TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Ijumaa njema wakuu,
Kuna upotoshaji mkubwa unatembea mitandaoni tangu kuhusu pesa za ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard gauge. Upotoshaji huu umefuatia ombi la rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumuomba rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma kuzishawishi nchi zinazounda umoja wa BRICS(Brazil-Russia-India-China-South Africa) kutokana na mikopo yao kuwa ya masharti nafuu kukubali kuipa Tanzania mkopo utakaowezesha ukamilishaji wa miradi yake ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
UPOTOSHAJI unaotembea mitandaoni ni pamoja na:
1. Kwamba rais alishasema reli hiyo itajengwa kwa pesa za ndani
2. Kwamba rais amemwangukia rais Zuma baada ya kukataliwa mkopo na nchi za China, Uturuki, Morocco, Marekani na Marekani
Sote ni mashahidi na sote tunafuatilia hotuba za rais Magufuli na ukweli wa alichokisema rais ni huu.
1. Pesa za ndani zitatumika kujenga reli kwa awamu ya kwanza ambapo itaishia Morogoro, rais hajasema reli yote kutoka Dar hadi mwanza itajengwa kwa pesa za ndani. Hii maana yake ni kwamba zitahitajika pesa nje ya zile za ndani kukamilisha ujenzi huo.
2. Tanzania ilikataa mkopo kutoka China kutokana na masharti walioyatoa ya kutaka wakandarasi wa ujenzi huo watoke China na kwamba mkopo huo ni lazima upitie Benki ya EXIM ambayo ni ya china. Hakuna sehemu yoyoye ile ilipotolewa taarifa rasmi ya serikali kwamba nchi za Morocco, Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya zimeombwa mkopo na kukataa.
Myatake: Upotoshaji unaosambazwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii ina lengo gani? Nani yuko nyuma yake? Tunapaswa kuwa wafuatiji wazuri wa mambo ya nchi ili kujiridhisha na ukweli wa mambo. Upotoshaji wa ama makusudi ama kwa sababu ya kutokuwa na uelewa mzuri wa jambo lenyewe ni hatari kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu.