Hivi ndivyo matapeli wanavyotumia namba zako za NIDA

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,092
1,433
TCRA walituambia tusajili laini kwa kutumia alama za vidole kwakuwa usajili huo ni imara na salama lakini matapeli wakishirikiana na wasajili line wanafanya yafuatayo.

Unaenda kusajili laini unafata taratibu zote usajili unakamilika anakuambia kuna tatizo usajili haujakamilika hivyo mrudie tena.

Wewe hujui hili wala lile unarudia tena kumbe anakusajilia laini ya pili bila wewe kujua baada ya hapo laini moja unachukua halafu moja anampa tapeli anatumia usajili wako kiuraahiiiiisi unajikuta ushatumika kufanya utapeli

Sasa ikitokea akakwambia turudie tena kusajili komaa line ya kwanza uondoke nayo na ukienda kuijaribu unakuta imekamilika usajili ndugu muwe makini.

Namna ya kuangalia namba zilizosajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho chako cha Taifa(NID)
1) Bonyeza *106# kisha piga (bonyeza OK)

2) Chagua namba 2 = kuangalia namba zilizosajiliwa kwa yako

3) Jaza namba yako ya kitambulisho cha Taifa kisha bonyeza OK

Zitakuja namba zote ulizosajili kwa kitambulisho chako kwa mtandao husika. Mfano: Kama umetumia njia hii kwa laini ya Tigo basi utaziona namba za tigo tu zilizosajiliwa kwa namba yako na kama una namba zaidi ya mtandao mmoja utapaswa kurudia kwa kila mtandao.

Endapo kuna namba huzijui nenda ofisi za mtandao husika na tatizo lako litashughulikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii tahadhari ilishatolewa humu na niliichukua nikajiongeza nilipokuwa nasajili line zangu mmoja wa Tigo akaniambia rudia tena nilichokifanya nikamwambia ahirisha zoezi nitajisajili kwengine maana kila sehemu mawakala wametapakaa ajabu akaniambia basi imekubali lipia tu ile ya mwanzo imekubali.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
1)Bonyeza *106# ok.
kisha chagua namba 2= kuangalia namba zilizossjiliwa kwa nida yako.
jaza namba yako ya nida kisha piga ok.
zitakuja namba zako zoote ulizo sajili kwa nida kwa mtandao husika.kama umetumia njia hii kwa laini ya tigo basi utaziona namba za tigo tu zilizosajiliwa kwa nida yako.alikadhalika pia na voda,airtel,halotel n.k.

Sasa kama kuna namba huzijui nenda tigo shop ama voda shop kapige pini namba ambazo huzitambui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna namba ya tigo niliangalia kwa kutumia ule utaratibu wa TCRA kuangalia namba ambazo kitambulisho chako kimesajili nikakuta mbili sizijui nikaenda tigoshop kuzifuta haraka sana,najaribu kuwaza kwa wasio na taarifa juu ya kuangalia idadi ya namba ambayo kitambulisho kimesajili huenda ndio hizo ambazo matapeli wanazidi kuzitumia,mwisho wa siku kesi ya mwenye kitambulisho.
 
Ni zipi hizo namba ili nami nijue, maana kuna.line moja nilirudia mara 2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii tahadhari ilishatolewa humu na niliichukua nikajiongeza nilipokuwa nasajili line zangu mmoja wa Tigo akaniambia rudia tena nilichokifanya nikamwambia ahirisha zoezi nitajisajili kwengine maana kila sehemu mawakala wametapakaa ajabu akaniambia basi imekubali lipia tu ile ya mwanzo imekubali.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Du!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1)Bonyeza *106# ok.

kisha chagua namba 2= kuangalia namba zilizossjiliwa kwa nida yako.

jaza namba yako ya nida kisha piga ok.
mm nilitumia utaratibu huu wa *106#kwenye voda nikakuta kuna namba ya voda siijui na ipo hewani ukipiga inaita.
basi nakapiga cm huduma kwa wateja kuwa hiyo ni namba yangu waizuie nimeibiwa sim,nikawatajia namba ya nida wakaipiga pini.
nilivyopata muda nikai renew.nikaitumia buku mpesa salio likasoma elfu 45.
nikarudi tena vodashop kufanya pin reset kurekebisha namba ya siri.nikatoa mzigo laini nikatupa nikarudi tena voda kuifuta usajili.

Hahahahaha. Umetisha mkaliiii

Ila mkuu, ulipata wapi namba tano zile wanazotakaga?
 
mm nilitumia utaratibu huu wa *106#kwenye voda nikakuta kuna namba ya voda siijui na ipo hewani ukipiga inaita.
basi nakapiga cm huduma kwa wateja kuwa hiyo ni namba yangu waizuie nimeibiwa sim,nikawatajia namba ya nida wakaipiga pini.
nilivyopata muda nikai renew.nikaitumia buku mpesa salio likasoma elfu 45.
nikarudi tena vodashop kufanya pin reset kurekebisha namba ya siri.nikatoa mzigo laini nikatupa nikarudi tena voda kuifuta usajili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilikuta minamba nisiyoijua na nikakumbuka msajili alifanya uhuni kwa kusajili namba nyingine kinyemera.
 
1)Bonyeza *106# ok.
kisha chagua namba 2= kuangalia namba zilizossjiliwa kwa nida yako.
jaza namba yako ya nida kisha piga ok.
zitakuja namba zako zoote ulizo sajili kwa nida kwa mtandao husika.kama umetumia njia hii kwa laini ya tigo basi utaziona namba za tigo tu zilizosajiliwa kwa nida yako.alikadhalika pia na voda,airtel,halotel n.k.

Sasa kama kuna namba huzijui nenda tigo shop ama voda shop kapige pini namba ambazo huzitambui.

Sent using Jamii Forums mobile app

Daah we jamaa umefaa sana aiseee nimekuta kwangi bumbe zipo nne za tigo haa tatu nazitambua ila moja hapa, siitambui.
 
Back
Top Bottom