Hivi ndivyo rais wa kwanza wa Zanzibar Mh. Abeid Karume alivyouawa

HISTORIA YA ABEID AMANI KARUME.

Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa
Rais wa kwanza wa Zanzibar . Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi .
Karume aliongoza nchi baada ya
mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964 .
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere . Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania , Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.




KUIPINDUA SERIKALI YA SULTANI MPAKA KUWA RAIS.


Usultani wa Zanzibar ulikuwa umepewa na Uingerezauhuru wake mwaka 1963 . Kabla ya hapo, Waarabu walikuwa wamefaulu kudumisha katika mfululizo wa chaguziutawala waliokuwa nao tangu zamani za Zanzibar kuwa chini ya Usultani wa Omani.
Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilichowakilisha hasa Waafrika, kilipoona kwamba bungeni kina viti vichache ingawa kilipata 54% za kura katika uchaguzi wa Julai 1963 , kilipatana na chama cha mrengo wa kushoto Umma Party .
Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John Okello (1937 - 1971 ?) kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa
kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao. Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake. Waliokufa katika mapigano wamekadiriwa kuwa 80 hivi tu.
Kumbe yalifuata kwa siku kadhaa (labda hadi tarehe 20 Januari )
maangamizi ya kimbari dhidi ya Waarabu (waliokuwa 50,000 hivi) na
Waasia wa Asia Kusini (waliokuwa 20,000 hivi); hakuna hakika kuhusu
idadi ya waliouawa: makadirio yanataja kuanzia mamia kadhaa hadi 20,000.
Kiongozi wa ASP Abeid Karume, asiyekuwa na msimamo mkali akawa
rais wa kwanza wa nchi, na wanachama wa Umma party walipewa nafasi serikalini. Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kimeshanyang'anywa silaha.
Mwelekeo wa Kikomunisti wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha nchi za Magharibi . Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa. Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na
Marekani waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.
Wakati huo nchi za Kikomunisti za
China , Ujerumani Mashariki na Umoja wa Kisovyeti zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.
Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa
Tanzania ; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.
Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama
sikukuu ya taifa zima la Tanzania.

KUUAWA KWAKE.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abeid Amani Karume, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira na sababu za kutatanisha.
Risasi nane zilitolewa mwilini kwake mwili wake ulipofikishwa kwenye Hospitali ya V. I. Lemin, mjini Unguja kwa uchunguzi, sawa na idadi ya miaka minane ya utawala wake tangu 1964 hadi kifo chake.




ILIKUWA HIVI:

Rais Karume na Makomredi wenzake wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP) alikuwa na mazoea ya kucheza karata, damma au dhumuna kwenye ukumbi wa ofisi za makao makuu ya Chama hicho Kisiwandui, kila jioni kama sehemu ya mapumziko. Siku hiyo alifika saa 11.00 jioni akiwa na walinzi wake, akaingia ndani nao wakabaki nje kulinda.
Ikafika zamu yake kucheza; akawa anacheza na Mzee Maalim Shaha Kombo ambaye alionekana kulemewa. Ndipo Karume akamwita Mzee Mtoro Rehani ajitayarishe baada ya Kombo, naye akaitikia kwa kuaga kwanza aende msalani kujisaidia.
Sekunde chache baada ya hapo na kabla Mzee Mtoro Rehani hajarejea kutoka msalani, ghafla watu wawili wenye silaha walivamia chumba alimokuwa Karume na wenzake na kumimina risasi wakimlenga; na kufumba na kufumbua, akawa katika dimbwi la damu kimya, amepoteza uhai. Hakuna mtu mwingine aliyeuawa mbali na kujeruhiwa tu, mmoja wao akiwa Katibu Mkuu wa ASP, (sasa) Hayati Thabit Kombo Jecha.
Risasi uaji (the fatal bullet ), mbali ya risasi zote, iliyochukua uhai wa Karume ilitoka kwenye bunduki ya Luteni Hamoud Mohammed Hamoud wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT), ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi huu na aliyefyatua risasi ya kwanza wakati Karume akicheza na wenzake. Inasemekana, Hamoud aliuawa papo hapo na mlinzi wa Karume.
Wauaji wengine waliofuatana na Hamoud katika uvamizi huo ni Kapteni Ahmada Mohamed, Koplo mmoja wa jeshi ambaye jina lake halijafahamika hadi leo, na raia mmoja aliyekwenda kwa jina la Ali Khatibu Chwaya, ambao inaelezwa wote hao waliuawa kwenye mapambano ya silaha nje ya eneo la tukio.
Dakika chache baada ya mauaji kutokea, alifika Kanali Ali Mahfoudhi na askari mwingine, Kapteni Makame Hamis, wakauchukua mwili wa Karume na kuukimbiza hospitali.
Itakumbukwa, Kanali Mahfoudhi ni mmoja wa vijana wa Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed Babu, kilichoungana na ASP baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kuunda Serikali ya mseto. Ni kati ya vijana waliopelekwa Cuba kwa mafunzo ya kijeshi, na ni mmoja wa wapiganaji walioendesha mapambano ya kisayansi usiku wa Mapinduzi na kukamata uwanja wa ndege mchana Aprili, 1972.
Ni mmoja wa wanaharakati wa siasa za mrengo wa Kikomunisti ambao hawakutakiwa Zanzibar wakati wa utawala wa Karume, hivi kwamba kufuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 1964, Karume alishinikiza kwa Nyerere wapewe kazi Tanzania Bara aweze “kupumua” ambapo Mahfoudhi alipewa cheo cha Mkurugenzi wa Operesheni katika JWT.




Mungu Ibariki Tanzania.


Mungu Ibariki Africa.


Serikali ya Zanzibar iliyopinduliwa haikuwa ya Sultan .. Hakuna serikali iliyopinduliwa Zanzibar. Kilichotokea ni uvamizi ulioongozwa na Nyerere akisaidiwa na vibaraka wake kutoka ASP na Umma party. Walimkamata Waziri Mkuu Muhammed Shamte ,aliyechaguliwa na wananchi, pamoja na mawaziri wake na kuwafunga katika magereza YA Tanganyika bila kuwafikisha mahakamani, kabla hata ya huu uitwao Muungano haujafikiriwa.
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom