digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,890
- 14,342
Habari wakuu,hamjambo ? Naomba niende kwenye hoja yangu
Nimekuwa mdau Mkuu Wa elimu kwa miaka mingi sana toka enzi za ulipaji karo hadi elimu bure,nashukuru na kumpongeza rais kwa kujitahidi kuziba wapiga dili katika awamu yake,lakini naomba nikiri kuwa watu wanashusha mijengo mikubwa kwa kutumia fedha hizo.
Mwaka Jana nikiwa miongoni mwa wasimamizi Wa Shule yenye watoto Wa kidato cha NINE watoto 80 na kidato cha pili watoto 120, tulitakiwa Kuchangia pesa za mitihani ya Mock ,ambapo kwa kila mtoto tuliamuliwa kutoa sh 3000/= ili kufanikisha mitihani hiyo, kwa hiyo ukizidisha Mara idadi ya watoto ni 200x 3000=600,000/= kwa Shule moja tu.
Naomba izingatiwe kuwa hii ni mitihani ya mock wilaya/mkoa. Katika wilaya Yangu kuna Shule 20 na kwa makadirio kila Shule iwe na watoto 200 kwa kidato cha pili na cha nne ambao wanapaswa kufanya mtihani Wa mock wilaya/mkoa ,ukizidisha 20x600,000/= utapata 12,000,000/= kwa mwaka kila mtihani Wa mock unapofanyika, hii ikumbukwe kuwa ni miradi ya watu kwani tenda za uchapaji na urudufishaji Wa mitihani hii hupelekwa kwa masteshenari ya maafisa elimu na kujipatia neema ya pesa za umma
Mwaka huu tulijaribu kuwashauri wasimamizi Wa mitihani ya mock kuwa tuwe na Mashine za kuchapa na kurudufu kwa halimashauri yetu ili kuokoa gharama za milioni 12 kila mwaka walikataa kabisa,ambapo Mashine ya kiwango cha juu na yenye ubora tulipoulizia madukani tuliambiwa ni milioni 9 pekee.lakini kwa kuwa hii ni miradi ya maafisa elimu hili haliwezi kukubalika kiurahisi.
MAONI YANGU
Naomba serikali iingilie kati suala hili ili kuzilazimisha kila halimadhauri kuwa na Mashine ya kuchapa na kurudufu mitihani kwani jambo hili litaokoa mamilioni ya fedha zinazopigwa na maafisa elimu kila mwaka kwa baadhi ya halmashauri
Pili ili kusaidia uendeshaji na uchapaji Wa mitihani kila Shule itatakiwa kupeleka ream paper kulingana na udadi ya watahiniwa
Mwisho kila mtanzania lazima awajibike kutetea na kulinda Mali za umma na kupiga kelele pale anapoona kuna ubadhirifu.
Ahsanteni.