Hivi ndivyo risasi nane zilizotolewa mwilini mwa Lissu nchini Kenya, nje ya 5 zilizotolewa pale Dodoma

Risasi mbili zivunje mguu zaidi ya mara 5 basi Ana matatz ya mifupa.. dogo alopogwa risasi faya ya mguu na police kavunjika mara moja na ile risasi ni ya smg pia..


au wanaongeza chumvi watoa taarifa maana mfupa ni tafauti na kioo jamn
 
Mh. Lissu narudia tena Mungu lazima ajilipize kisasi juu yako, labda km siku hizi aoni aisei..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mateso aliyoyapitia TAL ni zaidi ya MANDELA; makaburu walimuweka ndani kwa muda mrefu lakini hawakumfanyia unyama kama huu. Nawalinganisha waujaji hawa wa Tanzania kuwa ni zaidi ya makaburu wa Afrika Kusini.

Naomba sasa.

Baba Mungu muweza wa yote, unawajua wahusika wote waliopanga na kutekeleza unyama huu dhidi ya TAL, wewe ndio uliyempa akili TAL na ujasiri, na alizitumia akili hizo na ujasiri kuwatetea watanzania ambao wengi wao ni waoga na wenye uwezo mdogo wa kujua uovu unaotendwa katika nchi yao.

Ninawasogeza mbele ya kiti chako cha hukumu wote kuanzia mkubwa wao mpaka yule aliyepewa jukumu la kumpiga risasi TAL, nikiomba kisasi chako kiwe juu yao na watoto wao kuanzia kizazi cha kwanza mpaka cha tatu.

-Mateso anayoyapitia TAL na maumivu yawapate wao mara saba zaidi
-Kwa uweza ulionao naomba uwaondolee kinga waliyonayo ili yawapate mabaya kuliko yaliyompata TAL
-Watie alama watu hawa ili kila mtu anayewaona au kuwasikia awachukie na kuwalaani
-Weka kati yao na wazao wao magonjwa ambayo hayatapata tiba kwenye hospitali yoyote duniani.
-Kama vile walivyoharibu tumbo la TAL, wao pia matumbo yao yapate magonjwa ya kansa za matumbo.
-Asikosekane mtu kwao na uzao wao ambaye hatatembelea magongo, asikosekane mtu kwao ambaye hatatokwa damu mwilini mwake, asikosekane mtu kwao ambaye hatakuwa kichaa na kuokota makopo barabarani na kula mavi.
-Uwafute watu hao katika uso wa dunia baada ya kupata mateso mazito hapa duniani. AMEN
 
Eeh Mungu wa Mbinguni. Mponye TL mtetezi (wa haki za watanzania na utawala wa sheria). Tunakumbuka jinsi Sauli alivyokua anawinda kitoa uhai wa Daidi ktk Biblia baada ya Daudi kukubalika na watu wako. Jinsi ulivyomwokoa Daudi asiuawe tunaomba uwape uwezo wa juu madaktari waweze kuponya afya ya TL. Eeh Mungu twajua jaribu analopitia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imenitoa machozi...TL kama binadamu anaweza kuwa ana mapungufu yake,lakini hakustahili unyama huu.Miaka 20 iliyopita,wakati wengine wakiwa hawajaingia kwenye siasa,TL alikuwa Bulyahulu kuwatetea wananchi walibomolewa nyumba zao na Serikali ili kumpisha muwekezaji,walihamishwa kinyama bila fidia wala chochote.

Wakati akiyafanya haya,serikali ilimuita mchochezi na kumfungulia kesi kibao.Aliwatetea raia wa Nyamongo kando ya Mgodi wa North Mara bila hata kulipwa senti,zaidi ya vijana 200 walikuwa wamefungwa jela kwa kesi za kubambikiwa kwa ushirika wa DC wa Tarime na Mgodi wa North Mara.TL alifunga safari toka Dsm mpaka Tarime,aliwatetea bureee na wote wakatoka.Huyu hakustahili adhabu hii ambayo watesi wake wamemchagulia.

Wakati TL akiwa peke yake,akipambana kwa vifungu vya sheria za nchi na za kimataifa dhidi ya ubabe na uonevu wa wananchi kutoka kwa wawekezaji wa Migodi,hao wanaomuita "msaliti" walikuwa busy bungeni kupitisha sheria ambazo leo wao ndio wanaziona za kinyonyaji.

Mungu atakupa nguvu mnyampaa Tundu Lissu,utarudi tena katika pumzi na uhai wako,kama Mungu alivyomuokoa Daniel katikati la Simba wenye njaa,ndivyo atakavyotenda kwako,katikati ya watesi watakaolipwa hapahap duniani.

Ni kwanini Mungu umeyaruhusu haya kwa TL?Ni wapi alipokosea zaidi ya sisi wengine na kustahili unyama huu?Lakini wewe Mungu mwenye haki ulinena,ya kwamba hautatuacha kamwe,na wala hautaweza kutupa majaribu yashindayo imani zetu.Jaribu hili kwa TL,linaonyesha uimara na imani yake kubwa kwako.Tenda Mungu,tenda ewe mwenye haki,tenda sawasawa na fadhila zako

Upone haraka TL
Inaumiza sana kwakweli!
 
Unyama huu naufananisha na wa mnyama hatari anaishi misitu ys Amazon huko America Kusini anaitwa ANAKONDA.
 
Ni position ya miguu tu!! Inawezekana wa kulia alinyoosha wa kushoto kakunja!! Pale wa kulia ulipokuwa ndipo risasi nyingi zikamiminikia hapo. Au vice versa lakini kikubwa miguu inaonekana haikukaa sawa, aliipishanisha na ulipokuwa wa kulia ndipo palishambuliwa zaidi!!

Ukiangalia mchoro vizuri unaweza kuona kuwa alipigwa kwanza bega la kushoto kisha akaamua kulaza kiti halafu akageuka kulala kifudifudi, kwa maana kuwa mguu wa kulia ukawa upande wa mlango ambapo zilipita risasi. Na kwa sababu tayari aliishaishiwa nguvu na fahamu hakuweza kujizuia au kugeuka tena.

I can imagine it was one of the worst tragedy a human being can ever come accross, na hiyo ni picha halisi ya roho na moyo wa mtu aliyepanga na kutekeleza unyama huu kwa mtu ambaye hakuwahi kutumia silaha katika kuwatetea watanzania bali akili aliyopewa na Mungu na kinywa chake.

Bado sijaona ni kosa gani alilowafanyia watanzania hata kudeserve kufanyiwa unyama huu!!
 
Kumbe kubenea yupo sahihi kuliko ndugai?
Kumbe sio risasi tano tu!
Yule "Chizi" wa Dodoma analazimisha ziwe tano tuu,kiasi cha kutaka kumsulubu Kubenea kwa kusema risasi zilikuws nyingi zaidi ya hizo tano zake

KWA HYO KUBENEA KAONGEA UKWELI KUWA NI RISAS ZAID YA 38. NGUGAI KADANGANYA BUNGE

GET WELL SOON TUNDU LISSU

32 + 8= 40
Nduguai Vs Kubenea, ngoma mbichi ila mshindi ni dhahiri.

;

Kwani Kubenea na Ndugai nani alikuwa wa kwanza kutamka? Je yawezakana wote wakawa sahihi kutokana na wakati wa tamko?
 
Munguatosha amponye na ampe nguvu.

"Never stop learning because life never stop teaching"
 
Risasi mbili zivunje mguu zaidi ya mara 5 basi Ana matatz ya mifupa.. dogo alopogwa risasi faya ya mguu na police kavunjika mara moja na ile risasi ni ya smg pia..


au wanaongeza chumvi watoa taarifa maana mfupa ni tafauti na kioo jamn
Kama haujashuhudia kitu ni bora ukanyamaza ndugu, hali iliyopo ni mbaya sana na kiuhalisia mguu wake mmoja umesagika na inawezekana hata kuunga ikawa ni kazi ngumu sana, hivyo usiandike kwa kuwa tu umeonyeshwa kufurahia kwa kilichofanyika. Tambua siku zote Mungu ulipa hapa hapa na inawezekana hata wewe unayeshabikia ujinga huu ukapata hukumu stahiki kwa unyama huu uliofanyika.
 
Kuna watu wameamua kuchagua kukaa upande wa shetani na kujiondolea hofu ya Mungu mioyoni mwao, madaraka yamewalevya wapo tayari kumwaga damu kisa hawataki kukosolewa.

Eee Mwenyezi Mungu mpiganie Mpendwa wetu Lissu na pigana juu ya watesi wake.
Ni kweli; tena yuko kwenye kiti anazunguka na kunywa juisi akiona nge tu anakimbia kuogopa kuumwa na kufa lakini yeye amesababisha binadamu mwenzake kumiminiwa risasi ili afe.
 
Haijawahi tokea mtu kupata amani au furaha kwa kumwuua adui yako na ndio maana maandiko yanatuambia adui yako mwombee kwa Mungu ili kisasi cha Mungu kiwe juu yake. Ukiua adui yako amani yako na furaha yako itaathirika na inaweza isiwepo kabisa. Ukiweza kuwauliza maswali wezi waliowahi kuua watakueleza walivyo na guilty katika mioyo na maisha yao yote.
 
Inasikitisha sana sana sana!!! Lakini naamini Mwenyezi Mungu aliyemuweka hai hadi sasa ataendelea kumlinda zaidi, kumpa afya njema na maisha marefu.
Pole sana Mheshimiwa Tundu Lisu kwa maumivu makali unayoyapitia sasa, Mungu yu pamoja nawe.

Kwa jinsi unyama huu unavyolaaniwa na watu wengi sana, wale mashetani wote waliohusika lazima wapoteze consistency na muda si mrefu wataanza kukwaruzana wao kwa wao na wataumbuka. WALAANIWE.

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom