Hivi ndivyo CUF walivyosagana kikatiba, wala wasitafute mchawi

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Natumai mpo ktk hali njema wale wote wanaopitia ukuta wangu huu kwa njia ya kujifunza, kukebehi na hata wengine kuanza kufunzwa na muda juu ya maandiko yangu yanayoendelea kuishi. Niliahidi kuja na andiko hili na nitaliandika ktk mfumo wa masuali na majibu, masuali ambayo watanzania wanajiuliza na majibu yake nitayatoa kupitia katiba ya chama cha CUF

Kabla sijaenda ktk hoja husika naomba niweke kumbukumbu ya tarehe zifuatazo ambazo zitanisaidia kurudi ktk masuali ya wapendwa wangu

1.Tarehe 5.08.2015 Profesa Lipumba aliaandika barua ya kujiuzulu na tarehe 6.08.2015 akawathibitishia waandishi wa habari na watanzania wote

2. Tarehe 13.06.2016 Lipumba alitengua maamuzi yake ya kujiuzulu

3. Tarehe 22.08.2016 CUF waitisha mkutano mkuu kuridhia Lipumba kujiuzulu

Kupitia vidokezo hivyo sasa narudi ktk andiko langu na kuanza kwa mfumo nilioueleza hapo juu

1. Je chama cha CUF kilikua sahihi kuitisha mkutano mkuu wake tarehe 22.08.2016 kuridhia kujiuzulu kwa Lipumba na kufanya uchaguzi wa mwenyekiti mpya?

Katiba ya CUF Inajibu....Nanukuuu...

Ibara ya 71(5) Endapo kiongozi mkuu wa chama ataachishwa au kufukuzwa uongozi basi uchaguzi wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kuvuliwa madaraka kiongozi mkuu yeyote utaitishwa kwa kipindi kisihozidi siku mia moja na themanini (180) tangu nafasi hio iwe wazi

Ufafanuzi....kwa kua nafasi ya mwenyekiti wa CUF ilikua wazi tokea tarehe 5.08.2015 na mkutano mkuu uliitishwa tarehe 22.08.2016 hii ni takribani siku 382 kwa maana zimezidi siku 180 zilizotakiwa kikatiba kwa maana hio hapa CUF wamevunja katiba yao mchana kweupe bila kumurika na tochi ktk hili wasimtafute mchawi tukija kisheria kwa mujibu wa katiba ya CUF Mkutano ule haukua halali

2. Je katiba ya CUF inaruhusu au hairuhusu kiongozi mkuu kujiuzulu na kutengua maamuzi yake ya kujiuzulu?

Katiba ya CUF inajibu.....nanukuu

Ibara 107(1) Kiongozi yeyote wa chama anaweza kukiuzulu uongozi wake wakati wowote ule.
(2)Kiongozi atajiuzulu kwa kuandika barua na kuweka saini yake kwa katibu wa mamlaka iliyomchagua au kumteua na kiongozi huyo atahesabiwa kuwa amejiuzulu ikifika tarehe aliyoanisha katika barua yake kuwa atajiuzulu pindipo akikubaliwa na mamlaka iliyomchagua au iliyomteua, au kama hakuainisha tarehe ya kujiuzulu kwake basi atahesabiwa amejiuzulu mara baada ya katibu wa mamlaka iliyomteia au kumchagua kupokea barua hiyo na kuijibu.

Ufafanuzi ....
Katiba ya CUF imekaa kimnya kuhusu kutengua maaamuzi ya kujiuzulu kwa hali hio kama katiba haijaeleza chochote basi sheria inaruhusu kutengua maamuzi hayo na pia hakuna ushahidi wa majibu aliyopewa Lipumba na katibu wake kama katiba inavyotaka na hali hio ikamfanya Lipmba kutengua maamuzi yake tarehe .13.06.2016 kabla ya mkutano mkuu kuitishwa.. Hapa wa kumlaumu ni katibu mkuu aliyeshiriki kumlea huyu msaliti Lipumba kwa kukosa umakini na majukumu yake kikatiba pamoja na katiba butu ya CUF

3. Je ni sahihi kukaimisha madaraka ya katibu mkuu hata kama yupo?

Katiba ya CUF inajibu.
.
Ibara 96(1) Pale ambapo mwnachama yeyote wa chama mwenye madaraka kwa mujibu wa masharti ya katiba hii, kwa sababu yoyote ile, hawezi kutekeleza kazi zake kwa muda, au amesimamishwa au kuvuliwa madaraka kwa mujibu wa masharti ya katiba hii, mamlaka iliyo na uwezo wa uchaguzi au uteuzi wa nafasi hiyo inaweza kumteua mwanachama mwengine mwenye sifa zinazohitaji kukaimu madaraka hayo

4. Je nisahihi naibu katibu mkuu bara kua ndiye mwenye mamlaka ya juu Zaidi kuliko naibu katibu mkuu Zanzibar?

Katiba ya CUF inajibu ..

Ibara 72(3) Naibu katibu mkuu atakayemfuatia katibu mkuu kwa madaraka ni yule anayetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka katibu mkuu

NB...

MAALIM SEIF NA LIPUMBA KWA PAMOJA WALIVUNJA KATIBA YA CUF KWA KWA KUMTEUA MANSUR KUA MSHAURI WA WA KATIBU MKUU

KATIBA YA CUF INAJIBU...

Ibara 103(6) Mwanachama mpya wa chama hataweza kuchaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi ya uongozi katika chama kwa ngazi yoyote hadi hapo mwanachama Huyo ametimiza angalau miezi sita kama mwanachama isipokua pale ambapo pameanzishwa tawi jipya na ambapo wanachama wa tawi hilo wote ni wapya , katika mazingira hayo masharti ya kifungu hichi hayatatumika, ila katika hali hiyo viongozi wa muda wa tawi watachaguliwa na watashika madraka kwa kipindi kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi tisa ambapo itabidi viongozi wa kudumu wa tawi wachaguliwe
 
Umeeleweka Mkuu!
Prof alisoma na kuelewa vizuri loophole za Kikatiba Ndio sababu akalianzisha lakin Kama ilivyo mkurupuko wa Ukawa wakakurupuka lakin Mtatiro baada ya kutulia na kusoma kaelewa kaanza kujua walipokosea the same na aliekuwa anakaimu Kamati ya Uongoz mh.Wakili Msomi Mzee Taha Taslima nae kagundua walipochemka Ndio sababu kakaa kando

Maalim Seif ni ama akaombe radhi kwa Prof au ahamie Chadema maana Chama alichopanga kuhamia cha Jahazi Asilia kinafutwa kwa kutotimiza Masharti na ni Marufuku Chama kipya kuanzishwa mpaka 2020 baada ya Uchaguzi
Maalim anatakiwa kuhamia Chadema ili iwe rahisi kuvurugana na kina Mbowe maana Wapemba nao wanaijua ruzuku Kama walivyo Wachagga
 
Lipumba toka awali yuko sahihi kikatiba sio kwa mihemko ya wengine kuhusu huu migogoro.

Kazi ipo hapo kwasababu Maalim Seif alishakataa kata kata kufanya kazi na Prof Lipumba
 
BAdo Katiba yao inasema huwezi kurudi kwenye nafasi uliojiuzulu hadi ufikishe miaka miwili nje ya uongozi,Je Lipumba alifikisha hiyo miaka miwili??
 
BAdo Katiba yao inasema huwezi kurudi kwenye nafasi uliojiuzulu hadi ufikishe miaka miwili nje ya uongozi,Je Lipumba alifikisha hiyo miaka miwili??
Soma Vizuri aliyeleta ameleta na Vifungu Vya katiba na maswali yote likiwemo hili yamejibiwa. Nilivyo elewa katika inatamka aliyejiuzuru kwa kuandika barua anatakiwa awe amejibiwa maombi yake ya kukubaliwa au kukataliwa ndani ya miezi mitatu siku ila lipumba amekaa mwaka mzima siku 360 hakujibiwa barua yake. Katiba hapo ilishavunjwa na Chama Chenyewe na Lipumba tena akaandika barua ya kutengua maamuzi yake kabla Chama hakija amua Yale ya kwanza miezi miwili badae baada yalipumba kufuta kauli yake ndio wakakaa Pamoja kukubari maombi ya lipumba kituambacho so sasa kikatiba. So lipumba amewashika Pabaya kwa Kutumia katiba yao hawamuwezi hatawaende wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma Vizuri aliyeleta ameleta na Vifungu Vya katiba na maswali yote likiwemo hili yamejibiwa. Nilivyo elewa katika inatamka aliyejiuzuru kwa kuandika barua anatakiwa awe amejibiwa maombi yake ya kukubaliwa au kukataliwa ndani ya miezi mitatu siku ila lipumba amekaa mwaka mzima siku 360 hakujibiwa barua yake. Katiba hapo ilishavunjwa na Chama Chenyewe na Lipumba tena akaandika barua ya kutengua maamuzi yake kabla Chama hakija amua Yale ya kwanza miezi miwili badae baada yalipumba kufuta kauli yake ndio wakakaa Pamoja kukubari maombi ya lipumba kituambacho so sasa kikatiba. So lipumba amewashika Pabaya kwa Kutumia katiba yao hawamuwezi hatawaende wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwenye kujiuzulu kuna mawili je aliwapa muda ili wampe notice ya kukubaliwa au kutokubaliwa ,Je alitoa barua ya kutaka au kuwa na nia ya kujizuzulu au alijiuzulu bila kuwapa notice??
Kumbuka ukitoa 24 hours ya kujiuzulu maana yake hujawapa watu nafasi ya kuitathmini nia yake.

Hivyo huwezi kuweka kikao wakati ameshaondoka na ameishaamua kuondoka hivyo ile barua ya kutaka kujiuzulu hakutoa yeye ametoa 24 hours za kuacha akzi anarudije??
 
Back
Top Bottom