Hivi ndivyo Marekani kupitia Shirika lake la CIA walivyotekeleza Mapinduzi nchini Guentamala na kuondosha Serikali ya Kiraia ya Jacob Arbenz

MLO

Senior Member
Apr 2, 2012
194
79
Na. Belvin Kagoma

Miaka ya 1970 nchi ya marekani walipitisha Sheria maalumu ya Uhuru wa Kupata Taarifa (Freedom of Information Act). Moja wapo ya vipengele vya Sheria hii ni kulitaka Shirika la Kijasusi la CIA kuweka hadharani taarifa zao za siri kila baada ya miaka 50.

Hii imesaidia kupatikana kwa taarifa nyingi nyeti zihusuzo shirika la CIA, taarifa ambazo zilikuwa ni siri kubwa huko nyuma.

Katika makala hii nitaeleza kwa kina moja ya matukio muhimu ambayo yanadhihirisha namna ambavyo CIA inafanya kazi yake kuhakikisha kuwa ulimwengu wote unakuwa namna ambavyo taifa la marekani inataka uwe. Taarifa hizi ziliwekwa wazi mwaka 2004 na CIA kama ambavyo wanatakiwa na sheria ya uhuru wa habari (Freedom of Information Act).

👉Guatemala; Amerika ya Kusini
Mwezi machi mwaka 1952, Mwanamama Virginia Hall afisa nguli wa shirika la Ujasusi la CIA alitua kwa paradhuti nchini Guatemela kwa ajili ya kufanya upelelezi maalumu katika nchi hiyo.

Mwanamama huyu alikuwa ni mlemavu wa mguu mmoja. Mguu mwingine ulikatwa kutokana na jeraha kubwa alilolipata miaka ya nyuma kutokana na kupigwa risasi akiwa katika kazi maalumu nchini Uturuki. Hivyo mguuu mmoja ulikuwa bandia.

Kilichompeleka nchini Guatemala ilikuwa ni kazi maalumu aliyotumwa na mkurugenzi wa CIA kuchunguza taarifa waliyoipata kutoka kwa kampuni ya matunda ya kimarekani yenye mashamba nchini Guatemala kwamba kuna hatari ya masilahi ya kampuni za kimarekani yakatetereka kutokana na muenendo wa serikali ya Guatemela.

Kwahiyo kazi ya mwanamama Virginia Hall ilikuwa ni kuchunguza mwenendo wa serikali, pia kuangalia kama kuna tishio lolote kwa masilahi ya kampuni za kimarekani kisha atoe mapendekezo ya nini kifanyike.

Mzozo wa kimasilahi kati ya serikali ya Guatemala na kampuni za kimarekani ulianza kama ifuatavyo;

Kabla ya mwaka 1950, nchi ya Guatemala ilikuwa inaongozwa na madikteta wa kijeshi ambao walijimilikishanchi ya Guatemala kama Mali yao binafsi.

Moja wapo wa madikteta hawa wa kijeshi aliitwa Jorge Ubico ambaye alizipendela kampuni za kigeni hasa kampuni za marekani kwa kiwango ambacho kilitishia hata uchumi wa nchi yake.

Moja wapo ya kampuni za kimarekani zilizopendelewa sana iliitwa UFC (United Fruit Company). Kampuni hii iliendesha shughuli za kulima mashamba makubwa ya matunda hasa hasa zao la ndizi.

Kampuni hii ilimiliki asilimia kubwa ya ardhi na mashamba nchini Guatemala chini ya utawala wa dikteta Ubico pia ndio ilikuwa kampuni inayoongoza kwa uajiri nchini Guatemala na pia ilikuwa ndiyo kampuni inayoongoza duniani kwa uzalishaji na kuuza tunda la ndizi.

Kutokana na uswahiba waliokuwa wamejenga na Rais Ubico walifanikiwa kumshawishi dikteta huyo kutunga sheria ya kupiga marufuku wafanyakazi kugoma pale wakiona wanalipwa malipo kiduchu. Pia kampuni hii ilipewa ruhusa maalumu ya Rais kutolipa kodi ya aina yoyote ile ndani ya nchi ya Guatemala.

Na kama hiyo haitoshi Rais Ubico alibinafsishiwa bandari kuu ya nchi Puerta Barrios na kuifanya kampuni ya UFC kuwa na utajiri na ishawishi zaidi. Ilifikia kipindi Mapato ya kampuni ya kampuni ya UFC yalivuka Pato la Taifa la nchi ya Guatemala.

Wananchi wengi wa Guatemala walikuwa hawaridhishwi na mwenendo wa serikali na hivyo wakaungana na Jeshi la nchi hiyo kumpindua Rais Jorge Ubico.

Baada ya mapinduzi Jeshi la nchi likaitisha uchaguzi wa kidemokrasia ambapo Jose Alevaro Alishinda kiti cha uraisi na miaka michache baadae ukafanyika uchaguzi mwingine wa kidemokrasia ambapo Rais Jacob Arbenz Alishinda.

Baada ya rais Arbenz Kuingia madarakani akaweka dhamira ya dhati kuijenga upya nchi ya Guatemala.

Kwanza kabisa akaamuru bandari kuu ya nchi Puerto Barrios irudishwe na kuendeshwa na serikali badala ya kampuni ya UFC. Pia akapitisha Sheria maalumu iliyojulikana kama 'Agririan Act' ili kusaidia wananchi wengi kupata ardhi ya kulima na kufanya shughuli za kiuchumi.

Moja ya kampuni ambazo ziliathiriwa na Sheria hii ilikuwa ni kampuni ya UFC ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa inamiliki zaidi ya nusu ya ardhi nchini Guatemala lakini kiasi kikubwa cha ardhi hii walikuwa hawaiendeleza kwa kilimo wala shughuli yoyote.

Serikali ikailipa UFC kiasi cha dola 2 kwa kila ekari na kuirudisha ardhi kwa wananchi. (UFC walinunua ardhi hii kwa dola 1 kwa ekari kipindi cha utawala wa Ubico).

Ardhi pekee ambayo waliwaachia ilikuwa ni ile ambayo walikuwa wameiendeleza kwa kuilima.

Pia serikali ikafuta Sheria ya kuwazuia wafanyakazi kugoma ikitokea wakihisi kuwa wanalipwa fedha kiduchu kulingana na kazi wanayoifanya. Pia serikali ikaamuru kampuni zote kuongeza kiwango cha ujira kwa wafanyakazi wote wa viwandani na mashambani.

Hatua hizi zilizochukuliwa na Rais mpya wa Guatemala ziliungwa mkono na kuwafurahisha wananchi lakini ilikuwa ni pigo kubwa kwa kampuni ya UFC ambayo ilikuwa imejijengea mazoea ya kufanya kazi kwa kupendelewa na serikali ya dikteta Ubico aliyetolewa madarakani.

Hatua hizi zilikuwa ni za lazima ili kufufua uchumi wa Taifa la Guatemala lakini kampuni ya UFC hawakupendezwa nazo kwani ziliathiri moja kwa moja maslahi yao ya kibiashara.

Ndipo hapa ambapo kampuni ya UFC iliwasiliana Bw. John Dulles waziri wa mambo ya nje wa marekani wa kipindi hicho na kumueleza namna ambavyo kampuni yao inavyoathiriwa na hatua za serikali mpya ya Guatemala.

Ifahamike kwamba kwa kipindi hiki UFC ilikuwa moja ya makampuni makubwa zaidi ya kimarekani ikiwa inatengeneza faida ya zaidi ya dola milioni 300 kila mwaka. Hivyo suala hili lilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa serikali ya marekani.

Waziri Dulles baada ya kupewa taarifa hii kutoka kwa Wakurugenzi wa UFC akachukua hatua kadhaa ambapo moja wapo ya hatua kubwa alizo chukua ilikuwa ni kumbadilisha Balozi wa marekani nchini Guatemala na kumuweka shushushu wa CIA Bw John Peuorify Balozi huyu alipewa maagizo maalumu ya kumshinikiza Rais Arbenz alegeze misimamo yake na kama hayuko tayari kulegeza misimamo hiyo kwa kuhofia kufarakana na wananchi wake basi atoe upendeleo maalumu kwa kampuni za kimarekani.

Baada ya Balozi mpya shushushu John Peuorify Kufika Guatemala na kuweka mashinikizo haya, Rais Arbenz aliyapinga mashinikizo yote haya na akaendelea na msimamo wake wa kuweka uwiano sawa kwa makampuni yote yalimo ndani ya Guatemala na kuendelea kuhakikisha kuwa anafufua uchumi wa nchi yake.

Baada ya miezi kadhaa ya kumshawishi Rais Arbenz Alegeze msimamo kutozaa matunda yoyote ndipo hapa waziri Dulles akawasiliana na Dwight Eisenhower ambaye akikuwa Rais kwa kipindi hicho.

Baada ya changamoto hii kufikishwa mezani kwa Rais Eisenhower Alipendekeza kuwa CIA wahusishwe na wasikie wanatoa ushauri gani.
Hivyo basi moja kwa moja Waziri Dulles akiwasiliana na Mkurugenzi wa CIA na kumueleza juu ya changamoto inayowakabili.

Mkurugenzi huyo wa CIA baada ya kuelezwa kuhusu changamoto iliyopo, akapendekeza kuwa licha taarifa alizonazo kutoka kwa moja ya mashushushu wao nchini Guatemala (balozi wa marekani) lakini anahitaji kufanya uchunguzi zaidi ili aweze kutoa ushauri sahihi.

Akaongeza kuwa kutokana na uzito na unyeti wa suala hilo, inabidi atume walau moja ya wapelelezi wa CIA aliyepo ndani ya kikosi maalumu kilicho chini ya idara maalumu ndani ya shrika la CIA. Kitengo/idara hiki maalumu ndani ya CIA kilijulikana kama SAD (Special Activities Division).

Watu wanafahamu umahiri na upekee wa wa shirika la CIA lakini ndani ya CIA pia kuna na kikosi maalumu cha kipekee kwa ajili ya kazi nyeti maalumu na kazi hizo zilisimamiwa na maafisa wa Idara ya SAD ndani ya CIA. Yani kwa maneno mengine idara ya SAD ilikuwa na maafisa wa kipekee ndani ya shirika la kipekee (CIA).

👉Upekee wa SAD ndani ya CIA ni nini??
Kutokana kuongezeka kwa changamoto za kimataifa , ambazo nyingine zinatishia usalama au maslahi ya mrekani lakini marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana kujiepusha na lawama kutoka jamii ya kimataifa ndipo hapo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya suala hili.

Ndipo hapa ambapo serikali ya marekani ikaagiza shirika la kijasusi la CIA kuanzisha kitengo maalumu ndani yake ambacho kitakuwa na maafisa (wanajeshi) ambao wanaweza kutekeleza oparesheni yoyote ya kijeshi kwa kujitegemea pasipo kuhusisha serikali ya marekani.

CIA wakaanzisha idara maalumu ndani yake na kuuita Special Activities Division au kwa kifupi SAD ambayo idara yenyewe ilikuwa na maafisa wa siri ambao hawabebi vitambulisho na majina yao ni siri kubwa hayawezi kupatikana hata kwenye orodha ya maafisa wa CIA.

Lengo kubwa la kuanzishwa kwa idara hii ni kutekeleza oparesheni maalumu za kijeshi au proaganda na iikitokea wakakamatwa au kushitukiwa basi serikali ya marekani wanawakana kuwa si maafisa wao (Plausible deniability).

Kwahiyo kitengo hiki kilikuwa kinafanya kazi kwa niaba ya serikali ya marekani lakini kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serkali ya marekani.

Ndani ya Idara hii ya SAD kuna vitengo viwili;
Kitengo cha kwanza kinaitwa Political Action Group: kitengo hiki kazi yake kubwa ni kufanya ushawishi wa kisiasa (political influence), oparesheni za kisaikolojia (psychological operations) na vita za kiuchumi (Economic Warfares). Pia kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kitengo hiki kimeongezewa jukumu la vita za kimtandao (cyberwarfares).

Tuchukulie kwa mfano; katika nchi fulani kuna serikali au mwenendo wa serikalin uatishia maslahi ya Marekani basi kitengo hiki kinaingia kwa siri kubwa na kufanya mojawapo ya mambo ambayo nimeyaorodhesha hapo juu.

Moja ya matukio ambayo kitengo hiki kimehusika sana na CIA wamekiri kwenye nyaraka zilizowekwa wazi mwaka 2004 ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka 1953.

Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha kikomunisti cha Italia kushinda uchaguzi mwaka 1960. Pia kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya siri iliyoitwa Operation Mockingbird katika taifa la marekani. Oparesheni hii ilikuwa na lengo la 'kucontrol' habari zinazoandikwa na Vyombo vya habari nchini humo.

Oparesheni hii imekuja kupingwa vikali siku za karibuni na baraza la seneti kwa kuwa sheria hairuhusi CIA kufanya oparesheni yeyote ndani ya ardhi ya marekani.

Kitengo cha Pili kinaitwa Special Oparatins Group (SAG) na kazi yake ni kama ifuatavyo;
Kitengo hiki kinajumuisha wanajeshi wenye weledi wa hali ya juu kutekeleza malengo ya kivita pasipo kujulikana uhusika wa serikali ya marekani.

Ili kulinda utambulisho wao, wanajeshi wa kikosi hiki maalumu hawavai sare za jeshi wala kubeba vitambulisho.

Inasemekana kuwa hiki ndio kikosi maalumu cha oparesheni za kijeshi chenye usiri mkubwa nchini marekani.

Maafisa wa kitengo hiki wanapatikanaje??
Maafisa wote wanaojiunga katika kitengo hiki maalumu cha SAD wanachaguliwa kutoka katika vikosi vingine vya weledi vya jeshi la marekani mfano Army Rangers, Combat controllers, Delta Force, 24 th STS, US Army Special Forces, SEALs, Force Recon n.k.

Wakishakuchaguliwa wanapelekwa katika kituo maalumu cha mafunzo ya CIA kilichopo Virginia kinachojulikana kama Camp Peary (au maarufu kama 'The Farm') ambapo miezi 18 ya kwanza wanafundisha kuhusu intelijensia na ushushushu.

Baada ya miezi 18 hiyo wanapelekwa kwenye kituo kingine cha CIA kilichopo California ambacho kinajulikana kama 'The Point'.

Hapa wanafundishwa mafunzo ya hali ya juu ya kijeshi ambayo hayapatikani kwa kiwango hicho katika vikosi vingine vya marekani.
Mfano wanafundishwa; mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi (special hand to hand combat), kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi la marekani na nchi za kigeni, ufuatiliajj adui (tracking), Kukabiliana na hali ngumu kwenye mamzingira ya kawaida na nyikani ( extreme survival and wilderness train ing), Kumkwepa aduia, kuzuia adui na kutoroka adui (evasion, Resistance and escape - SERE) na pamoja na mafunzo hayo anaongezewa kozi maalumu ya kutambua fiziolojia ya binadamu (Udaktari).

Afisa ambaye anafuzu mafunzo haya anakabidhiwa katika idara ya SAD ndani ya CIA na anatambulika kama "Afisa Mwenye Mbinu Maalumu" (Specialized Skills Officer).

Katika oparesheni zao maafisa hawa huwa wanazitekeleza katika vikundi vya watu wachache sana wasiozidi sita na oparesheni nyingine zinatekelezwa na Afisa mmoja pekee.

Katika Ofisi za CIA kitingoji cha Langley jijini Virginia kuna ukuta wa majina ya Maafisa wa CIA waliotunikiwa tuzo za heshima kutoka na utumishi wao uliotukuka ( Distinguished Intelligance Cross na Intelligence Star). Majina ya maafisa wengi kwenye ukuta huo ni ya wale waliotumikia kitengo cha SAD ndani ya CIA.

Kwa kuzingatia kwamba makala hii inalenga kuzungumzia uhusika wa CIA katika mapinduzi ya serikali ya Guatemala. Hivyo basi tuone mifano michache sana ya oparesheni zilizotekelezwa na kitengo hiki cha SAD ndani ya CIA. Nitaeleza kwa ufupi ili tusitoke nje ya lengo kuu (mapinduzi ya Guatemala).

Ni idara hii maalumu ya CIA ambayo ilikabidhiwa raia wanne wa Tibet kutoka kwa kaka mkubwa wa kiongozi wa kiroho wa Tibet Mtukufu Dalai Lama ambapo idara ya SAD iliwapa mafunzo ya kikomando watibeti hao kisha wakawarudisha Tibet kutafuta raia wengine 300 ambao SAD iliwapa mafunzo ya kijeshi kwa siri katika kisiwa cha Saipan na mwezi oktoba SAD ikawaongoza wanajeshi hawa mpaka Tibet kuanzisha vuguvugi la kudai kujitenga na China.

Pia ni kikosi maalumu hiki cha idara ya SAD ambacho kilimtorosha kwa siri mtukufu Dalai Lama kwa kupita katikati ya majeshi ya China yaliyokuwa mpakani na kumpeleka India.

Mpaka leo haijulikani ni namna gani waliweza kufanya tukio hili.
Ni idara hii ya SAD ndani ya CIA ambayo ilihusika kuwapatia mafunzo ya kijeshi raia wa Cuba waliokuwa wanaishi uhamishoni na kuwaongoza katika jaribio la kumpindua Fidel Castro. Mapigano haya yakihistoria yalidumu kwa siku tatu na yanajulikana kwa jina maarufu la 'Bay Of Pigs Invasion'.

Jaribio hili la mapinduzi halikuwezekana na ndilo lililochangia kudorara kwa mahusiano kati ya Marekani na Cuba mpaka leo hii.
Kwa mujibu wa nyaraka za siri za CIA zikizowekwa wazi mwaka 2004. Amri ya kumpiga risasi Che Guevara katikakati mwa miaka ya 1960 ilitoka kwa makomado wa SAD.

Ilikuwaje; Jeshi la msituni lililojiita Jeshi la Ukombozi la Bolivia (National Liberation Army of Bolivia) lilianzisha vita dhidi ya serikali ya Bolivia ambayo ilikuwa inaungwa mkono na Marekani. Jeshi hili likuwa na vifaa vya kisasa na liliungwa mkono na mwanamapinduzi Che Guevara.

Katika za mwanzo za mapigano jeshi hili la waasi lilionekana kushinda dhidi ya majeshi ya serikali.

Ndipo hapo CIA wakatuma makomando wa kitengo cha SAD ambao walienda kutoa mafunzo kwa majeshi ya Bolivia katika milima Camiri. Na baada ya hapo wakawaongoza kupigana na waasi na kufanikiwa kuwashinda. Kisha makomando wa SAD wakawaongoza makomando wa jeshi la Bolivia (Bolivia Special Forces) kumkamata Che Guevara ambapo Mara tu baada ya kukamatwa komando wa SAD aliyeitwa Felix Rodriguez akaamuru auwawe.

Hii ni mifano michache kati ya mifano mingi amabayo CIA kwa kutumia kitengo cha SAD wameendesha opesheni maalumu za kijeshi katika nchi nyingi.

Ingawa Rais wa marekani ndiye anayetoa amri ya kufanyika kwa operesheni hizi za kuvamia kijeshi nchi nyingine au kuongoza mapinduzi ya serikali halali duniani kote lakini analindwa na sheria ya Marekani ambayo inampa Rais uwezo wa kukana uhusika wa Rais wa marekani kutoa amri au kufahamu kinachofanywa na kitengo hiki. (Plausible Deniability).

Sheria hii ilitingwa mwaka 1947 inajulikana kama National Security Act. Pia Sheria hii ilitiliwa mkazo na tamko la rais namba 12333 (Executive Order 12333) lenye kichwa cha habari National Intelligence Activities.

Naamini tumeelewa vya kutosha kitengo maalumu cha CIA cha Special Activities Division (SAD) namna kinavyofanya kazi.
👉TUREJEE KATIKA MAPINDUZI YA GUATEMALA NA UHUSIKA WA CIA.

Taarifa iliyorudishwa na shushu wa CIA mwanamaa Virginia Hall ziliendana kabisa taarifa za shushushu John Peurofy aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Guatemala.

Kwamba Sera za Rais Arbenz zilikuwa zinatishia uhai wa makampuni ya kimarekani nchini Guatemala na mbaya zaidi Rais Arbenz alikuwa hataki kulegeza msimamo.

Hivyo basi mwaka 1952 dikteta wa Nicaragua aliyeitwa Anastosio Somoza Garcia alifanya ziara ya kiserikali nchini marekani.

Katika kikao chake Ikulu ya marekani na Rais Dwight Eisenhower akamueleza kuwa kama atapatiwa silaha za kutosha ana uwezo wa kumuondoa madarakani Rais Arbenz wa Guatemala.

Wazo hili lilimpendeza Rais Eisenhower na akaagiza CIA washirikiane na serikali ya Nicaragua kuandaa mpango wa kumuondoa madarakank Rais Arbenz wa Guatemala

👉OPERATION PBFORTUNE
Baada ya CIA kupewa agizo hilo na Rais wakatengeneza mpango maalumu waliouita Operation PFFORTUNE. lengo kuu la mpango huu ulikuwa ni kuipindua serikali ya Guatemala kwa kutumia jeshi la Nicaragua.

Pia CIA wakawasiliana na Manuel Rejemez dikteta wa Venezuela wa kipindi hicho aliyeungwa mkono na marekani pia wakawasiliana na Rafael Trujillo dikteta wa Dominican Republic ambaye pia aliungwa mkono mpango Marekani na wote wakakubalina na mpango huo wakiahidi kutoa fedha na mafunzo kwa wanajeshi wa Nicaragua.

Baada ya mpango kuonekana umekamilika CIA walitumia meli ya kampuni ya UFC (United Fruit Company) kubeba silaha nzito za kijeshi kuelekea nchini Nicaragua ambapo walidanganya kwa kuwajulisha mamlaka za bandari kuwa mzigo huo ulikuwa ni vifaa vya kilimo vya kampuni ya UFC.

Meli ikaanza safari na kukaribia kabisa Nicaragua lakini zikaja taarifa za kusikitisha mno.

Rais wa Nicaragua Dikteta Anastasio Somoza alikuwa ni mtu wa majivuno mno. Na majivuno take yalisababisha kwenye kikao kimoja cha baraza lake la Mawaziri akajivuna kuwa yeye ni kiongozi makini mpaka imefikia hatua serikali ya Marekani kumuamini na kumuomba aongoze mapinduzi ya kumtoa madarakani Raid Arbenz wa Guatemala.

Baada ya taarifa hii ya siri kuropokwa mbele ya mawaziri, ilivuja mpaka kumfikia mwenyewe Rais wa Guatemala.

Arbenz akaitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo alitoa hotuba kali kuilaani Marekani kwa mpango huu na jamii ya kimataifa iliposikia habari hii iliilaani vikali marekani.

Hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kuamuru Meli iliyobeba silaha igeuze na kurejea Marekani.

Operation PBFORTUNE ikafia hapa kwa aibu kubwa.

👉OPERATION PBSUCCESS
Baada ya oparezheni ya kwanza kushindwa, CIA ikaomba idara yake maalumu ya SAD kutengeneza mpango maalumu wa kumuondoa madarakani Rais Arbenz.

SAD wakaja na mpango waliouita 'Operation PBSUCCESS' ambapo katika mpango huo walianisha kuwa ni lazima njia zote mbili zitumike ili kumuondoa madarakani Rais Arbenz.

Yaani ni lazima itumike prooaganda, ambapo watatumia kitengo chao kidogo cha Special Action group (kwa ajili ya propaganda na vita ya kisaikolojia) pia kitengo chake kidogo cha Special Activities group kitatumika kwa ajili ya shambulio la kijeshi.

Kwanza kabisa wakafungua ofisi ndogo maeneo ya Opa-locka Florida ambapo ndiyo yalikwa kama makao makuu ya Operation PBSUCCESS.

Propaganda:
kitengo maalumu cha SAG wakaanzisha kituo cha redio kilichoitwa "Voice Of Liberation" ambacho kilirusha matangazo nchini Guatemala kikidai kuwa kinamilikiwa na wanajeshi waasi walioko msituni ma dhima yao ilikuwa ni kumuondoa Rais Arbenz.

Ili kuleta ufanisi zaidi CIA wakatumia makomando wao kuharibu antena za redio ya Umma ya serikali hivyo kukifanya redio yao ya VOL kusikika pekee nchini Guatemala.

Pia walitimia muda wote kutangaza ni namna gani Arbenz anahiharibu nchi ya Guatemala.

Taratibu sumu ikapandikizwa kwenye vichwa vya wananchi wa Guatemala.

Pia CIA walitumia ndege kudondosha vipeperushi mara kadhaa kwa wiki wakimtaka Rais Arbenz ajiuzuru. Sumu ikaendelea kupandikizwa.

Pia likaja kongamano la nchi za Bara America (Organisation Of American States) Marekani wakashinikizwa iongezwe Agenda ya "Kupinga Ukomunist Kwenye Bara Amerika".

Kitendo cha hiyo Agenda kujadiliwa tu sumu ikazidi kuenea kuwageuza miyo ya watu dhidi ya Rais Arbenz.
Oparasheni za kijeshi;

Makomando wa SAD wakawasiliana na Generali Muasi Castillo Armas aliyeishi uhamishoni nchini Nicaragua wakimuomba wamtumie baada ya miaka ya nyuma kujaribu kufanya mapinduzi bila mafanikio.

Walichomuahidi ni kwamba akikubali kushirikiana nao basi watamfanya kuwa Rais baada ya mapinduzi. Na akaelezwa akusanye wananchi wengine wa Guatemala wanaoishi uhamishoni na kuunda jeshi wao watampatia silaha na fedha ya kuwalipa wanajeshi wake.

Generali Armas akakusanya wanajeshi 300 na CIA wakampatia dola 225,000 kwa ajili ya kujikimu yeye na jeshi lake.

Kisha wakafundisha wanajeshi kadhaa wa wa Generali Armas uruabani wa kijeshi na kazi yao ilikuwa moja tu. Kwa kutumia ndege za kivita walizopewa na CIA walikuwa wanavizia na kulipua miundombinu kadhaa nchini Guatemala kama vile madaraja na maghala ya silaha.

Uharibifu haukuwa mkubwa sana lakini ulitosha kuchochea hofu ambayo tayari ilikuwa imepandikizwa kwa wananchi wa Guatemala.
Kisha redio VOL ikatangaza kuwa muda wa mapinduzi umewadia na ndani ya wiki hiyo Rais Arbenz anang'olewa madarakani na wazalendo wa Guatemala walioko mpakani.

Rais Arbenz akaulizia taarifa za intelijinsia na akaambiwa kuwa ni kweli kuna wanajeshi wanaonekana mpakani mwa Guatemala na Nicaragua.

Rais Arbenz pasipo kujua, akaingia mtegoni akaamuru jeshi lote lielekee mpakani kusambaratisha waasi.

Walipofika mpkani walishangaa kukuta wanajeshi 180 pekee wa Generali Armas ambao waliwasambaratisha kwa masaa machache huku wanajeshi 30 pekee walisalia na kurudi upande wa pili wa mpaka nchini Nicaragua alipo Generali Armas.

Rais Arbenz akachanganyikiwa asijue maana ya fumbo hilo. Akijiingiza zaidi kwenye mtego. Akaamuru majeshi yasitoke mpakani kwani anaamini wanajeshi hawa ni chambo tu lakini lazima kuna wengine watakuja.

Hiki ndicho walichokitaka marekani. Kesho yake Radio ya VOL ikatangaza kuwa kwa kuwa majeshi ya serikali yanatumia nguvu kubwa kuua wazalendo hivyo basi marekani inaungana na waasi hao kwa kutuma jeshi lake kufanya uvamizi na kumuondoa Rais Arbenz.

Jioni ya siku hiyo marekani wakatoa tamko kali kuipinga serikali ya Rais Arbenz pasipo kuthibitisha wala kukataa kama wanaungana kijeshi na waasi.

Hii ilitosha kupasua mioyo ya wananchi na wanajeshi wa Guatemala. Wote walifahamu kama marekani anaingia vita hiyo hakuna uwezekano wowote wa majeshi ya Guatemala kushinda vita.

Wanajeshi wa serikali wakawasiliana na Generali Armas kuwa kama watakubali 'kusarenda' ni hatua gani atachukua dhidi yao??
Generali Armas akawajibu kuwa kwa maslahi mapana ya Taifa atawasamehe na kuwarudisha kazini.

Kesho yake majeshi ya serikali yaliyojo mpakani yakatangaza kuwa hawako tayari kupigana kwa niaba ya Rais Arbernz na wanamtaka ajiuzulu kwa maslahi ya taifa.

Rais Arbenz akachanganyikiwa zaidi akaitisha kikao na viongozi wa vyama vya wakulima na wafanyakazi akiwaomba wawashawishi wanachama wao wapewe silaha na kupigana kuitetea nchi yao.

Viongozi wa vyama wakakubali wakatoa matangazo nchi nzima wananchi wajitokeze kushika silaha kutetea nchi yao na wanatakiwa kesho yake wote wafike katikati ya mji kukabidhiwa silaha.

Jambo la aibu ni kwamba wananchi 120 pekee ndio walijitokeza huku wengine wote wakianzisha maandamano kumtaka Rais Arbenz ajiuzulu kwa maslahi ya Taifa.

Taarifa hii ikamfikia Generali Armaz na CIA. Generali Armas akampa amri ya mwisho Rais Arbenz kuwa ajiuzulu kwa hiari ndani ya Massa 24 na atahakikisha anamuacha aondoke kwa amani ndani ya Guatemela na kwenda kuishi uhamishoni.

Kama hataki kujiuzulu kwa hiari atatumia jeshi ambalo sasa liko chini yake kumuoindua na kumfunga gerezani.

Rais hakuwa na chaguo, jioni ya siku hiyo tarehe 27 June 1954 kwa uchungu, Rais Jacobo Arbenz aliutangazia umma kuwa anajiuzulu.
Na Generali kama alivyomuahidi akamruhusu aondoke kwa amani kwenda kuishi uhamishoni.

Kesho yake Generali Castillo Armas akawa Rais mpya wa Guatemala.

Na huu ndio ukawa mwanzo wa nchi hii kutawaliwa na viongozi wa kijeshi wanaoungwa mkono na marekani.HIVI NDIVYO MAREKANI KUPITIA SHIRIKA LAKE LA CIA WANAVYOITAWALA DUNIA.

Miaka ya 1970 nchi ya marekani walipitisha Sheria maalumu ya Uhuru wa Kupata taarifa (Freedom of Information Act). Moja wapo ya vipengele vya Sheria hii ni kulitaka shirika la kijasusi la CIA kuweka hadharani taarifa zao za siri kila baada ya miaka 50.

Hii imesaidia kupatikana kwa taarifa nyingi nyeti zihusuzo shirika la CIA, taarifa ambazo zilikuwa ni siri kubwa huko nyuma.

Katika makala hii nitaeleza kwa kina moja ya matukio muhimu ambayo yanadhihirisha namna ambavyo CIA inafanya kazi yake kuhakikisha kuwa ulimwengu wote unakuwa namna ambavyo taifa la marekani inataka uwe. Taarifa hizi ziliwekwa wazi mwaka 2004 na CIA kama ambavyo wanatakiwa na sheria ya uhuru wa habari (Freedom of Information Act).

👉Guatemala; Amerika ya Kusini
Mwezi machi mwaka 1952, Mwanamama Virginia Hall afisa nguli wa shirika la Ujasusi la CIA alitua kwa paradhuti nchini Guatemela kwa ajili ya kufanya upelelezi maalumu katika nchi hiyo.

Mwanamama huyu alikuwa ni mlemavu wa mguu mmoja. Mguu mwingine ulikatwa kutokana na jeraha kubwa alilolipata miaka ya nyuma kutokana na kupigwa risasi akiwa katika kazi maalumu nchini Uturuki. Hivyo mguuu mmoja ulikuwa bandia.

Kilichompeleka nchini Guatemala ilikuwa ni kazi maalumu aliyotumwa na mkurugenzi wa CIA kuchunguza taarifa waliyoipata kutoka kwa kampuni ya matunda ya kimarekani yenye mashamba nchini Guatemala kwamba kuna hatari ya masilahi ya kampuni za kimarekani yakatetereka kutokana na muenendo wa serikali ya Guatemela.

Kwahiyo kazi ya mwanamama Virginia Hall ilikuwa ni kuchunguza mwenendo wa serikali, pia kuangalia kama kuna tishio lolote kwa masilahi ya kampuni za kimarekani kisha atoe mapendekezo ya nini kifanyike.

Mzozo wa kimasilahi kati ya serikali ya Guatemala na kampuni za kimarekani ulianza kama ifuatavyo;

Kabla ya mwaka 1950, nchi ya Guatemala ilikuwa inaongozwa na madikteta wa kijeshi ambao walijimilikishanchi ya Guatemala kama Mali yao binafsi.

Moja wapo wa madikteta hawa wa kijeshi aliitwa Jorge Ubico ambaye alizipendela kampuni za kigeni hasa kampuni za marekani kwa kiwango ambacho kilitishia hata uchumi wa nchi yake.

Moja wapo ya kampuni za kimarekani zilizopendelewa sana iliitwa UFC (United Fruit Company). Kampuni hii iliendesha shughuli za kulima mashamba makubwa ya matunda hasa hasa zao la ndizi.

Kampuni hii ilimiliki asilimia kubwa ya ardhi na mashamba nchini Guatemala chini ya utawala wa dikteta Ubico pia ndio ilikuwa kampuni inayoongoza kwa uajiri nchini Guatemala na pia ilikuwa ndiyo kampuni inayoongoza duniani kwa uzalishaji na kuuza tunda la ndizi.

Kutokana na uswahiba waliokuwa wamejenga na Rais Ubico walifanikiwa kumshawishi dikteta huyo kutunga sheria ya kupiga marufuku wafanyakazi kugoma pale wakiona wanalipwa malipo kiduchu. Pia kampuni hii ilipewa ruhusa maalumu ya Rais kutolipa kodi ya aina yoyote ile ndani ya nchi ya Guatemala.

Na kama hiyo haitoshi Rais Ubico alibinafsishiwa bandari kuu ya nchi Puerta Barrios na kuifanya kampuni ya UFC kuwa na utajiri na ishawishi zaidi. Ilifikia kipindi Mapato ya kampuni ya kampuni ya UFC yalivuka Pato la Taifa la nchi ya Guatemala.

Wananchi wengi wa Guatemala walikuwa hawaridhishwi na mwenendo wa serikali na hivyo wakaungana na Jeshi la nchi hiyo kumpindua Rais Jorge Ubico.

Baada ya mapinduzi Jeshi la nchi likaitisha uchaguzi wa kidemokrasia ambapo Jose Alevaro Alishinda kiti cha uraisi na miaka michache baadae ukafanyika uchaguzi mwingine wa kidemokrasia ambapo Rais Jacob Arbenz Alishinda.

Baada ya rais Arbenz Kuingia madarakani akaweka dhamira ya dhati kuijenga upya nchi ya Guatemala.

Kwanza kabisa akaamuru bandari kuu ya nchi Puerto Barrios irudishwe na kuendeshwa na serikali badala ya kampuni ya UFC. Pia akapitisha Sheria maalumu iliyojulikana kama 'Agririan Act' ili kusaidia wananchi wengi kupata ardhi ya kulima na kufanya shughuli za kiuchumi.

Moja ya kampuni ambazo ziliathiriwa na Sheria hii ilikuwa ni kampuni ya UFC ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa inamiliki zaidi ya nusu ya ardhi nchini Guatemala lakini kiasi kikubwa cha ardhi hii walikuwa hawaiendeleza kwa kilimo wala shughuli yoyote.

Serikali ikailipa UFC kiasi cha dola 2 kwa kila ekari na kuirudisha ardhi kwa wananchi. (UFC walinunua ardhi hii kwa dola 1 kwa ekari kipindi cha utawala wa Ubico).

Ardhi pekee ambayo waliwaachia ilikuwa ni ile ambayo walikuwa wameiendeleza kwa kuilima.

Pia serikali ikafuta Sheria ya kuwazuia wafanyakazi kugoma ikitokea wakihisi kuwa wanalipwa fedha kiduchu kulingana na kazi wanayoifanya. Pia serikali ikaamuru kampuni zote kuongeza kiwango cha ujira kwa wafanyakazi wote wa viwandani na mashambani.

Hatua hizi zilizochukuliwa na Rais mpya wa Guatemala ziliungwa mkono na kuwafurahisha wananchi lakini ilikuwa ni pigo kubwa kwa kampuni ya UFC ambayo ilikuwa imejijengea mazoea ya kufanya kazi kwa kupendelewa na serikali ya dikteta Ubico aliyetolewa madarakani.

Hatua hizi zilikuwa ni za lazima ili kufufua uchumi wa Taifa la Guatemala lakini kampuni ya UFC hawakupendezwa nazo kwani ziliathiri moja kwa moja maslahi yao ya kibiashara.

Ndipo hapa ambapo kampuni ya UFC iliwasiliana Bw. John Dulles waziri wa mambo ya nje wa marekani wa kipindi hicho na kumueleza namna ambavyo kampuni yao inavyoathiriwa na hatua za serikali mpya ya Guatemala.

Ifahamike kwamba kwa kipindi hiki UFC ilikuwa moja ya makampuni makubwa zaidi ya kimarekani ikiwa inatengeneza faida ya zaidi ya dola milioni 300 kila mwaka. Hivyo suala hili lilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa serikali ya Marekani.

Waziri Dulles baada ya kupewa taarifa hii kutoka kwa Wakurugenzi wa UFC akachukua hatua kadhaa ambapo moja wapo ya hatua kubwa alizo chukua ilikuwa ni kumbadilisha Balozi wa marekani nchini Guatemala na kumuweka shushushu wa CIA Bw John Peuorify Balozi huyu alipewa maagizo maalumu ya kumshinikiza Rais Arbenz alegeze misimamo yake na kama hayuko tayari kulegeza misimamo hiyo kwa kuhofia kufarakana na wananchi wake basi atoe upendeleo maalumu kwa kampuni za kimarekani.

Baada ya Balozi mpya shushushu John Peuorify Kufika Guatemala na kuweka mashinikizo haya, Rais Arbenz aliyapinga mashinikizo yote haya na akaendelea na msimamo wake wa kuweka uwiano sawa kwa makampuni yote yalimo ndani ya Guatemala na kuendelea kuhakikisha kuwa anafufua uchumi wa nchi yake.

Baada ya miezi kadhaa ya kumshawishi Rais Arbenz Alegeze msimamo kutozaa matunda yoyote ndipo hapa waziri Dulles akawasiliana na Dwight Eisenhower ambaye akikuwa Rais kwa kipindi hicho.

Baada ya changamoto hii kufikishwa mezani kwa Rais Eisenhower Alipendekeza kuwa CIA wahusishwe na wasikie wanatoa ushauri gani.
Hivyo basi moja kwa moja Waziri Dulles akiwasiliana na Mkurugenzi wa CIA na kumueleza juu ya changamoto inayowakabili.

Mkurugenzi huyo wa CIA baada ya kuelezwa kuhusu changamoto iliyopo, akapendekeza kuwa licha taarifa alizonazo kutoka kwa moja ya mashushushu wao nchini Guatemala (balozi wa marekani) lakini anahitaji kufanya uchunguzi zaidi ili aweze kutoa ushauri sahihi.

Akaongeza kuwa kutokana na uzito na unyeti wa suala hilo, inabidi atume walau moja ya wapelelezi wa CIA aliyepo ndani ya kikosi maalumu kilicho chini ya idara maalumu ndani ya shrika la CIA. Kitengo/idara hiki maalumu ndani ya CIA kilijulikana kama SAD (Special Activities Division).

Watu wanafahamu umahiri na upekee wa wa shirika la CIA lakini ndani ya CIA pia kuna na kikosi maalumu cha kipekee kwa ajili ya kazi nyeti maalumu na kazi hizo zilisimamiwa na maafisa wa Idara ya SAD ndani ya CIA. Yani kwa maneno mengine idara ya SAD ilikuwa na maafisa wa kipekee ndani ya shirika la kipekee (CIA).

Upekee wa SAD ndani ya CIA ni nini?
Kutokana kuongezeka kwa changamoto za kimataifa , ambazo nyingine zinatishia usalama au maslahi ya mrekani lakini marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana kujiepusha na lawama kutoka jamii ya kimataifa ndipo hapo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya suala hili.

Ndipo hapa ambapo serikali ya marekani ikaagiza shirika la kijasusi la CIA kuanzisha kitengo maalumu ndani yake ambacho kitakuwa na maafisa (wanajeshi) ambao wanaweza kutekeleza oparesheni yoyote ya kijeshi kwa kujitegemea pasipo kuhusisha serikali ya marekani.

CIA wakaanzisha idara maalumu ndani yake na kuuita Special Activities Division au kwa kifupi SAD ambayo idara yenyewe ilikuwa na maafisa wa siri ambao hawabebi vitambulisho na majina yao ni siri kubwa hayawezi kupatikana hata kwenye orodha ya maafisa wa CIA.

Lengo kubwa la kuanzishwa kwa idara hii ni kutekeleza oparesheni maalumu za kijeshi au proaganda na iikitokea wakakamatwa au kushitukiwa basi serikali ya marekani wanawakana kuwa si maafisa wao (Plausible deniability).

Kwahiyo kitengo hiki kilikuwa kinafanya kazi kwa niaba ya serikali ya marekani lakini kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serkali ya marekani.

Ndani ya Idara hii ya SAD kuna vitengo viwili;
Kitengo cha kwanza kinaitwa Political Action Group: kitengo hiki kazi yake kubwa ni kufanya ushawishi wa kisiasa (political influence), oparesheni za kisaikolojia (psychological operations) na vita za kiuchumi (Economic Warfares). Pia kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kitengo hiki kimeongezewa jukumu la vita za kimtandao (cyberwarfares).

Tuchukulie kwa mfano; katika nchi fulani kuna serikali au mwenendo wa serikalin uatishia maslahi ya Marekani basi kitengo hiki kinaingia kwa siri kubwa na kufanya mojawapo ya mambo ambayo nimeyaorodhesha hapo juu.

Moja ya matukio ambayo kitengo hiki kimehusika sana na CIA wamekiri kwenye nyaraka zilizowekwa wazi mwaka 2004 ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka 1953.

Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha kikomunisti cha Italia kushinda uchaguzi mwaka 1960. Pia kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya siri iliyoitwa Operation Mockingbird katika taifa la marekani. Oparesheni hii ilikuwa na lengo la 'kucontrol' habari zinazoandikwa na Vyombo vya habari nchini humo.

Oparesheni hii imekuja kupingwa vikali siku za karibuni na baraza la seneti kwa kuwa sheria hairuhusi CIA kufanya oparesheni yeyote ndani ya ardhi ya marekani.

Kitengo cha Pili kinaitwa Special Oparatins Group (SAG) na kazi yake ni kama ifuatavyo;

Kitengo hiki kinajumuisha wanajeshi wenye weledi wa hali ya juu kutekeleza malengo ya kivita pasipo kujulikana uhusika wa serikali ya marekani.

Ili kulinda utambulisho wao, wanajeshi wa kikosi hiki maalumu hawavai sare za jeshi wala kubeba vitambulisho.

Inasemekana kuwa hiki ndio kikosi maalumu cha oparesheni za kijeshi chenye usiri mkubwa nchini marekani.

Maafisa wa kitengo hiki wanapatikanaje??
Maafisa wote wanaojiunga katika kitengo hiki maalumu cha SAD wanachaguliwa kutoka katika vikosi vingine vya weledi vya jeshi la marekani mfano Army Rangers, Combat controllers, Delta Force, 24 th STS, US Army Special Forces, SEALs, Force Recon n.k.

Wakishakuchaguliwa wanapelekwa katika kituo maalumu cha mafunzo ya CIA kilichopo Virginia kinachojulikana kama Camp Peary (au maarufu kama 'The Farm') ambapo miezi 18 ya kwanza wanafundisha kuhusu intelijensia na ushushushu.

Baada ya miezi 18 hiyo wanapelekwa kwenye kituo kingine cha CIA kilichopo California ambacho kinajulikana kama 'The Point'.

Hapa wanafundishwa mafunzo ya hali ya juu ya kijeshi ambayo hayapatikani kwa kiwango hicho katika vikosi vingine vya marekani.

Mfano wanafundishwa; mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi (special hand to hand combat), kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi la marekani na nchi za kigeni, ufuatiliajj adui (tracking), Kukabiliana na hali ngumu kwenye mamzingira ya kawaida na nyikani ( extreme survival and wilderness train ing), Kumkwepa aduia, kuzuia adui na kutoroka adui (evasion, Resistance and escape - SERE) na pamoja na mafunzo hayo anaongezewa kozi maalumu ya kutambua fiziolojia ya binadamu (Udaktari).

Afisa ambaye anafuzu mafunzo haya anakabidhiwa katika idara ya SAD ndani ya CIA na anatambulika kama "Afisa Mwenye Mbinu Maalumu" (Specialized Skills Officer).

Katika oparesheni zao maafisa hawa huwa wanazitekeleza katika vikundi vya watu wachache sana wasiozidi sita na oparesheni nyingine zinatekelezwa na Afisa mmoja pekee.

Katika Ofisi za CIA kitingoji cha Langley jijini Virginia kuna ukuta wa majina ya Maafisa wa CIA waliotunikiwa tuzo za heshima kutoka na utumishi wao uliotukuka ( Distinguished Intelligance Cross na Intelligence Star). Majina ya maafisa wengi kwenye ukuta huo ni ya wale waliotumikia kitengo cha SAD ndani ya CIA.

Kwa kuzingatia kwamba makala hii inalenga kuzungumzia uhusika wa CIA katika mapinduzi ya serikali ya Guatemala. Hivyo basi tuone mifano michache sana ya oparesheni zilizotekelezwa na kitengo hiki cha SAD ndani ya CIA. Nitaeleza kwa ufupi ili tusitoke nje ya lengo kuu (mapinduzi ya Guatemala).

Ni idara hii maalumu ya CIA ambayo ilikabidhiwa raia wanne wa Tibet kutoka kwa kaka mkubwa wa kiongozi wa kiroho wa Tibet Mtukufu Dalai Lama ambapo idara ya SAD iliwapa mafunzo ya kikomando watibeti hao kisha wakawarudisha Tibet kutafuta raia wengine 300 ambao SAD iliwapa mafunzo ya kijeshi kwa siri katika kisiwa cha Saipan na mwezi oktoba SAD ikawaongoza wanajeshi hawa mpaka Tibet kuanzisha vuguvugi la kudai kujitenga na China.

Pia ni kikosi maalumu hiki cha idara ya SAD ambacho kilimtorosha kwa siri mtukufu Dalai Lama kwa kupita katikati ya majeshi ya China yaliyokuwa mpakani na kumpeleka India.

Mpaka leo haijulikani ni namna gani waliweza kufanya tukio hili.

Ni idara hii ya SAD ndani ya CIA ambayo ilihusika kuwapatia mafunzo ya kijeshi raia wa Cuba waliokuwa wanaishi uhamishoni na kuwaongoza katika jaribio la kumpindua Fidel Castro. Mapigano haya yakihistoria yalidumu kwa siku tatu na yanajulikana kwa jina maarufu la 'Bay Of Pigs Invasion'.

Jaribio hili la mapinduzi halikuwezekana na ndilo lililochangia kudorara kwa mahusiano kati ya Marekani na Cuba mpaka leo hii.

Kwa mujibu wa nyaraka za siri za CIA zikizowekwa wazi mwaka 2004. Amri ya kumpiga risasi Che Guevara katikakati mwa miaka ya 1960 ilitoka kwa makomado wa SAD.

Ilikuwaje; Jeshi la msituni lililojiita Jeshi la Ukombozi la Bolivia (National Liberation Army of Bolivia) lilianzisha vita dhidi ya serikali ya Bolivia ambayo ilikuwa inaungwa mkono na Marekani. Jeshi hili likuwa na vifaa vya kisasa na liliungwa mkono na mwanamapinduzi Che Guevara.

Katika za mwanzo za mapigano jeshi hili la waasi lilionekana kushinda dhidi ya majeshi ya serikali.

Ndipo hapo CIA wakatuma makomando wa kitengo cha SAD ambao walienda kutoa mafunzo kwa majeshi ya Bolivia katika milima Camiri. Na baada ya hapo wakawaongoza kupigana na waasi na kufanikiwa kuwashinda. Kisha makomando wa SAD wakawaongoza makomando wa jeshi la Bolivia (Bolivia Special Forces) kumkamata Che Guevara ambapo Mara tu baada ya kukamatwa komando wa SAD aliyeitwa Felix Rodriguez akaamuru auwawe.

Hii ni mifano michache kati ya mifano mingi amabayo CIA kwa kutumia kitengo cha SAD wameendesha opesheni maalumu za kijeshi katika nchi nyingi.

Ingawa Rais wa marekani ndiye anayetoa amri ya kufanyika kwa operesheni hizi za kuvamia kijeshi nchi nyingine au kuongoza mapinduzi ya serikali halali duniani kote lakini analindwa na sheria ya Marekani ambayo inampa Rais uwezo wa kukana uhusika wa Rais wa marekani kutoa amri au kufahamu kinachofanywa na kitengo hiki. (Plausible Deniability).

Sheria hii ilitingwa mwaka 1947 inajulikana kama National Security Act. Pia Sheria hii ilitiliwa mkazo na tamko la rais namba 12333 (Executive Order 12333) lenye kichwa cha habari National Intelligence Activities.

Naamini tumeelewa vya kutosha kitengo maalumu cha CIA cha Special Activities Division (SAD) namna kinavyofanya kazi.
TUREJEE KATIKA MAPINDUZI YA GUATEMALA NA UHUSIKA WA CIA.

Taarifa iliyorudishwa na shushu wa CIA mwanamaa Virginia Hall ziliendana kabisa taarifa za shushushu John Peurofy aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Guatemala.

Kwamba Sera za Rais Arbenz zilikuwa zinatishia uhai wa makampuni ya kimarekani nchini Guatemala na mbaya zaidi Rais Arbenz alikuwa hataki kulegeza msimamo.

Hivyo basi mwaka 1952 dikteta wa Nicaragua aliyeitwa Anastosio Somoza Garcia alifanya ziara ya kiserikali nchini marekani.

Katika kikao chake Ikulu ya marekani na Rais Dwight Eisenhower akamueleza kuwa kama atapatiwa silaha za kutosha ana uwezo wa kumuondoa madarakani Rais Arbenz wa Guatemala.

Wazo hili lilimpendeza Rais Eisenhower na akaagiza CIA washirikiane na serikali ya Nicaragua kuandaa mpango wa kumuondoa madarakank Rais Arbenz wa Guatemala

OPERATION PBFORTUNE
Baada ya CIA kupewa agizo hilo na Rais wakatengeneza mpango maalumu waliouita Operation PFFORTUNE. lengo kuu la mpango huu ulikuwa ni kuipindua serikali ya Guatemala kwa kutumia jeshi la Nicaragua.

Pia CIA wakawasiliana na Manuel Rejemez dikteta wa Venezuela wa kipindi hicho aliyeungwa mkono na marekani pia wakawasiliana na Rafael Trujillo dikteta wa Dominican Republic ambaye pia aliungwa mkono mpango Marekani na wote wakakubalina na mpango huo wakiahidi kutoa fedha na mafunzo kwa wanajeshi wa Nicaragua.

Baada ya mpango kuonekana umekamilika CIA walitumia meli ya kampuni ya UFC (United Fruit Company) kubeba silaha nzito za kijeshi kuelekea nchini Nicaragua ambapo walidanganya kwa kuwajulisha mamlaka za bandari kuwa mzigo huo ulikuwa ni vifaa vya kilimo vya kampuni ya UFC.

Meli ikaanza safari na kukaribia kabisa Nicaragua lakini zikaja taarifa za kusikitisha mno.

Rais wa Nicaragua Dikteta Anastasio Somoza alikuwa ni mtu wa majivuno mno. Na majivuno take yalisababisha kwenye kikao kimoja cha baraza lake la Mawaziri akajivuna kuwa yeye ni kiongozi makini mpaka imefikia hatua serikali ya Marekani kumuamini na kumuomba aongoze mapinduzi ya kumtoa madarakani Raid Arbenz wa Guatemala.

Baada ya taarifa hii ya siri kuropokwa mbele ya mawaziri, ilivuja mpaka kumfikia mwenyewe Rais wa Guatemala.

Arbenz akaitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo alitoa hotuba kali kuilaani Marekani kwa mpango huu na jamii ya kimataifa iliposikia habari hii iliilaani vikali marekani.

Hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kuamuru Meli iliyobeba silaha igeuze na kurejea Marekani.

Operation PBFORTUNE ikafia hapa kwa aibu kubwa.

OPERATION PBSUCCESS
Baada ya oparezheni ya kwanza kushindwa, CIA ikaomba idara yake maalumu ya SAD kutengeneza mpango maalumu wa kumuondoa madarakani Rais Arbenz.

SAD wakaja na mpango waliouita 'Operation PBSUCCESS' ambapo katika mpango huo walianisha kuwa ni lazima njia zote mbili zitumike ili kumuondoa madarakani Rais Arbenz.

Yaani ni lazima itumike prooaganda, ambapo watatumia kitengo chao kidogo cha Special Action group (kwa ajili ya propaganda na vita ya kisaikolojia) pia kitengo chake kidogo cha Special Activities group kitatumika kwa ajili ya shambulio la kijeshi.

Kwanza kabisa wakafungua ofisi ndogo maeneo ya Opa-locka Florida ambapo ndiyo yalikwa kama makao makuu ya Operation PBSUCCESS.

Propaganda:
kitengo maalumu cha SAG wakaanzisha kituo cha redio kilichoitwa "Voice Of Liberation" ambacho kilirusha matangazo nchini Guatemala kikidai kuwa kinamilikiwa na wanajeshi waasi walioko msituni ma dhima yao ilikuwa ni kumuondoa Rais Arbenz.

Ili kuleta ufanisi zaidi CIA wakatumia makomando wao kuharibu antena za redio ya Umma ya serikali hivyo kukifanya redio yao ya VOL kusikika pekee nchini Guatemala.

Pia walitimia muda wote kutangaza ni namna gani Arbenz anahiharibu nchi ya Guatemala.

Taratibu sumu ikapandikizwa kwenye vichwa vya wananchi wa Guatemala.

Pia CIA walitumia ndege kudondosha vipeperushi mara kadhaa kwa wiki wakimtaka Rais Arbenz ajiuzuru. Sumu ikaendelea kupandikizwa.

Pia likaja kongamano la nchi za Bara America (Organisation Of American States) Marekani wakashinikizwa iongezwe Agenda ya "Kupinga Ukomunist Kwenye Bara Amerika".

Kitendo cha hiyo Agenda kujadiliwa tu sumu ikazidi kuenea kuwageuza miyo ya watu dhidi ya Rais Arbenz.
Oparasheni za kijeshi;

makomando wa SAD wakawasiliana na Generali Muasi Castillo Armas aliyeishi uhamishoni nchini Nicaragua wakimuomba wamtumie baada ya miaka ya nyuma kujaribu kufanya mapinduzi bila mafanikio.

Walichomuahidi ni kwamba akikubali kushirikiana nao basi watamfanya kuwa Rais baada ya mapinduzi. Na akaelezwa akusanye wananchi wengine wa Guatemala wanaoishi uhamishoni na kuunda jeshi wao watampatia silaha na fedha ya kuwalipa wanajeshi wake.

Generali Armas akakusanya wanajeshi 300 na CIA wakampatia dola 225,000 kwa ajili ya kujikimu yeye na jeshi lake.

Kisha wakafundisha wanajeshi kadhaa wa wa Generali Armas uruabani wa kijeshi na kazi yao ilikuwa moja tu. Kwa kutumia ndege za kivita walizopewa na CIA walikuwa wanavizia na kulipua miundombinu kadhaa nchini Guatemala kama vile madaraja na maghala ya silaha.

Uharibifu haukuwa mkubwa sana lakini ulitosha kuchochea hofu ambayo tayari ilikuwa imepandikizwa kwa wananchi wa Guatemala.

Kisha redio VOL ikatangaza kuwa muda wa mapinduzi umewadia na ndani ya wiki hiyo Rais Arbenz anang'olewa madarakani na wazalendo wa Guatemala walioko mpakani.

Rais Arbenz akaulizia taarifa za intelijinsia na akaambiwa kuwa ni kweli kuna wanajeshi wanaonekana mpakani mwa Guatemala na Nicaragua.

Rais Arbenz pasipo kujua, akaingia mtegoni akaamuru jeshi lote lielekee mpakani kusambaratisha waasi.

Walipofika mpkani walishangaa kukuta wanajeshi 180 pekee wa Generali Armas ambao waliwasambaratisha kwa masaa machache huku wanajeshi 30 pekee walisalia na kurudi upande wa pili wa mpaka nchini Nicaragua alipo Generali Armas.

Rais Arbenz akachanganyikiwa asijue maana ya fumbo hilo. Akijiingiza zaidi kwenye mtego. Akaamuru majeshi yasitoke mpakani kwani anaamini wanajeshi hawa ni chambo tu lakini lazima kuna wengine watakuja.

Hiki ndicho walichokitaka marekani. Kesho yake Radio ya VOL ikatangaza kuwa kwa kuwa majeshi ya serikali yanatumia nguvu kubwa kuua wazalendo hivyo basi marekani inaungana na waasi hao kwa kutuma jeshi lake kufanya uvamizi na kumuondoa Rais Arbenz.

Jioni ya siku hiyo marekani wakatoa tamko kali kuipinga serikali ya Rais Arbenz pasipo kuthibitisha wala kukataa kama wanaungana kijeshi na waasi.

Hii ilitosha kupasua mioyo ya wananchi na wanajeshi wa Guatemala. Wote walifahamu kama marekani anaingia vita hiyo hakuna uwezekano wowote wa majeshi ya Guatemala kushinda vita.

Wanajeshi wa serikali wakawasiliana na Generali Armas kuwa kama watakubali 'kusarenda' ni hatua gani atachukua dhidi yao??
Generali Armas akawajibu kuwa kwa maslahi mapana ya Taifa atawasamehe na kuwarudisha kazini.

Kesho yake majeshi ya serikali yaliyojo mpakani yakatangaza kuwa hawako tayari kupigana kwa niaba ya Rais Arbernz na wanamtaka ajiuzulu kwa maslahi ya taifa.

Rais Arbenz akachanganyikiwa zaidi akaitisha kikao na viongozi wa vyama vya wakulima na wafanyakazi akiwaomba wawashawishi wanachama wao wapewe silaha na kupigana kuitetea nchi yao.

Viongozi wa vyama wakakubali wakatoa matangazo nchi nzima wananchi wajitokeze kushika silaha kutetea nchi yao na wanatakiwa kesho yake wote wafike katikati ya mji kukabidhiwa silaha.

Jambo la aibu ni kwamba wananchi 120 pekee ndio walijitokeza huku wengine wote wakianzisha maandamano kumtaka Rais Arbenz ajiuzulu kwa maslahi ya Taifa.

Taarifa hii ikamfikia Generali Armaz na CIA. Generali Armas akampa amri ya mwisho Rais Arbenz kuwa ajiuzulu kwa hiari ndani ya Massa 24 na atahakikisha anamuacha aondoke kwa amani ndani ya Guatemela na kwenda kuishi uhamishoni.

Kama hataki kujiuzulu kwa hiari atatumia jeshi ambalo sasa liko chini yake kumuoindua na kumfunga gerezani.

Rais hakuwa na chaguo, jioni ya siku hiyo tarehe 27 June 1954 kwa uchungu, Rais Jacobo Arbenz aliutangazia umma kuwa anajiuzulu.
Na Generali kama alivyomuahidi akamruhusu aondoke kwa amani kwenda kuishi uhamishoni.

Kesho yake Generali Castillo Armas akawa Rais mpya wa Guatemala.

Na huu ndio ukawa mwanzo wa nchi hii kutawaliwa na viongozi wa kijeshi wanaoungwa mkono na Marekani.
 
Gmox

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
309
468
mbona mnatumia nguvu kubwa sana kuupotosha umma juu ya mtu wanaye mtumaini ??? Kwanini msitumiye nguvu hiyo hiyo kumnadi mgombea wenu...je mnamdanganya nani kiasi hiki tena kwa kumchafua mtu😕
 
ligend

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
617
1,792
Kwa Wakati tuliopo ni mtu mmoja tu ndiye anayeweza kumshinda TUNDU ANTHIPAS LISSU na si mwingine ni TUNDU ANTHIPAS LISSU mwenyewe.
 
MLO

Senior Member
Apr 2, 2012
194
79
mbona mnatumia nguvu kubwa sana kuupotosha umma juu ya mtu wanaye mtumaini ??? Kwanini msitumiye nguvu hiyo hiyo kumnadi mgombea wenu...je mnamdanganya nani kiasi hiki tena kwa kumchafua mtu😕
Kondoo pekee ndiye anaweza kukataa na kutotambua kutumika kwa Lisu
 
cmoney

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
3,525
5,262
Connection?
Yule mzungu wenu https://twitter.coma/robertamsterdam mnaopenda mpostia kila tukio linalotokea Tanzania yupo kimaslahi tu na hata hao wamarekani wenyewe wanamjua ni mchuma tumbo
Rick Scott sends letter shaming D.C. firm for representing Nicolás Maduro government

U.S. Sen. Rick Scott is again urging a D.C. firm to cease its representation of the Nicolás Maduro government.

Scott berated Amsterdam & Partners LLP late last week for taking on the controversial contract in which the firm will push back against U.S. sanctions on Maduro. Now, Scott is following up with a letter directly to the firm.

“This is shocking news considering the absolute genocide Maduro is perpetrating on his citizens. He is a thug and a dictator who is murdering children and starving his people,” Scott said, before recounting his visits to the Venezuela border.

“I’ve seen the starvation, the hunger, the pain. Children are starving to death — children the age of my grandsons. These same children were walking for hours each way to go to school in Cúcuta just across the border. Mothers and their young children trudged through dense forests and across rivers to get their only meal of the day. Men, women, and children are dying, and it’s all at the hands of Nicolas Maduro — the socialist dictator whose government you have agreed to represent.”

Scott added, “No business in the United States should have any contact with Maduro’s government, let alone willingly take money to lobby on its behalf.”
 
MLO

Senior Member
Apr 2, 2012
194
79
je hiyo ndiyo sera ya mgombea wenu kumzushia uwongo mshindani wake😡😡
uvivu wenu wa kusoma na tamaa ya madaraka bila kujua walionyuma ya lisu mtayajua haya 2070 CIA wakiyaweka hadharani. Matamshi ya Lisu yathibitisha ktumiwa na CIA angalia report hizi za 2970's dhidi ya zanzibar na Sera za uchumi za Mgufuli na Nyerere
 
Attachments

 • IMG_20200920_153614.png
  IMG_20200920_153614.png
  85.2 KB · Views: 8
 • IMG_20200920_112351.png
  IMG_20200920_112351.png
  42.3 KB · Views: 8
 • IMG_20200920_112405.png
  IMG_20200920_112405.png
  66.1 KB · Views: 7
 • IMG_20200920_112437.png
  IMG_20200920_112437.png
  46.1 KB · Views: 8

Morgan Fisherman

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
1,563
1,551
mataga bhn
uvivu wenu wa kusoma na tamaa ya madaraka bila kujua walionyuma ya lisu mtayajua haya 2070 CIA wakiyaweka hadharani. Matamshi ya Lisu yathibitisha ktumiwa na CIA angalia report hizi za 2970's dhidi ya zanzibar na Sera za uchumi za Mgufuli na Nyerere
 
Nyabutoro

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
1,202
1,401
Kuna kitu kinaweza kutuvusha na mipango ya uovu kama hii dhidi yetu.Tufanye yafuatayo:
1.Uhuru wa kutoa Mawazo
Shida kubea ya Wajamaa ni kuzuia Mawazo ya wengine na kuwakandamiza na wakati mwinhine kuwauwa.

2.Kujenga umoja wa kitaifa.
Unapotuhusu watu kusema unajenga mijadala ya kitaifa na umoja, ukizuia huwezi kujua chochote, kila mtu anabki kimya kwa kuogopa kuwajibishwa.

3.Kujenga taasisi badala ya watu.

Hapa inaonekana rais alikuwa anapenda kusifiwa yeye tu, na alitamani kuua taasisis na yeye na watu wachache kuwa maarufu kuliko mifumo yao

4.Kutolipa visasi.

Kwenye mada hii hukusema, lakini inawezekana huyu bwana alilipa visasi kwa waliokosea, na wao wakamfix.

NAWASILISHA
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom