Hivi ndivyo ninavyo ingiza kipato cha 30,000 kwa siku baada ya kubadili fikra zangu

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
76
150
Habari ya leo wakuu,mimi ni kijana wa kiume naishi Dar najihusisha na ujasiriamali wa usafi na dawa kwa uchafu sugu katika Tiles,Masink,Vioo na Sofa.

Mwezi wa 10 mwaka jana nili hama kimakazi kutoka mkoani kuja Dar lengo likiwa ni kutafuta kazi ama shughuri yoyote ya kuni ingizia kipato maana nili amini huku fursa za kazi ni nyingi tofauti na mikoani.

Nilipo fika nika anza kutafuta kazi kila sehemu kulingana na uzoefu wangu hasa shughuri za masoko na mauzo,kwakweli ili kuwa mtihani kupata kazi hata ya kuchoma chips na nyama maana pia nna uzoefu nayo.

Nilipo ona kuna changamoto ya kuendesha maisha hata kuhudumia familia ikawa tabu maana nna mke na mtoto 1 ikanibidi nianze kukopa pesa kwa watu nnao fahamiana nao kwa kuweka kisingizio ambacho nili hisi siwezi kukosa pesa, changamoto ilikuwa ni kutumia pesa ikaisha na sijui nta pata vipi nyingine na namna ya kuirejesha kama nilivo ahidi maana nili ahidi baada ya wiki 1 tu ili kumshawishi mtu kunipatia pesa.

Miezi kadhaa iliyo pita nika ona mdau mmoja wa humu Jamii Forum kwa jina lake "Digital Base" ali post uzi unao elezea njia kadhaa za kujiajiri katika usafi hasa uchafu sugu kwenye Tiles Masink na Sofa.

Nili chukua yale maelekezo yake nikaenda kufanyia kazi japo changamoto nilikutana nayo katika namna bora ya kung'arisha ili kurudisha mng'ao na dawa nzuri ya kutumia.

Nili amua kumtafuta ili anisaidie maelekezo zaidi ili niweze kufanya kazi hiyo kwa ufanisi kwakweli namshukuru sana huyu Kaka alinisaidia maelekezo yaliyo niwezesha kuwa fundi na mtaalam wa viwango ambapo kwa sasa naweza kung'arisha hata sink lililo fubaa sana ama Tiles zilizo fubaa.

Kwa sasa kila siku naingia mtaani naongea na watu pia natumia mitandao ya kijamii hasa Facebook kutafuta wateja na kwa siku sikosi 30,000 na kuna baadhi ya siku napata mpaka 100,000 maana naweza kwenda nyumba ya mtu nika msafishia Sofa, Masink,Tiles na pia ana nipa kazi mpaka kwa wapangaji wake namfanyia kazi na bado ana niunganisha na watu wengine maana namfanyia usafi wa viwango vya juu sana kiasi ambacho haku tegemea alikuwa na mpango Kubadili sink aweke jipya lakini Mimi nang'arisha hilo hilo lina rudi kuwa jipya ama kupaka rangi kwenye tiles ili kuziba uchafu lakini Mimi namsaidia kuondokana na hiyo changamoto na kupunguza gharama.

Kwahyo ndugu yangu ama rafiki unaye kaa bila kazi kwa kusema kuwa ajira hamna tunaweza kushirikiana kufanya kazi kwa pamoja na ikiwezekana tufanye uzalishaji wa dawa za usafi za kung'arishia Tiles na Masink maana pia nime fundishwa na yule Mr natumia dawa zangu mwenyewe kufanyia usafi kwahyo ikiwa mtaji utakuwa mkubwa tunaweza kuzalisha bidhaa nyingi zingine tuka uza kwa wateja wetu wanao hitaji dawa tu au tulio wafanyia huduma.

Natamani sana Vijana wenzangu pia wapate ujuzi huu na formula hii inaweza kukusaidia kuingiza Kipato cha uhakika kila siku maana mteja mwingine uliye mfanyia kazi anaweza kuku unganisha na rafiki yake mwingine.

Asanteni sana Jamii Forum kwa kutu unganisha hapa kuna watu wana nia ya kweli kusaidia wana jukwaa wenzao ili wafaidike pia .

Asante sana πŸ™πŸ™ ❀️ Jamii Forum.
 

OllaChuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
16,918
2,000
Hongera sana mkuu em towa somo Hapa ili na wengine wajue.

Je ni "kila siku" kama ulivyosema unapata kazi? Na hiyo 30k ndio malipo au ndio faida mkuu?

Vip kuhusu gharama za uendeshaji wa hiyo shughuli yako? Je una ofisi au unafanya kuzunguka tu majumbani? Na ni vip watu wanakuamini uingie ndani ya nyumba zao?

BTW hongera sana kijana.
 

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
76
150
Hongera sana mkuu em towa somo Hapa ili na wengine wajue.

Je ni "kila siku" kama ulivyosema unapata kazi? Na hiyo 30k ndio malipo au ndio faida mkuu?

Vip kuhusu gharama za uendeshaji wa hiyo shughuli yako? Je una ofisi au unafanya kuzunguka tu majumbani? Na ni vip watu wanakuamini uingie ndani ya nyumba zao?

BTW hongera sana kijana.
Nashukuru sana mkuu,mimi bado sina ofisi maana ndo nime anza natamani niki pata mtaji nianze process za kusajili kampuni ya usafi ili niweze kupata soko pia katika taasisi ambako kwa sasa siwezi kufika.

Pia kuhusu hiyo 30,000 ni faida yangu maana matumizi ya dawa si makubwa hii dawa ina tumika kidogo sana naweza tumia Lita 3 tu kwa nyumba nzima ikiwa ni pamoja na Tiles na kama ni masink tu ni chini ya hapo pia dawa natengeneza mwenyewe kwa gharama ndogo tofauti na kununua.

Kuhusu gharama za uendeshaji sana sana kwa sasa ni nauli , chakula kabla ya kazi na baada ya kazi pamoja na dawa ndo vinavyo nigharimu.

Kuhusu Imani kwa wateja inatokana na aina ya mtu nnaye kutana naye na asiye weza kuni amini namuuzia dawa akiona matokeo yake ana nitafuta nimfanyie kazi.
 

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
76
150
Bila shaka huu ni uzi tangazo...naamini wenye uhitaji wa huduma yako wamekusoma
Sawa mkuu ni wazo pia kama uzi ume kaa kitangazo nielekeze niandike vipi ili maana yangu ieleweke vizuri maana wengine hatuna ujuzi wa Copywriting naweza Kubadili ili nieleweke maana yangu huenda huja nielewa kutokana na kuto kuwa na taaluma ya uandishi.
Mmi siji tangazi hapa na sina nia kufanya hivyo Am sorry boss πŸ™πŸ™πŸ™
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,703
2,000
Sawa mkuu ni wazo pia kama uzi ume kaa kitangazo nielekeze niandike vipi ili maana yangu ieleweke vizuri maana wengine hatuna ujuzi wa Copyright naweza Kubadili ili nieleweke maana yangu huenda huja nielewa kutokana na kuto kuwa na taaluma ya uandishi.
Mmi siji tangazi hapa na sina nia kufanya hivyo Am sorry boss πŸ™πŸ™πŸ™

Umeandika vizuri tu mkuu usijali...

Mi nimekupigia promo tu, watu wenye nyumba za marumaru wasiishie kusoma tu bali wakupe "shavu"
 

judey

Member
Jul 17, 2021
50
125
Sawa mkuu ni wazo pia kama uzi ume kaa kitangazo nielekeze niandike vipi ili maana yangu ieleweke vizuri maana wengine hatuna ujuzi wa Copyright naweza Kubadili ili nieleweke maana yangu huenda huja nielewa kutokana na kuto kuwa na taaluma ya uandishi.
Mmi siji tangazi hapa na sina nia kufanya hivyo Am sorry boss
Duuh imekaa pouwa Sana I wish kufanya hiii bro
 

Junnie27

Member
Aug 18, 2021
87
125
Hongera sanaa kaka kwa kuweza kuwa jasili share experience ako na mapito ako even kuonyesha fursa kwa vijana wengne ila ningeomba ungeweza rahisisha kaz kwa kuweka mawasiliano ili watu waweze faidika zaidi na ujuzi wako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom