Hivi ndivyo Mwanaume hutambua kuwa unampenda kwa dhati

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,378
12,571
Niende kwenye mada, sita elezea mada hii nikihusisha na story yangu binafsi ila nitaweka story ya Bondia Hassan Mwakinyo.

Kiukweli ni ngumu sana kumjua mwanaume mwenye nia njema kwa mpenzi wake na mwenye akili ya maisha, sio ngumu tu kumtambua hata kukutana nae ni nadra sana.

Jinsi ya kumpata mwanaume huyo inawezekana, ila si mada ya leo. Pengine waweza kumpata kwa bahati tu na ukawa nae, kwani naye alipata nafasi ya kuwa nawe karibu na kusema kuwa anakupenda.

MADA
Kitu kikubwa ambacho wanaume huangalia kwa Mwanamke tunapokua kwenye mahusiano ni Mwanamke kua muwazi na mkweli, hatupendi janja janja na uwongo.

Mwanamke kuwa muwazi kwa mwanaume ambae umeamchagua kua mwanaume wa ndoto zako ni muhimu sana, ongea nae mwambia yanayo kuhusu, usifikirie kua atakudharau kwa lolote, kama ataonyesha dharau basi huyo sio mtu sahihi kwako.

Mwambie hali yako ya maisha, mwambie unacho waza rohoni mwako na unachopenda maishani, mwambie ndoto zako za baadae.

Mwamini kwa kila jambo kua anaweza na kumthamini na yeye atakuthamini daima.

STORY YA MWAKINYO.
Mwakinyo alipoulizwa, wewe una mpenzi ? Alisema sina kwa sasa na kuanza kuelezea mahusiano yake yaliopita..

Sina mwanamke kwa sasa ambaye naweza sema ananipenda mimi, mwanamke niliyekuwa naye last alikuwa ananipenda kweli, tena sana. Nilikuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, kipindi hicho bado sijawa na mafanikio katika hii fani yangu.

Ilifika wakati nikaona kuliko kumchezea na siwezi kumuoa kwa sasa, bora nimuache aolewe tu na mwanaume mwingine.

Kuna mwanaume alimpata kisha akanieleza na kunionesha, alikuwa na hela ndio lakini niliona hamfai,
Basi nikamwambia achana nae subiri nitakuoa mimi.

Tukaendelea, akaja kunionesha mwanaume mwingine huyo nikaona anafaa, alikuwa na kila kitu na yuko tayari kumuoa, nikakubali aolewe nae.

Kwa sasa yuko kwenye ndoa yake na Ana watoto.

------++++end++++-----------

Hizo ni hekima za Hassan Mwakinyo.

Anakiri mwanamke huyo ndie mwanamke pekee alionesha kumpenda kwa dhati, japo hawakuweza kuwa pamoja kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.
 
kwa maneno mengine huyo mwanamke ameolewa na mwanaume mwingine japo bado anampenda Mwakinyo.

Huyo mwanamke anaishi kwenye hiyo ndoa kwa kuwa Mwakinyo ameamua aishi huko, siku Mwakinyo akimuambia avunje ndoa then inakuwa mwisho!

Huo siyo upendo.
 
kwa maneno mengine huyo mwanamke ameolewa na mwanaume mwingine japo bado anampenda Mwakinyo.

Huyo mwanamke anaishi kwenye hiyo ndoa kwa kuwa Mwakinyo ameamua aishi huko, siku Mwakinyo akimuambia avunje ndoa then inakuwa mwisho!

Huo siyo upendo.
Tukisema mwanamke akubali kuolewa na mwanaume masikini hatuta mtendea haki.

Tafuta pesa ukizipata unakua na haki ya kuowa sasa.

Huyo binti mie naona anajielewa vizuri, kwani pia hujui kua wazuri ni wengi lakini wenye nia nzuri niwa chache ????
Yeye alitaka ndoa na kaipata na mwanaume sio kwamba sio hb ma hb tupo wengi tuuu, ila kutunza mwanamke wengine tunashindwa.
 
Nafikiri hiki kizazi cha sasa kina shida ya kila mtu kujiona 'special'..

Ndo maana mahusiano Yana tabu nyingi
Kila mtu mpweke ingawa Wana sex kila siku
Na watu tofauti..

Mimi nawaulizaga vijana wengi hili swali
Na wengi hawajibu

'what makes you think you are special'?
 
Kwahiyo Mwakinyo kamthaminishia mume bora, huyo demu wake
Kwam huyo demu anamsikiliza Mwakinyo hivyo si hata akimwita atakuja tu

Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
Kibiblia.
Kumpata mke au mume bora inahitaji hekima nyingi sana kutoka kwa Mungu.
Kama huna hapa ndio inakuja ile style ya kwenda kwa mchungaji na kumwambia akuombee au kukuonesha mwenza wako ni yupi ?

Sasa uwe na hakika kweli mchungaji wako ana akili za kimungu.

So, hapo Mwakinyo kasimama kama kijana bora wa mwenyezi Mungu.

note: kupata mtu sahihi inahitaji akili sana na sio rahisi.
 
Nafikiri hiki kizazi cha sasa kina shida ya kila mtu kujiona 'special'..

Ndo maana mahusiano Yana tabu nyingi
Kila mtu mpweke ingawa Wana sex kila siku
Na watu tofauti..

Mimi nawaulizaga vijana wengi hili swali
Na wengi hawajibu

'what makes you think you are special'?
True.

Wanajio wanajua kuchagua na ndio kila siku wanazalishwa na kuachwa.
 
Tukisema mwanamke akubali kuolewa na mwanaume masikini hatuta mtendea haki.

Tafuta pesa ukizipata unakua na haki ya kuowa sasa.

Huyo binti mie naona anajielewa vizuri, kwani pia hujui kua wazuri ni wengi lakini wenye nia nzuri niwa chache ????
Yeye alitaka ndoa na kaipata na mwanaume sio kwamba sio hb ma hb tupo wengi tuuu, ila kutunza mwanamke wengine tunashindwa.
Sifa imeongezeka...Mtumishi,IT saiV Handsome.
 
Maisha ni kitu cha ajabu sana. Story ya mwakinyo inaenda sana na story Kama hiyo kwa rafiki yangu. Yeye na mchumba wake wapo kwenye mahusiano wanaenda mwaka wa tatu huu, jamaa ni mtu mwenye maono makubwa na anafanya kazi kwa bidii sana(yaani kupigania ndoto) binti yeye anatoka kwenye familia nzuri kiasi kiuchumu na hivyo sio yule mwanamke wa kumsumbua jamaa kuhusu pesa zaidi ni jamaa anamuelisha sana hasa mambo ya ujasiriamali maana ni mtu anayesoma vitabu na kutafiti mambo makubwa hasa yahusiyo biashara za mabara(intercontinental trade).
Kwa sasa jamaa ananiambia changamoto yake ni kuwa umri wa binti unaenda na yeye kwa mujibu wa Imani yake ni hadi aweze kubeba majukumu ya kifamilia ndio waweze kuingia ndoani, mtihani ni siku binti akileta demand Kama hiyo hatakuwa na budi Bali kumruhusu aende japo anadai anampenda sana.
 
Back
Top Bottom