Hivi ndivyo marehemu Nicola mmiliki wa Slipway na Coastal Aviation alivyoagwa na wafanyakazi wake

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg

Hivi ndivyo mmiliki wa Slipway Hotel na kampuni zake nyingine ikiwemo kampuni ya ndege ya Coastal Aviation ndugu Nicola Colangelo alivyoagwa na wafanyakazi wake.

Toka Hotel ya Slipway mpaka viunga vya Ras Kutani-Kigamboni,Camps za Watalii katika pori la Selous na Hotel zake kule visiwa vya Mafia ilikuwa ni majonzi matupu.

Mtoni Marine Zanzibar mpaka CSI na maeneo yote alipokuwa amewekeza,ilikuwa ni vilio na kwikwi za huzuni.Wafanyakazi wake wote katika maeneo yote aliyowekeza,walitenga muda wa kukaa kimya na kufuatilia habari za mazishi yake huko kwao Italia.

Ilikuwa ni siku ya huzuni,katika picha wapo wazee walioanza kufanya kazi na Nicola akiwa hana utajili mkubwa.Hakuwahi kuwaacha eti kwa sababu amejenga hoteli kubwa ya kitalii na wao hawakuwa na elimu kubwa ya kuhudumia utalii,Nicola alienda nao,na leo ametangulia mbele za haki na wao wamebaki.

Kuna wapishi wake walioanza kumpikia chakula binafsi toka miaka ya 1970's wakiwa mabinti wadogo,mpaka leo ni wabibi lakini alikuwa nao pamoja.

Picha hizi ni muunganiko wa matukio,katika hotel ya Slipway,Uwanja wa ndege wa JNIA eneo la Terminal One zilipo ndege zake,Mafia na Selous.

Hivi ndivyo,Nicola alivyoagwa,mtu wa watu na mlowezi aliyewekeza kwa wazawa kwa moyo mmoja.

Pumzika kwa Amani Nicola.

image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    64.3 KB · Views: 116
Apumzike tuuu, sio kwa amani. Hawa ndio waliochangia kuangusha biashara ya utalii na umiriki wa Ndege za kwenda mbugani kwa serikali
NAONA Electronic Fiscal Device (EFD) za TRA zikiendelea kutafuta figisu figisu
Duuh
 
Apumzike tuuu, sio kwa amani. Hawa ndio waliochangia kuangusha biashara ya utalii na umiriki wa Ndege za kwenda mbugani kwa serikali
NAONA Electronic Fiscal Device (EFD) za TRA zikiendelea kutafuta figisu figisu
Usipotoshe mkuu
Serikali haiwezi biashara ya ndege kwenda porini,hii ni rahisi kwa sekta binafsi...muhimu ni serikali kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji.

Au uliwahi kusikia ATCL wana ndege za kwenda porini miaka ya nyuma?
 
Apumzike tuuu, sio kwa amani. Hawa ndio waliochangia kuangusha biashara ya utalii na umiriki wa Ndege za kwenda mbugani kwa serikali
NAONA Electronic Fiscal Device (EFD) za TRA zikiendelea kutafuta figisu figisu

Taifa sasa linalishwa ujinga na kuaminishwa kuwa kila aliyetajiri basi alituibia ili awe tajiri!

Hizi ni tabia za jamii maskini.
 
Samahani hao wanaomlilia wanalia kwa kuondokewa nae ' Kipenzi ' chao Nicola au wanalia baada ya kujua kwamba labda sasa maisha yao yataenda kubadilika na kuwa magumu kwani kikawaida tu Binadamu tunatofautiana sana kwa roho za Utu, Hekima, Busara na Huruma. Labda wameshamjua ' Bosi ' ajaye alivyo ' mnoko ' hivyo wanamlilia ' Nicola ' na kusikitika kwanini Mungu amemchukua haraka.
 
Back
Top Bottom