Hivi ndivyo Dawa za Kulevya zilivyomnufaisha Makonda ndani ya kipindi kifupi tu

muvika online

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
374
283
MAKONDAA.jpg


Baada ya kuja na operesheni ya kupambana na dawa za kulevya, jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda linaweza kuwa ndilo lililotajwa zaidi katika mkutano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita na kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki ya pili sasa.

Makonda alianza kuwa mjadala ndani na nje ya nchi baada ya kutaja orodha ya kwanza na ya pili ya watu maarufu wakiwamo wasanii, wanasiasa na viongozi wa dini na kuagiza wafike Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam wahojiwe kuhusu dawa za kulevya.

Kasi ya kutajwa kwa jina lake iliongezeka zaidi Jumatano iliyopita baada ya kumtaja Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima na mfanyabiashara Yusuf Manji.

Hata hivyo, Mbowe, Gwajima na Manji wamekanusha vikali kuhusika na biashara hizo na kuahidi kumshtaki Makonda kwa kashfa. Gwajima na Manji wameshahojiwa polisi.Katika mtandao wa kijamii wa JamiiForums, hadi kufikia juzi saa 8:00 mchana, kulikuwa na kurasa 49 ambazo jina la Makonda lilikuwa limetajwa mara 961 katika mijadala iliyokuwa ikiendelea.Mijadala hiyo ilikuwa ikihusu kama Makonda yuko sahihi au la katika utaratibu alioutumia na kama ana mamlaka ya kuagiza watu kuripoti polisi.
 
hapa naona makonda akihusika moja kwa moja sasa baada ya kupata naona anataka kutoka msafi.Serikali inafaa wamchunguze lakni naona hilo haliwezekani kutokana na ukanda.Tanzania ni bora ya jana.
 
Vita dhidi ya mkuu wa Mkoa wa Dar ilipambamoto kama sio kushika kasi baada ya kutangaza list ya madawa ya kulevya.

Hii sio mara ya kwanza kwa juhudi dhidi ya vita ya madawa ya kulevya kupata upinzani mkubwa sana pale kunapoonekana juhudi za kuhakikisha kuwa yanamalizika.

Tukumbuke kuwa ilishawahi kupelekwa bungeni kwa hoja ya List ya wauzaji wa madawa ya kulevya kusomwa ili wananchi wawafahamu lakini hoja hiyo ilikufa kabla hata ya kuanza.

Baada ya Mh. Mkuu wa mkoa kuonesha nia ya dhati ya kupambana na wauza madawa tuhuma mbali mbali toka kila kona ya nchi na nje ya nchi zilianza kumiminika kwake.

Jambo la kushangaza zaidi tuhuma hizo zilianzishwa na watu waliotuhumiwa au kuwa na uhusiano na watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Kuna kila dalili za wazi zinazopelekea kuamini kwamba kuna nguvu kubwa ya kiuchumi nyuma ya wale wanaopambana na mkuu wa mkoa, na wazo la kwanza linakwenda kwa wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.

vile vile ni jambo lililowazi kuwa Mkuu wa mkoa anatumika kuhamisha attention ya watu kutoka kwa vita ya madawa ya kulevya mpaka vita vya hisia zisizo na ushahidi kwa mkuu wa mkoa.

Mpaka sasa hakuna hata mmoja kati ya washtaki wa mkuu wa mkoa aliyekuja na ushahidi wa wazi kuhusiana na madai yao, jambo linalozidi kudhihirisha ukweli kwamba madai haya ni ya kupika yenye lengo la kupoteza jitihada za nia ya dhati ya mkuu wa mkoa kupambana na madawa ya kulevya.

Vita hii ya madawa ya kulevya ni kubwa kwani inahisisha kiwango kikubwa sana cha fedha, na ni mara chache sana nguvu ya fedha kushindwa isipokuwa tu kwa wazalendo wenye malengo mema na nchi hii.

Rai yangu kwa wananchi ni kutokubali kuyumbishwa na yanayoendelea sasa kwani yanatokana na vita aliyoianzisha mkuu wa mkoa dhidi ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.
 
nyie watu bogus kabisa. hao wauza unga ndio walimtuma atende jinai za kughushi nyaraka (CSEE certificate nk) na kuteka nyara kituo cha utangazaji? hili suala la cheti lingeibuka tu siku moja. si tumesikia kwamba alikuwa anajipanga agombee ubunge jimbo la Nyamagana, unafikiri huko lisingeibuka suala la cheti feki? hivi ni kitu gani cha maana saaaana kipya ambacho Bashite kakifanya katika hiyo vita feki dhidi ya dawa za kulevya ambayo haijawahi kufanywa? naona kitu kipya pekee ni ku-blackmail watu ili apate magari, nyumba na fenicha. hawa mapapa ya unga hayajaingia kwenye vita dhidi ya Bashite maana hajawagusa kama anapigwa nao basi ni vidagaa vya unga. Mnawajua mapapa ya unga au mnawasikia tu?
 
Kweli mkuu, Makonda kawashika pabaya "nyoka" wote wametoka shimoni. Hatukuwahi kuwaona na kuwajua kumbe ndo drug dealers wenyewe. Wengine wanajiita naaskofu kumbe ni wazee wa ngada, wananajisi Biblia kumbe ndo wanaosababisha kuharibika kwa ndugu zetu mitaani.

HRLC, Askofu, TLS, Magazeti na wengine ni nyoka waliofumuka mashimoni na sasa hari zao si nzuri. Wanasema wanaifia nchi huku wakiua ndugu zetu, Mungu na awalaani
 
Mnapotosha Jamii

Madawa ndio yalimtuma kutumia jina na vyet vya mtu mwingine

Madawa ndio yalimtuma kuvamia tv station kulazimisha kipindi "chake" kurushwa?
 
nyie watu bogus kabisa. hao wauza unga ndio walimtuma atende jinai za kughushi nyaraka (CSEE certificate nk) na kuteka nyara kituo cha utangazaji? hili suala la cheti lingeibuka tu siku moja. si tumesikia kwamba alikuwa anajipanga agombee ubunge jimbo la Nyamagana, unafikiri huko lisingeibuka suala la cheti feki? hivi ni kitu gani cha maana saaaana kipya ambacho Bashite kakifanya katika hiyo vita feki dhidi ya dawa za kulevya ambayo haijawahi kufanywa? naona kitu kipya pekee ni ku-blackmail watu ili apate magari, nyumba na fenicha. hawa mapapa ya unga hayajaingia kwenye vita dhidi ya Bashite maana hajawagusa kama anapigwa nao basi ni vidagaa vya unga. Mnawajua mapapa ya unga au mnawasikia tu?
Labda nikusahihishe mkuu,suala la cheti lilishaibuliwa toka mwaka 2015 kuna uzi upo humu ila sijui jonsi ya kuutrace, sema lilikuwa halijashika kasi.

Kutokana na kufanya vitu bila weredi ndio watu wakataka kujua uwezo na elimu yake maana mnaweza kumlaum mtu kumbe uwezo wake mdogo.....hapo ss ndio makaburi yakafukuliwa kwa kasi na hadi kutufikisha tulipo ss
 
Madawa ya kulevya ndo yalienda clouds fm? madawa ya kulevya ndo yaliyofoji vyeti? Mbona kamishna wa kupambana na madawa kamuita Ridhiwan lakini hatusemi ni vita ya madawa?
Bachite anatishia watu kuwaweka kwenye list ya dawa za kulevya!
 
Back
Top Bottom