananchi..Ee Mungu baba wa mbinguni nakuomba ukaonekane katika wale wote wakudhihakiao nakulitumia jina lako kuhadaa watu.Mponye kamanda wetu lissu na uwaoneshe watesi wake kama wewe ni Mkuu.kwa jina LA Yesu kristo aliye hai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie tokea jana nilivyosikia ile taarifa ya akina Mashinji na Prof. Safari nilijisikia vibaya sana. Kweli Lisu amepata maumivu makali. Na imagine wakati mwingine hata nikikata kitunguu jikoni, ikitokea bahati mbaya nikajikata na kisu maumivu yake yanakuwa makali sasa sembuse risasi!
Yaani inaumiza mno, kila ukiwaza alivyokua anashtuka risasi zinapovunja mifupa Yale maumivu moyoni nawaza tofauti Sana, laiti ningekua na uwezo sijui ningefanyaje kwakweli.
 
Kwa sisi Wakristo, umaarufu wa Manabii na Watumishi wa Mungu ulipatikana baada ya mateso na kuuwawa. Hawa manabii hawakuwa na ulinzi wowote isipokuwa wa kiroho.
Kwa hiyo ni kwaida kwa mtu anayetaka kuwa maarufu na anayefikiri kuwa anatetea wanyonge kupata matatizo kama haya.
Ndiyo maana Viongozi wakuu wa Inchi wanakuwa na ulinzi mkali kwa sababu ya kuwa watetezi wa Watu.
Tundu Lissu anafanya makosa kushindana na kundi lenye nguvu bila ya kuwa na ulinzi wowote.
Apewe ulinzi ili hata kama atapata shambulio tupate pahala pa kuanzia.
"ignorance is too expensive"
Mwalimu Nyerere japokuwa amekufa lakini yu hai.
Unakosea, hata Yesu aliuawa kwakuwa hakuwa na walinzi wenye silaha kama za akina Herode na watawala wenzake. Waliomkamata na waliomtesa na kumuua hawakukutana na vikwazo vyovyote. Hatuwezi kusema Yesu alikosea kumhubiri Mungu eti kwakuwa alifanya hivyo bila kuwa na ulinzi wa kibinadamu. Mtu anayedhani yuko sahihi kuua watu wema na aangalie pia aliposimama sio salama. Watu wengi wamehuzunishwa na tukio hili, kama tukisema tuwaite watu wote waliosononeshwa na tukio la Lissu tutakosa pa kuwakusanyia. Ingawa pa kuwakusanyia kimwili hapapo lakini pakuzikusanyia roho na mioyo yao papo. Kama TL angekuwa sio mwema asingechaguliwa na wanaSingida kuwa mbuge wao na asingechaguliwa na wanasheria wenzake kuwa kiongozi wao. Bila shaka TL ni mwema katika vigezo vya wazi, hatujui kwenye vigezo vya siri anapata alama ngapi.
 
Back
Top Bottom