Hivi ndivyo nimjuavyo Mwigulu Nchemba

Tema Mate

Senior Member
Dec 19, 2013
107
193
FAHAMU,UJASIRI NA MSIMAMO WA MH:MWIGULU NCHEMBA HAUJAOTA KAMA UYOGA,NILIPATA KUSOMA NAYE NA HUYU NDIYE MWIGULU NCHEMBA NINAYEMFAHAMU MIMI NA WATANZANIA WENYE UWEZO WA KUCHAMBUA UWEZO WA VIONGOZI WETU.

1798508_499004793537271_1354415385_n.jpg

NDG zangu nilipata bahati kusoma shule moja na kiongozi huyu kidato cha 1-4 Ilboru (1994-97) na kidato cha 5-6 (1998-2000) Mazengo na chuo kikuu UDSM na sasa ni mwl niko Dodoma naitwa Hamad.

(1) Nilianza kujua umahiri wa Mwigulu kuongoza pale alipoongoza kama kaka mkuu wa shule yenye kidato cha 5&6 huku akiwa kidato cha tatu. Wanafunzi walimkubali kwani alikuwa akiona hitilafu kwenye masilahi ya wanafunzi anamwita mkuu wa shule na kumwambia makosa ya utawala black and white. Nakumbuka siku moja chakula kilikuwa kibaya akaita wanafunzi tukaenda na sahani akatwambia chakula leo kibaya naomba tusile mpaka nimlete mkuu nimwambie arekebishe. Tukasubiru akajanae akamwambia, nanukuu, mkuu chakula leo ni kibaya hakifai kwa afya ya binadam. Hivyo nimewambia wanafunzi wenzangu tusile mpaka kitakapopikwa kingine. Wakapika "KITEI"

(2) Tukiwa Mazengo kulikuwa na tabia ya

walimu wote kutembeza bakora kila jumatatu. Mwigulu alipochaguliwa kuwa katibu mkuu akamwambia headmaster mwl Msasa aliyekuwa anaogopeka mpk kwa walimu kuwa hataki walimu waje na viboko kuchapa wanafunzi kwa vikosa vidogovidogo kwamba kuna serikali ya wanafunzi na kazi ya kusimamia wanafunzi ni kazi yao wawaache wafanye kazi yao. Alibadili tabia ya wanafunzi kukimbilia kujificha "sudani"

(3) Mwigulu alikuwa akiwambia black&white ma profesa wa chuo kikuu, alipokuwa akipigania upatikanaji wa viti vya kusomea mabibo hostels. Nanukuu, Maprofesa wazima mnatuletea baa humu hostel huku mkijua hatua pakusomea. Hivi ni kweli hamjui tumefuata nini hapa? Sasa wanafunzi wenzangu tutachukua viti vya baa tuvifanye vya kusomea, baa itarejea tukishamaliza shule na kufaulu au watakapotuletea viti.

Wanafunzi zaidi ya 4000 walichukua viti huku wakiimba wanaimani na Chifu jina alilokuwa akifahamika nalo chuoni. Kitendo hicho kilimfanya asimamishwe, wiki 2. Aliporudi akakuta viti hakuna akaita mkutano tena, akasimamishwa wiki 3 akarudishwa baada ya chuo kuweka viti chini ya kila bweni mabibo.

(4)Akiwa BOT nilipata taarifa tokea kwa classmate wetu kuwa Mwigulu alihoji kwa GOV kwanini wakurugenzi wamekopeshwa magari mapya tena bila kodi, wanapewa mafuta yakutosha wala hawaishi mbali lakini wanatumia magari ya pool ya ofisi? Hii ni ukosefu wa uadilifu. Wafanyakazi wakampenda wakurugenzi baadhi wakamchukia baada ya wiki mbili akapewa uhamisho tokea makao makuu kwenda Arusha.

(5) Akiwa kwenye chama rafiki yangu aliyeko Lumumba aliniambia huyu jamaa ana ujasiri wa wapigania uhuru alisema kama ambavyo huwakemea wapinzani akitolea mfano wa mbowe aliyedanganya umma kuwa hataki gari ili kupunguza mzigo ila baadae akachukua jipya kimyakimya na alivyo mlipua mbowe alivyokwenda na kimada wake dubai kwa gharama za bunge (kodi za watanzania), alisema jamaa huyu hamwogopi hata mwenyekiti wake kwenye vikao. Alitilea mfano swala la loliondo.
Mwigulu alipowasikiliza wananchi nakuelewa hoja yao, aliwambia nimewasikia na nimewaelewa. Katika kikao alichoitisha Rais akiwepo mwigulu na badhi ya mawaziri. Mwigulu alisema bila ardhi wananchi wa loliondo hawana maisha hivyo serikali aangalie upya msimamo wake. Ndipo waziri mmoja akasema kuliko kufuata ushauri wa mwigulu bora aache uwaziri. Mwigulu alichofanya alichana karatasi akampa waziri huyo na kumwambia Rais mpe kalamu waziri wako ajihudhuru sasa hivi aende nje halafu sisi tuendelee kujadili maisha ya watu wa loliondo. Waziri akaomba radhi na jambo hilo likaisha mpk leo Loliondo walituma ujumbe wa watu 80 wakimwomba mwigulu akagombee ubunge loliondo au aombe nafasi ya kitaifa ili nao wampigie kura.

(6) Sasa baada ya kuwa Serikalini ameendelea kuweka msimamo kwenye mambo yenye tija kwa watanzania
(A) Kulipokuwa na mjadala wa wabunge wa bunge maalumu kutaka waongezewe posho tokea laki 3 hadi saba, mwigulu alijitokeza nakusema, nanukuu watanzania wanashida sana. Kuna wanaokula mlo mmoja, kuna wazabuni wanadai, walimu wanadai, huduma bado duni hosipitalini. Wabunge hawa wamebajatika kuteuliwa na jambo la katiba ni sehemu tu ya wajibu wao. Hatujawakodi tokea kenya, uganda au ulaya kama consultants.

Anayedhani hapa anapata hela kidogo kuliko alikokuwa kwa heshima zote na afunge virago aondoke zake. Baada ya kauli yake mjadala huu ukafa. Huu ni ujasiri wa aina yake. Taarifa zilisema kuwa wabunge hao walipangiwa laki 8 kwa siku mwigulu akazikataa baada tu ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

(7) Sasa hivi majuzi ameweza kuwambia ukweli wazungu. Hotuba kama hii wazungu walizoea kuona kwa Mwl Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Nelson Mandela na Patrice Emery Lumumba.
MWIGULU NCHEMBA AHUTUBIA BUNGE LA ACP NA EU,APINGA WAZI WAZI MAPENZI YA JINSIA
Sehemu ya Majibu yake ni haya hapa.
As I have just said, the ACP Council recognizes the strategic importance of access of sexual and reproductive health care including family planning. To our values, tradition and beliefs sexual and reproductive health and rights includes pre-and post natal care and safe delivery, prevention and treatment of infertility and STDs including HIV and AIDS, access to contraceptives, reducing the recourse to unsafe abortions and comprehensive sexual education. The matters related to homosexuality are strictly out of contexts. I would argue the international community with due respect to refrain from linking the development assistances with the specific country stand on homosexual policies. Just like there was colonization, and it come to pass, and we have passed through various periods of Development Assistances with various conditionality's but if we are told to choose between our Values without assistance or Assistance tied with homosexual conditions, we will in top of our voices and in confidence remain with our Values without an assistance in dishonour of homosexual policies.

(8) Zipo taarifa pia kuwa Mwigulu alikataa kupangishiwa hotel baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri kwa madai kuwa watanzania wanashida nyingi hawezi kwenda kuishi hotelini.Walipomwambia ndio utaratibu mwigulu alisema hapendi kwenenda kwa mazoea bali anaenenda kwa uhalisia. Alisema zaidi ya robo tatu ya ndg zake wanaishi nyumba za tembe na nyasi. Hawezi kufanya hotel ndio nyumba yake ya kuishi.

Nisiwachoche, in short Najivunia kumjua kiongozi huyu maarufu aliyevuma kwa kasi zaidi katika siasa za Tanzania. He is Bold, Firm, Visioned and Consistent, ana Sifa za kiongozi anayetakiwa kuongoza Taifa hili tunakoelekea.
Wenu,

Hamad Mohamed
hamadmohamed23@gmail.com
Dodoma
Tanzania

Alisomea uzeeni? Miaka hiyo unayosema alikuwa O-level wadogo zake walikuwa wapo chuo kikuu
 
jamani jamani, NA WIZI WA EPA NAO NI UJASIRI?. MAUAJI YA MWANGOSI NAO NI UJASIRI?, HAPA KWA KWELI KIKWETE KAJISHUSHIA HESHIMA KABISA KUMPA UWAZIRI MTU WA AINA HII, SUBIRI UCHAGUZI UFIKE.
 
Hamad Mohamed! Mbona imani yetu haituruhusu kukaa uchi. Ni kwa nini unatumia picha ya mwanamke kaacha maziwa nje kama avatar?
 
Mbona unaonyesha udhaifu sana kwa Mwigulu Chemba?
 
safi sana kijana wetu, watu watabeza ila wataishia kwenye keboard wakati mwigulu yeye yuko kivitendo. time will tell , mungu akulinde mwigulu wetu, tanzania kwanza, hawa hawa wanaokubeza ndio wanaleta umimi, changu ni changu(utanganyika na uzanzibari). hakika tanzania itadumu daima kwani ni mpango wa mungu
 
Kwamba hotuba aliyoitoa EU ni ”babukubwa“ haijawahi kutolewa na wengine zaidi ya JK Nyerere na K.Nkurumah...kwamba Mkapa na hata Kikwete ktk utumishi wao wa Mambo ya Nje hawajawahi toa hotuba ka ya huyu gaidi(Pathetic)
Nilikuwa nasikia tu,kwamba siku hizi kuna wanaume wanawasifia wanaume wenzao kuzidi hata mwenye mume,jamaa umemsifia Mwigulu zaidi hata ya anavyosifiwa na mke wake.
Ukitaka kujua huyu jamaa aliiba jina la mtu,angalia sura na umri wake,then linganisha na miaka aliyosoma...1998-2000 ndio alikuwa Advance????
Mwigulu punguza kujisifia,una safari ndefu sana...yaani kupeWa unaibu Waziri umeanza kuwaza Urais??halafu huko Chuo kikuu kama ninyi mlidai haki,kwanini sasa hivi vijana wa chuo mnawabana wakidai haki zao??chuo kikuu vijana hawahojika watoto wa shule ya upili???
 
Back
Top Bottom