Hivi ndivyo gari huwa zinawaka moto

Hii ni Audi A3 2.0 TSI Hatchback ya mwaka 2010. Nimeifanyia Diagnosis kama kawaida ina error codes kibao (Zaidi ya Faults 50).

Sasa katika kwenda kutest waya za mojawapo ya sensor ambayo ilionesha ina shoti, Pembeni kidogo ya battery si nikakuta moshi unafuka. Halafu lile eneo la fusi box nikakuta ni la moto balaa.

Anyway nmefungua mfuniko wa fuse box ndio nakutana na kitu hiki hapa chini.

View attachment 1929415

Ikabidi nizime gari then nifanye mpango wa kuchomoa hivyo vibati vilivyobakia hapo maana lile plastic lote la fuse limeshayeyuka na limeanza na kuyeyusha sehemu ya fuse box.

Nikakutana na kitu hiki

View attachment 1929416

Aiseee ukitazama vizuri hicho kibati kina nyaya nyaya ambazo zimewekwa na mafundi.

Kama kawaida mtu aliona fuse imeungua akaamua kunjunga na mayokeo yake waya umepata current kubwa then moto umeanza. Gari nyingi fuse zake zimezungushwa waya kama ilivyofanywa hii.

Other pictures

View attachment 1929419

View attachment 1929420

View attachment 1929422

View attachment 1929426


Kama kawaida naendelea kusisitiza. Gari za ulaya siyo za kununua kama unanunua nyanya.

Rejea

Thread 'Gari za Ulaya/Marekani hazitaki ubabaishaji kabisa' Gari za Ulaya/Marekani hazitaki ubabaishaji kabisa

Sasa hebu angalia faults za hii ya leo.

View attachment 1929434

View attachment 1929435

View attachment 1929437

View attachment 1929438

Pia hizi siyo gari za kuendesha tu ilimradi unaona inatembea. Check up inamatter sana. Otherwise siku ukija kupima ndio utatajiwa matatizo mpaka kichwa kikuume.



Kama una tatizo na gari yako au unahitaji Diagnosis nicheck.

Iwe gari yoyote ndogo ya Ulaya, Asia au Marekani tunapima na kusolve.

Nipo Dar.

0621 221 606.
Somebody about to fire his car huku manzee RRONDO mshauri mwanetu Holy Man awe makini na hii mambo ya Diagnosis
 
Hahahahah nimeinyaka hii, tusiige tembo tutapasuka! Jana kuna kijana alikuwa na 2.0T Quattro nacheza nae mandela road nikakuwaza sana mzee kumbe kunakuwaga na michezo ya hatari humu humu mjini! Inabidi tuchekiane badae
Ni kam kulazimisha penzi, utapewa ila kama umewekewa gogo😁😁😁 nipo nipo tu
 
Hahahahahah hapo kutatua matatizo yote hayo ni aheri ulipie mke mahari uoe 😅😅😅 na harusi kabisa!

Tukiwaambia gari zetu wamatumbi ni Toyota wanajitia ujuaji! Hapo Service tu ya vifaa vyote cost yake ni bora kununua IST tu! Niliwahi ona BMW 3 series inauzwa juzi kati et 4.5m na gari ni DPT imenyooka😅 sana nikajiuliza dah 4.5m for a Bmw kuna namna!


Ungelipia tu mpunga bila kujiuliza...


Unaachaje mambo mazuri kama hayo?😂😂😂

Halafu uache kufananisha gari za Ulaya na mke...

Bora kuwa na gari la Ulaya linakupasua kichwa ndani kuliko kulipa mahari...
 
Ungelipia tu mpunga bila kujiuliza...


Unaachaje mambo mazuri kama hayo?😂😂😂

Halafu uache kufananisha gari za Ulaya na mke...

Bora kuwa na gari la Ulaya linakupasua kichwa ndani kuliko kulipa mahari...
😅😅😅😅😅😅 hizo fault 20 unaziangalia kwa wasiwasi eeh! Hata zingekuwa kila moja kuiondoa ni elfu 50 tu still kipengele kizito
 
Hahahahaahaah mkuu wewe acha sema toyota wacha aendelee kupendwaa ...changamoto ya European car ukizoea huwez kutoka ..mama akifungua fweeezwaaa walahi country man inanihusu

Sema at least now utakuwa na experience.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Izo nimereplace juzi mkuu,,,izo fuse zilikuwa zimepigwa waya nyingi na kubwa balaa lkn nilikuwa nakula tu maisha na nimezibadili sio kwa sababu kulikuwa na tatizo kwa kweli wacha mjep awe mjep,,ila Nina swali mkuu naweza kufanya computer diagnosis kwenye starlet ep 82!?View attachment 1930296

Aiseeee....

Lisipotokea tatizo lolote kwenye gari hizo fuse unaweza kuzitumia na waya hizo kwa muda mrefu. Ila siku ilitokea short circuit au current kubwa, moto unaanz.

Kwa starlet haiwezekani mkuu. Kidogo ni gari ya zamani.
 
Toyota never disappoints, usijaribu hili kwenye Merc, Beamer ama Audi! Utalia

Kwenye gari yoyote kunjunga waya hivyo siyo shida sana.

Ila siku short circuit ikitokea au current kuwa kubwa umeisha....

Ila katika hali ya kawaida hamna shida.

Sababu hata huyo jamaa hiyo fuse katembea nayo sana ikiwa hivyo...
 
😅😅😅😅😅😅 hizo fault 20 unaziangalia kwa wasiwasi eeh! Hata zingekuwa kila moja kuiondoa ni elfu 50 tu still kipengele kizito

Hahahah... Shida ndio kama nilivosema hizo gari ukiendesha tu ilimradi inawaka na kutembea with time utalia kilio kikuu.

Tena Benz/BMW/Land Rover/Jeep/Ford zinaweza kukuvumilia.

Audi/VW japo spea ni cheap ukilinganisha na wengine ila matatizo huwa yanafululiza kama mwenye gari hajali...
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom