Hivi ndivyo Makonda, Ikulu walivyomponza Askofu Malasusa kwa kumshawishi kuukana waraka na kuendeshwa kwa gari ya Ikulu

kiben10

JF-Expert Member
Apr 28, 2018
616
789
Na Mwandishi Wetu

NGUVU iliyosababisha usaliti wa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), ambaye ametengwa na Baraza la Kuu la maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imejulikana.

Kanisa lilifanya uamuzi wa kumtenga katika kikao cha maaskofu kilichomalizika Jumanne tarehe 24 Aprili 2018 mjini Arusha, Tanzania. Kwa kutengwa kwake huku, Askofu Malasusa ameondolewa katika kamati zote za maaskofu wa KKKT, na hawezi kushiriki vikao vya maaskofu. Anabaki kuwa “mtu wa Dar es Salaam tu.”

SAUTI KUBWA ina taarifa za uhakika kuwa mbali na udhaifu wa dhamiri yake mwenyewe, waliomponza Askofu Malasusani pamoja na Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (ambaye jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite), na maofisa kadhaa wa Ikulu waliokuwa wanahaha kutengeneza mgawanyiko katika kanisa, ili waraka wa maaskofu uonekane si wa kanisa zima, na ukose mvuto kwa umma.

KKKT liliandika waraka maalumu wa maaskofu uliobeba ujumbe wa Pasaka kwa waamini na Watanzania wote mwaka huu, ukiwataka kuzingatia amani, na kuitaka serikali iwajibike kulinda amani ya raia wanaotekwa, wanaoteswa, na wanaouawa na “watu wasiojulikana,” ambao serikali imegoma kuwachukulia hatua.

Kwa nguvu ya Makonda na maafisa hao, Askofu Malasusa alipuuza makubaliano ya kanisa yaliyotaka kila askofu asambaze waraka huo na kuusoma katika makanisa yaliyopo kwenye dayosisi yake siku ya Jumapili ya Matawi (Mitende).

Kilichotokea kati ya Ikulu, Bashite na Askofu Malasusa

Tarehe 24 Machi 2018, Jumamosi, (ambayo waraka ulitoka ili usomwe makanisani kesho yake Jumapili ya Mitende), Askofu Malasusa alikuwa na kikao kirefu na Bashite na maafisa wawili kutoka Ikulu.

Kikao kilifanyikia ofisini kwake. Baada ya kikao hicho, ambacho kiliisha usiku, maafisa wa Ikulu walifuata wahariri wa gazeti la UPENDO – linalomilikiwa na KKKT – na kuwataka waondoe habari iliyohusu waraka wa maaskofu, na waraka wenyewe ambao ulikuwa umechapishwa ndani ya gazeti.

Wahariri hawakukubaliana nao, bali walieleza maofisa wa Ikulu kuwa gazeti lilikuwa limeshapelekwa kiwandani, hivyo hawakuwa na njia nyingine ya kuondoa habari au waraka huo.

Wahariri walijitetea wakisema kwamba hata kama wangefanikiwa kuondoa habari hiyo na waraka, bado ingeweza kutoka kwenye magazeti mengine, na wao wangeonekana ni wasaliti.

Maafisa wa Ikulu walisema bora habari iandikwe na magazeti mengine, lakini gazeti la kanisa lisiwe nayo. Baada ya ubishi huo, maofisa hao walielekea kiwandani. Wanajua walivyofanya, wakachomoa habari hiyo na waraka wa maaskofu uliokuwa umewekwa gazetini.

Hatua hiyo ilihakikishia Ikulu kwamba kwa kuwa gazeti la kanisa halikutaja waraka huo, basi hata nguvu na athari ya waraka huo ingepungua.

Usaliti wa Askofu Malasusa ulileta taharuki katika kanisa hilo na kwenye jamii, huku serikali ikijitahidi kupotosha umma kwamba “waraka ule si wa kanisa bali ni maoni ya maaskofu wachache.”

Wachambuzi wa masuala ya dini wanasema kuwa kitendo cha Askofu Malasusa kutii mamlaka ya mkuu wa mkoa na kuzuia salaam za maaskofu, ni ukiukaji wa kiapo cha uaskofu wake kwa sababu “amemtii mwanadamu kuliko Mungu,” na kwamba alijisafisha mbele ya Kaisari badala ya kujiweka mbele ya Mungu.

Siku ya uwekaji jiwe la msingi la uwanja wa ndege (Terminal Three) Dar es Salaam, Askofu Malasusa aliingia uwanjani hapo kwa gari la Ikulu lenye kimulimuli akitokea Mabibo alikokuwa amekwenda kufungua mkutano wa akina mama wa KKKT.

Ikulu ilimtumia gari limuwahishe kwenye tukio kwa sababu ya kuhofia kuwa msongamano wa magari barabarani ungeweza kumsababisha achelewe. Katika tukio hilo, mbele ya Askofu Malasusa na viongozi wengine wa dini, Rais John Magufuli aliwataka “maaskofu waombee viwanda badala ya kuandika nyaraka.”

Kwa uamuzi wa KKKT kumtenga Askofu Malasusa, kanisa limejenga heshima na kuhakikishia waamini na wananchi kuwa lipo imara, lina kauli moja isiyotetereka, na kwamba ujumbe wa waraka wa maaskofu ni upo pale pale kama kauli ya kitume na kinabii ya kanisa.

SAUTI KUBWA haikufanikiwa kujua “kifungo” cha Askofu Malasusakinamalizika lini, lakini msaidizi wake ndiye anatarajiwa kuwa msimamizi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Hata hivyo, baadhi ya wachungaji wa DMP wanasema kuna tetesi kuwa Askofu Malasusa anatafakari jinsi ya “kuondoa dayosisi yake katika KKKT.” Baadhi yao wanasema iwapo atafanya hivyo atakuwa amejitangaza rasmi kuwa “askofu wa serikali” badala ya kuwa askofu wa kanisa.
 
Nasikitika Baba Askofu wangu anaangukiwa na Jumba bovu. Kweli nilijiuliza sana kwa nini waraka haukusomwa usharikani kwetu? Nilipodadisi, nikaambiwa katika Dayosisi yetu "Waraka" hakusomwa popote na wala hautasomwa.

Na kwa kauli ya AB kuwa Mkoa wetu uko shuwari na hakuna cha waraka, nikajua tu kuwa kuna jambo, na jambo lenyewe limejitokeza.

Collective responsibility matters!
 
Hivi ndivyo Bashite, Ikulu walivyomponza Askofu Malasusa
Ansbert Ngurumo28th April 2018

Na Mwandishi Wetu

NGUVU iliyosababisha usaliti wa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), ambaye ametengwa na Baraza la Kuu la maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imejulikana.

Kanisa lilifanya uamuzi wa kumtenga katika kikao cha maaskofu kilichomalizika Jumanne tarehe 24 Aprili 2018 mjini Arusha, Tanzania. Kwa kutengwa kwake huku, Askofu Malasusa ameondolewa katika kamati zote za maaskofu wa KKKT, na hawezi kushiriki vikao vya maaskofu. Anabaki kuwa “mtu wa Dar es Salaam tu.”

SAUTI KUBWA ina taarifa za uhakika kuwa mbali na udhaifu wa dhamiri yake mwenyewe, waliomponza Askofu Malasusa ni pamoja na Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (ambaye jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite), na maofisa kadhaa wa Ikulu waliokuwa wanahaha kutengeneza mgawanyiko katika kanisa, ili waraka wa maaskofu uonekane si wa kanisa zima, na ukose mvuto kwa umma.

KKKT liliandika waraka maalumu wa maaskofu uliobeba ujumbe wa Pasaka kwa waamini na Watanzania wote mwaka huu, ukiwataka kuzingatia amani, na kuitaka serikali iwajibike kulinda amani ya raia wanaotekwa, wanaoteswa, na wanaouawa na “watu wasiojulikana,” ambao serikali imegoma kuwachukulia hatua.

Kwa nguvu ya Makonda na maafisa hao, Askofu Malasusa alipuuza makubaliano ya kanisa yaliyotaka kila askofu asambaze waraka huo na kuusoma katika makanisa yaliyopo kwenye dayosisi yake siku ya Jumapili ya Matawi (Mitende).

Kilichotokea kati ya Ikulu, Bashite na Askofu Malasusa

Tarehe 24 Machi 2018, Jumamosi, (ambayo waraka ulitoka ili usomwe makanisani kesho yake Jumapili ya Mitende), Askofu Malasusa alikuwa na kikao kirefu na Bashite na maafisa wawili kutoka Ikulu.

Kikao kilifanyikia ofisini kwake. Baada ya kikao hicho, ambacho kiliisha usiku, maafisa wa Ikulu walifuata wahariri wa gazeti la UPENDO – linalomilikiwa na KKKT – na kuwataka waondoe habari iliyohusu waraka wa maaskofu, na waraka wenyewe ambao ulikuwa umechapishwa ndani ya gazeti.

Wahariri hawakukubaliana nao, bali walieleza maofisa wa Ikulu kuwa gazeti lilikuwa limeshapelekwa kiwandani, hivyo hawakuwa na njia nyingine ya kuondoa habari au waraka huo.

Wahariri walijitetea wakisema kwamba hata kama wangefanikiwa kuondoa habari hiyo na waraka, bado ingeweza kutoka kwenye magazeti mengine, na wao wangeonekana ni wasaliti.

Maafisa wa Ikulu walisema bora habari iandikwe na magazeti mengine, lakini gazeti la kanisa lisiwe nayo. Baada ya ubishi huo, maofisa hao walielekea kiwandani. Wanajua walivyofanya, wakachomoa habari hiyo na waraka wa maaskofu uliokuwa umewekwa gazetini.

Hatua hiyo ilihakikishia Ikulu kwamba kwa kuwa gazeti la kanisa halikutaja waraka huo, basi hata nguvu na athari ya waraka huo ingepungua.

Usaliti wa Askofu Malasusa ulileta taharuki katika kanisa hilo na kwenye jamii, huku serikali ikijitahidi kupotosha umma kwamba “waraka ule si wa kanisa bali ni maoni ya maaskofu wachache.”

Wachambuzi wa masuala ya dini wanasema kuwa kitendo cha Askofu Malasusa kutii mamlaka ya mkuu wa mkoa na kuzuia salaam za maaskofu, ni ukiukaji wa kiapo cha uaskofu wake kwa sababu “amemtii mwanadamu kuliko Mungu,” na kwamba alijisafisha mbele ya Kaisari badala ya kujiweka mbele ya Mungu.

Siku ya uwekaji jiwe la msingi la uwanja wa ndege (Terminal Three) Dar es Salaam, Askofu Malasusa aliingia uwanjani hapo kwa gari la Ikulu lenye kimulimuli akitokea Mabibo alikokuwa amekwenda kufungua mkutano wa akina mama wa KKKT.

Ikulu ilimtumia gari limuwahishe kwenye tukio kwa sababu ya kuhofia kuwa msongamano wa magari barabarani ungeweza kumsababisha achelewe. Katika tukio hilo, mbele ya Askofu Malasusa na viongozi wengine wa dini, Rais John Magufuli aliwataka “maaskofu waombee viwanda badala ya kuandika nyaraka.”

Kwa uamuzi wa KKKT kumtenga Askofu Malasusa, kanisa limejenga heshima na kuhakikishia waamini na wananchi kuwa lipo imara, lina kauli moja isiyotetereka, na kwamba ujumbe wa waraka wa maaskofu ni upo pale pale kama kauli ya kitume na kinabii ya kanisa.

SAUTI KUBWA haikufanikiwa kujua “kifungo” cha Askofu Malasusa kinamalizika lini, lakini msaidizi wake ndiye anatarajiwa kuwa msimamizi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Hata hivyo, baadhi ya wachungaji wa DMP wanasema kuna tetesi kuwa Askofu Malasusa anatafakari jinsi ya “kuondoa dayosisi yake katika KKKT.” Baadhi yao wanasema iwapo atafanya hivyo atakuwa amejitangaza rasmi kuwa “askofu wa serikali” badala ya kuwa askofu wa kanisa.

Home - Sauti Kubwa
 
Ngurumo, ushafeli kwenye mambo mengi sana na umekuwa desperate na hauna dira ya maisha yako, na unakuwa mkimbizi mpaka vijukuu vyako

nakupa ushauri tu, ukitaka SAUTI KUBWA iwe ncha kali,

1.address watu kwa heshima zao na title zao
2.ondoa chuki binafsi na kutaka gazeti lako liwe linakubalika upande mmoja
3.epuka lugha za kuudhi na mipasho
4. weka evidences

ukiniambia mkuu wa mkoa wa DSM Paul makonda(ambaye jina lake halisi ni....Bashite) hapa unataka ku achieve nini? lengo la hii sentensi ni nini? mshabiki wa makonda anaishia hapa

Mange aliambiwa sana akabisha, akajiona mjanja ana haha kila kona

You have such talent, skills na chances za kutengeneza mwanzo wako mpya...certainly sio kwa style hii...

ukibisha, see you 10yrs from now, inshaallah
 
Ahsanteni maasikofu kwa kuimalisha kanisa, iliniuma sana tulivokeleliwa na Bashite eti "hakuna waraka uliosomwa kwenye mkoa wangu sina masihara"Hapo nilijua tu kakaangu Askofu Malasusa kateleza amepigwa mkwara na Bashite akaogopa, Uamuzi na msimamo wa maasikofu naukubari na napongeza umeurudishia heshima kanisa Na ushauri wangu wa bure kwa Malasusa asijidanganye kwa lolote zaidi ya kujitafakali nakuliomba radhi kanisa
 
Iringa pia haukusomwa huko yupo makonda pia ?
 
Ngurumo, ushafeli kwenye mambo mengi sana na umekuwa desperate na hauna dira ya maisha yako, na unakuwa mkimbizi mpaka vijukuu vyako

nakupa ushauri tu, ukitaka SAUTI KUBWA iwe ncha kali,

1.address watu kwa heshima zao na title zao
2.ondoa chuki binafsi na kutaka gazeti lako liwe linakubalika upande mmoja
3.epuka lugha za kuudhi na mipasho
4. weka evidences

ukiniambia mkuu wa mkoa wa DSM Paul makonda(ambaye jina lake halisi ni....Bashite) hapa unataka ku achieve nini? lengo la hii sentensi ni nini? mshabiki wa makonda anaishia hapa

Mange aliambiwa sana akabisha, akajiona mjanja ana haha kila kona

You have such talent, skills na chances za kutengeneza mwanzo wako mpya...certainly sio kwa style hii...

ukibisha, see you 10yrs from now, inshaallah
Yaani hilo jarida litasomwa na wanaufipa tu. Sasa sijui lina utashi gani kwa wananchi kwa ujumla. Hata hiyo miaka kumi uliyompa huyu kibwengo ni mingi sana.
 
Back
Top Bottom