Hivi ndivyo Rais wa Botswana alivyomfagilia Rais Magufuli

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Hivi ndivyo Rais wa Botswana alivyo mfagilia Rais Magufuli


BY CHOICETZ ON AUGUST 30, 2016NEWS

Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC, ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dk. Seretse Khama Ian Khama, amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

botswana.jpg



Rais huyo wa Botswana ametoa pongezi hizo wakati akifungua Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo katika Mkutano huo Rais Magufuli anawakilishwa na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan.

Amesema ana imani kubwa na viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani, uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa Shelisheli na kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.

Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.

Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.

Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika)

Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

botswana-1.jpg



Baadhi ya wajumbe katika mkutano wa TROIKA nchini Swaziland
 
Back
Top Bottom