Hivi ndivyo Freeman Mbowe na genge lake anavyotafuna pesa za CHADEMA!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Mkaguzi Mkuu wa serikali(CAG) ameanika wazi jinsi ambavyo mabilioni ya pesa za CHADEMA yanatafunwa bila huruma na wajanja wachache huku chama kikiendelea kuwa na ofisi Kuu katika kibanda kwenye mtaa wa Ufipa Kinondoni wakati huo huo Mbowe akidai chama hakina pesa za kuwalipa watumishi mikoani na wilayani.

Haya yamebainishwa katika repoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Hii inazidi kudhihirisha kuwa CHADEMA ina wenyewe kwa sababu hakuna kiongozi au mwanachama atakayethubutu kuhoji sana sana watajitokeza wapambe wake kumtetea kwa kutumia hoja za nguvu badala ya nguvu za hoja.

Kwa mtaji huu wa kujichotea pesa bila kuulizwa au kuwajibishwa, Mbowe hawezi kuachia nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa!

Kinachoshangaza zaidi ni kuwa CCM ya sasa katika ukaguzi huu haina ufisadi kama wa CHADEMA pamoja na kwamba ni chama kikubwa na chenye pesa nyingi na miradi mingi.

Kwa maelezo zaidi nimekuwekea hapa chini sehemu ya uozo ndani ya CHADEMA uliobainishwa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya serikali 2016/17.

Screenshot_2018-04-12-02-05-22.png

Screenshot_2018-04-12-02-01-15.png

Screenshot_2018-04-12-02-03-10.png
 
Chama kitolee maelezo hizi tuhuma. Hauwezi kujinasib au kuwa na uhalali wa kuikosoa serikali kama una walakini kwenye namna unayoendesha mambo yako.

Chamsingi, isije tu ikawa siasa imechukua mkondo wake badala ya taaluma na weledi tukaja kuambiwa hii taarifa ni siri.
 
Tangu serikali ya ccm ilipoanza kutafuna pesa za walipa kodi umepiga mahesabu?
Nilijua tu watetezi wa aina yako watajitokeza.

Kwa kukusaidia ni kuwa upande wa CCM hesabu zake hazina matatizo ya ufisadi kama ilivyo CHADEMA.

Hata kama kungekuwa na matatizo huwezi kusema viongozi wa CHADEMA wanalipiza kile ambacho kimefanywa na serikali ya CCM!

Hizi ni fikra ndani ya akili matope!

Kwa mtaji huu haishangazi kuona siku hizi hata neno ufisadi limekuwa bidhaa adimu ndani ya midomo ya wanaCHADEMA!

Kwa mtindo huu wakipewa hazina yote ya taifa itakuwaje?
 
Mbowe anaikopesha CDM 2 billion, tena kwa riba kali hapa lazima kuna mgongano wa ki maslahi. Huyu “Kim Jong Un” wa CDM akipewa nchi atafilisi kila kitu. Nyumbxxx watakuja kutetea hadi huu uozo wa wazi, kama misukule vile.
Pesa imekuwa ikihibwa miaka yote ktk serikali ya ccm lakini hamsemi! Ila hivyo visenti vya CDM vinawatoa roho wanga nyiye.
 
Kwa hiyo Nkurunzinza Mbowe tumuweke fungu moja na kina Chenge, mafisadi wote walio uraiani?
2020 Mbowe ataki imbia CDM baada ya ruzuka kuporomoka huku akiwachagiza nyumbxxx wake kuwa amegawa kijiti, hapo ndio utajua Mmachame si mtu wa mchezo mbele ya pesa.
Umachame unahusiana nini? Unaonyesha jinsi gani ulivyo mkabila. Mbowe mtoto wa mjini na amekulia Dar. Kabila amerithi tu wala halina influence yeyote kwake!
 
Chama kitolee maelezo hizi tuhuma. Hauwezi kujinasib au kuwa na uhalali wa kuikosoa serikali kama una walakini kwenye namna unayoendesha mambo yako.

Chamsingi, isije tu ikawa siasa imechukua mkondo wake badala ya taaluma na weledi tukaja kuambiwa hii taarifa ni siri.
CHADEMA wakitolea maelezo ya kuridhisha naomba unistue!

Hakuna mwenye kuhoji na kama akijitokexa basi lazima ajue kuwa huo ndio mwisho wa uanachama wake ndani ya CHADEMA.
 
Sijaona hela zilipotafunwa, zaidi ya kanuni kutokuzingatiwa wakati fedha zinakopwa. Ni kweli CHADEMA ina wenyewe na watu hao ni wana CHADEMA.
Acha ushamba, huelewi maana ya conflict of interest, Msechu wa NHC analala Kisutu saivi kwa makosa haya haya, alikuwa anajipa tenda yeye mwenyewe na mke wake, Ukiruhusu huu ujinga, Mbowe ana uwezo wa kwenda kukopa bank kwa riba ndogo halafu anakuja kuikopesha CDM kwa riba kubwa, mwisho wa siku ruzuku haionekana kwa kuwa inaishia kulipa wizi wa Mbowe.
 
Upuuzi uliopitiliza na hoja mufilisi hii. Hivyo mleta mada unayajua mahesabu ya CCM? Ni heri usiyajue, waweza kuzimia iwapo wewe ni mzalendo wa kweli.
Mimi nimeleta ya CHADEMA, hayo ya CCM ni kazi yako kuyaleta.

Kwa hiyo kama mahesabu ya CCM ni mabovu ndiyo inahalalisha pia mahesabu ya CHADEMA kuwa mabovu.

Huu ujinga umejifunzia wapi?
 
Nilijua tu watetezi wa aina yako watajitokeza.

Kwa hiyo viongozi wa CHADEMA wanalipiza kile ambacho kimefanywa na serikali ya CCM!

Hizi ni fikra za karai!

Kwa mtindo huu eakipewa hazina yote ya taifa itakuwaje?
Wewe uko biased na huo usema kweli wako ni wamashaka.
 
Back
Top Bottom