Hivi ndivyo NIDA inavyoshughulikia Watanzania Wazawa?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
296
1,000
Wakuu ukweli ni kwamba Wazawa ndio wanaopewa namba za kitambulisho cha Taifa. Kwa Watanzania wenye asili ya Asia wote wana vitambulisho vya Taifa. How come wazawa tunakuwa treated kihivi?

Watanzania wenye asili ya Asia wao wametumia njia zipi kupata vitambulisho? Je, wazawa hawawezi tumia hizo njia?

Kwanini wazawa tunaishia kupewa namba huu ni mwaka wa 3 sasa. Nilijiandikisha mwaka 2017 mwezi wa 12 mpaka sasa nina namba tu.

Tuelezwe vigezo vinavyo tumika kuwapatia Wa Asia wote vitambulisho ilihali sisi tuna pewa namba tu.

Wazazi wetu kule bushi wana namba pekee na wameitumikia hii nchi na wengine kupigana vita vya kumuondoa Iddi Amini.

Hii sio sawa kabisa
 

Emiir

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
23,415
2,000
Vile watumishi wa NIDA wanavyolitizama hili bandiko lako
tapatalk_1584285770354.jpegˡ ˡⁱᵏᵉ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ
 

Frank King

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
1,311
2,000
Serikali ya chama cha mapinduzi ndivyo ilivyo,,,,binafsi nina namba tu,,,,of course walinitumia sms kwamba kitambulisho nikakichukue kipo tayari,,,nikajizoazoa mzima mzima nikafika,kisha nikauliza Kitambulisho na nikawaonyesha na sms waliyonitumia,,,

Jibu walilonipa”HAKIONEKANI,WENDA KIMEPELEKWA KATA,,TUTAKUJULISHA KWENYE NAMBA ZAKO ZA SIMU,,,,ok sikukata tamaa nikaenda kata,,,wakaniambia bado hawajapeleka,vipo vitambulisho vya zamani tu,,,

CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI YAKE NDIVYO WALIVYO.
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
4,029
2,000
Kwani ukipewa No. Ya NIDA si unafanikisha shughuli zako zote bila tabu au kuna sehemu ukitoa No. Bila ID hupati huduma?

Khs wahindi hao ni watoa kitu kidogo maarufu.
 

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,022
2,000
kule. vijijini kwetu wazazi wetu hata hizo namba hawana. na kila siku wanatishiwa kufungiwa laini. wanaishi hawajui kesho yao. tukiwasajilia huku wa namba zetu tunafungwa miaka mitano.


asante awamu ya tano. tumenyooka kweli


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,078
2,000
Nadhani hili suala la familia toka babu, bibi, baba, mama n.k kuhifadhi nyaraka zote muhimu linarahisisha NIDA kutoa vitambulisho bila shida yoyote.

Lakini kwa baadhi ya waTanzania kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuhifadhi nyaraka, vyeti n.k inapofika unahitaji pasipoti , kadi ya NIDA lazima utatakiwa kwenda kutafuta affidavit kwa kuapa mahakamani kupata / kutibitisha nyaraka iliyochakaa kutokana na kutotunzwa vizuri iwe cheti cha kuzaliwa, cheti cha kifo cha baba, babu, mama n.k

Pia suala la baadhi ya wanafamilia kuhama toka maeneo yao na kuhamia mjini pekee yao huku huko tulikotoka kijijini hakuna utamaduni wa kuhifadhi nyaraka muhimu na hii pia inaweza kuwa sababu ya kuchelewa kupata unachotaka kwa haraka maana unaanza moja kutengeneza nyaraka hizo chini ya kiapo wakati waTanzania wengine vitu hivyo wanavyo tayari mikononi in original form.

WaTanzania wenye nyaraka hizi muhimu bila kuapa wanaweza kutibitisha uwaza wao vizuri kwa kuonesha vizazi vyao vilivyozaliwa Tanzania kwa zaidi ya miaka 70 nyuma. Wakati mtu mfano wa Kigoma aliyeweza kufaulu masomo na kuishia Dar es Salaam anakuja na kulowea mjini bila nyaraka hizo muhimu kuonesha uzawa wake bila kutegemea viapo.
 

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
1,580
2,000
Kwani amuwezi ishi bila kulalamika??mnalialia kama watoto wa kambo,kama wenzako wanapata ww unashindwaje si ujiongeze au potezea mazima nayo inawezekana.
 

toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
2,481
2,000
mjomba ulikuwa hujui kwamba nida ni mavi ya mbwa, nlienda temeke nikamkuta dogo mmoja nimesoma nae chuo yan alijiona profesa ana phd wakati kalikuwa kanashika mkia na kalikuwa kamekondeana kama nzi, kalinijibu shit wakati nawaona waarabu wanatoa mlungula wabachukua ID, mjomba nida ni gaguo la malaya kila mtu analichezea, MBWA KABISA HAO SITAK KUWASIKIA *****


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,493
2,000
Wakuu ukweli ni kwamba Wazawa ndo wanao pewa namba za kitambulisho cha Taifa. Kwa Watanzania wenye asili ya Asia wote wana vitambulisho vya Taifa. How come wazawa tunakuwa treated kihivi?

Watanzania wenye asili ya Asia wao wametumia njia zipi kupata vitambulisho? Je wazawa hawawezi tumia hizo njia?

Kwa nini wazawa tunaishia kupewa namba huu ni mwaka wa 3 sasa. Nilijiandikisha mwaka 2017 mwezi wa 12 mpaka sasa nina namba tu.

Tuelezwe vigezo vinavyo tumika kuwapatia Wa Asia wote vitambulisho ilihali sisi tuna pewa namba tu.

Wazazi wetu kule bushi wana namba pekee na wameitumikia hii nchi na wengine kupigana vita vya kumuondoa Iddi Amini.

Hii sio sawa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasikiimbieee nchiii kwikwii
Mengine sifikihukooo
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
7,720
2,000
Wakuu ukweli ni kwamba Wazawa ndo wanao pewa namba za kitambulisho cha Taifa. Kwa Watanzania wenye asili ya Asia wote wana vitambulisho vya Taifa. How come wazawa tunakuwa treated kihivi?

Watanzania wenye asili ya Asia wao wametumia njia zipi kupata vitambulisho? Je wazawa hawawezi tumia hizo njia?

Kwa nini wazawa tunaishia kupewa namba huu ni mwaka wa 3 sasa. Nilijiandikisha mwaka 2017 mwezi wa 12 mpaka sasa nina namba tu.

Tuelezwe vigezo vinavyo tumika kuwapatia Wa Asia wote vitambulisho ilihali sisi tuna pewa namba tu.

Wazazi wetu kule bushi wana namba pekee na wameitumikia hii nchi na wengine kupigana vita vya kumuondoa Iddi Amini.

Hii sio sawa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimekuelewa kwa sehemu kubwa, isipokuwa tu hapo pa mTanzania Mzawa na mTanzania wa Asia.

'Nitty gritty' ya hii pia naweza nikaielewa kwa sehemu kubwa na uzoefu, lakini nadhani kuna kitu tunakikosea.

Hivi mTanzania wa asili ya Asia hawezi kuwa "mTanzania mzawa"?

Hili tu ndilo linalonisumbuaga na mambo ya namna hii.

Akija mkenya hapa, akahamia na akaenda NIDA akapewa kitambulisho, naye tutasema ni "mTanzania mzawa" kwa vile tu rangi yake pekee ni sawa na hii yetu? Kwa sababu najua hakuna sehemu inayouliza wewe ni mTanzania gani katika fomu za maombi ya vitambulisho hivyo.

Maana yangu ni kwamba, kila mtu tumwangalie kwa matendo yake kwanza bila ya kuwahusisha na wengine wanaofanana naye lakini matendo yao hayana dosari.

Najua ugumu wa kuyatetea haya ninayoandika hapa, lakini ndiyo ninayoyaamini.

Hii NIDA inaonekana inaubovu wa aina yake. Mwanzo nilidhani hawapewi fungu la kutosha ili wakamilishe kazi yao; lakini yanapotokea mambo kama haya yanayoelezwa na mleta mada inakuwa wazi kuwa huko NIDA kuna matatizo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom