Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,304
- 12,965
Wakati wa mjadala mkali wa kashfa ya Richmond bungeni, huku tume iliyochunguza kashfa hiyo ikibanwa kuwa haikutoa nafasi kwa watuhumiwa hasa Lowassa kujitetea, aliibuka mwenyekiti wa tume ile Mh. Mwakyembe na kusema kuwa kama watu hawaridhiki waombe kanuni zitenguliwe ili aweze kuwasilisha upya ripoti yake ili aweze kusema hata siri waliyoificha ili kuikoa serikali isiporomoke yote.
Kwa maneno hayo mimi nilliewa kuwa kumbe tume ile iliwasilisha ukweli nusu na hivyo kumtoa kafara Lowassa na mawaziri wawili ili kumwokoa rais ambaye kwa maneno ya Mwakyembe kama wangeyasema yote, ingesababisha serikali yote kuporomoka. Kwa ufupi nilivyoelewa ni kuwa taarifa ile ilikuwa inamgusa rais moja kwa moja na kwa maana hiyo alipaswa kuondolewa madarakani lakini akaokolewa na tume kwa kuficha siri. Hivyo kilichofanyika ilikuwa ni kukivunja kichwa (Lowassa) kwa kosa lililofanywa na ulimi (rais). Na ndio maana katika kikao kimojawapo cha chama Lowassa alimuhoji mwenyekiti kuwa ni jambo gani ambalo yeye aililifanya ambalo yeye hakujua au kumtuma?
Hivi majuzi kamati ya bunge ya hesabu za serikali iiwasilisha bungeni taarifa kuhusiana na akaunti ya Esrow. Ndani yake ilipendekezwa kuwajibishwa na kushitakiwa kwa viongozi mbali mbali wakiwamo mawaziri na Waziri mkuu. Lakini kamati hii nayo ilifanya kama ile ya Mwakyembe. Wakati wa kuwasilisha taarifa yake, Deo Filikunjombe akiwa anasoma baada ya kumpokea Zitto alinukuu kitabu cha Mwl Nyerere ambapo alisema "… mnaweza kumwondoa waziri mkuu na nchi ikabaki imara lakini hamwezi kumwendoa rais bila nchi kuyumba…" Kwa maelezo yake alisema kama rais akiondolewa nchi itayumba lakini sio waziri mkuu. Hivyo wakapendekeza waziri mkuu naye awe miongoni mwa watakaowajibishwa.
Kwa maelezo hayo ni wazi kamati iligundua uhusika wa ikulu katika sakata zima la Escrow hivyo moja kwa moja kumgusa rais. Ilionesha wazi jinsi ikulu ilivyoshiriki katika mchakato mzima wa kutoa fedha za Escrow na jinsi baadhi ya maofisa wa ikulu walivyopokea mgano wao. Hivyo kwa sisi wengine wenye akili ‘fupi' tulichoelewa kutokana na nukuu ile ni kuwa rais naye alipaswa kuwajibishwa au kuondolewa lakini alikolewa na kamati kupitia maoni ya Mwl Nyerere yaliyonukuliwa na kamati kutoka katika kitabu cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania" cha baba wa Taifa Mwl Nyerere.
Baada ya kuwasilisha taarifa zao tume zote hutoa mapendekezo ya utekelezaji ambayo serikali kwa maana ya rais ndiye anayepaswa kutekeleza. Kinachotokea ni kuwa mapendekezo yote ya kamati za bunge huwa hayatekelezwi yote au kwa ukamilifu kwakuwa anayepelekewa kutekeza ndiye alipaswa kwanza kuwajibishwa. Hivyo anapelekewa kutekeleza maamuzi ambayo yanamgusa yeye moja kwa moja pamoja na washirika wake ambao anaweza kuwa aliwatuma au wao walimtumia yeye. Na kutokana na hilo ndipo tumeshuhudia utekelezaji wa maazimio ya kashfa ya Richmond mengi kukwamba ingawa yaliwazoa waziri mkuu na mawaziri wawili lakini wahusika wengine waliachwa mpaka wastaafu. Tumeshuhudia pia kutotekelezwa kwa maazimio juu ya katibu mkuu wa wizara ya nishati bwana Jairo wakati ule. Na sasa tunashuhudia kukwama kwa utekelezaji wa maazimio mengi ya bunge katika sakata la Escrow kwa kuwa baadhi ya wahusika walionufaika na pesa hizo wapo ikulu. Kwa sisi wenye akili ‘fupi' tunaweza tukaconclude kuwa wale wa ikulu hawawezi kuadhibiwa kwakua zile walizopata katika mgano hazikuwa zao bali walichukua kwa niaba yake. Tutakuwa tumekosea wapi
Hivyo mitindo inayotumiwa na kamati za uchunguzi zakashfa mbali mbali za kuficha siri za wahusika wakuu au kuogopa kuchukua hatua kutokana na nukuu za Nyerere ndio itakayosababisha nchi iendelee kuwa na kashfa baada ya kashfa kwa kuwa tume zinajitahidi kukata matawi badala ya kung'oa shina na mizizi yake.
Nakumbuka mbunge mmoja alitoa hoja bungeni kuwa bunge limekuwa likitoa maazimio ya utekelezaji lakini mara nyingi yamekuwa hayatekelezwi na akataka bunge litoe msimamo itakuwaje endapo maazimio waliyopendekeza hayatatekelezwa tena kama yale ya Richmond bunge lichukue hatua gani? Hoja hii ilifinyangwa kijanja na spika kwakuwa alijua wanampelekea mtuhumiwa kutekeleza maazimo yanayomgusa moja kwa moja. Maokeo yake tumeyaona. Amesema pesa hazikuwa za umma. Wakati wa EPA alisema pia kuwa hazikuwa za serikali ila zilikuwa zinazagaa zagaa pale benki kuu ndipo wajanja wakazichukua.
Mimi nilivyoelewa kuhusu hiyo akaunti ya Esrow ni kuwa pesa zile ni za Tanesco ambazo ziliwekwa pale ili kusubiri mgogoro baina yakena mdai usuluhishwe ili kama kutakuwa hakuna tatizo ndipo zile pesa zilipwe kwa IPTL. Kwa maana hiyo kwakuwa msuluhishi alikuwa hajaamua mgogoro ule zile pesa zilikuwa ni za Tanesco kwa maana ya kuwa Tanesco hakumlipa mdai wake kwa kuwa mahakama haikusema kuwa zile pesa sasa zilipwe IPTL na kwa maana hiyo Tanesco mpaka sasa hawana risiti ya malipo ya pesa zile kutoka IPTL. Sasa zilitolewaje wakati mgogoro haujamalizwa??!! Pesa zile ni za Tanesco na Tanesco ni shirika la umma hivyo pesa zile ni za umma ambazo kisheria zilikuwa zinasubiri kutatuliwa kwa mgogoro kisha zote zilipwe IPTL au zingine zirudi Tanesco.