Hivi ndivyo CAG kaonesha sio dhaifu kama Ndugai.


heradius12

heradius12

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Messages
9,272
Points
2,000
heradius12

heradius12

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2011
9,272 2,000
Hili sakata limenifanya nifatilie na nijue nini maana ya neno "dhaifu" na je "dhaifu" ni tusi?

Maana ya neno "dhaifu" kutokana na kamusi.

Maana ''dhaifu'' , kivumishi....ni kitu kisicho na mashiko, isiyo kuwa na sifa, isiyovutia, enye afya mbovu, iliyokosa unono, namna duni duni, isiyo na uwezo au nguvu, isiyo kakamavu.

Je dhaifu ni tusi?
Katika maandiko ya kidini, Biblia Takatifu na qurani, zinaeleza kuwa wanadamu wote ni dhaifu. Hakuna mwanadamu mkamilifu mbele ya Mungu. Ndyo maana wote tunahitaji huruma na msamaha wa Mungu.

Yesu Kristu mwenyewe aliwaita wafuasi wake kuwa ni dhaifu akiwasisitiza wakeshe wakiomba huruma na msamaha wa mungu.( Nahisi ndugai angekuwa mmoja wa wafuasi wa yesu siku iyo iyo angeleft group).

Sio kuwa binadamu pekee ndyo wanaweza kuwa dhaifu, hata vitu wanavyofanya au kusimamia pia kwa mikono au akili zao vinaweza kuwa dhaifu. Serikali au Taasisi yeyote inaweza kuwa dhaifu maana haiendeshwi na mashine au maroboti. Inaendeshwa na binadamu ambao ni dhaifu.

Awamu ya 4 iliyoongozwa na Rais mstaafu Jakaya kikwete mara nyingi sana iliitwa dhaifu. Wapinzani wengi walimuita Raisi ni dhaifu sababu alishindwa kupambana ipasavyo na hali ya ufisadi uliokuwepo kipind icho.

2012 john Mnyika alisema bungeni kuwa Rais Jakaya kikwete ni dhaifu na wabunge wa CCM ni wazembe. Naibu Spika ambaye alikuwa ni Ndugai awamu iyo, alimtoa nje John mnyika baada ya kukataa kufuta kauli yake na kusisitiza kuwa Rais JK ni dhaifu. Ila Baada ya apo maisha yakaendelea kama kawaida.

Kikwete hakuwahi kuwajibisha yeyote kwa kumuita dhaifu. Mwishoni mwa awamu yake, aliwaambia watanzania kuwa walisema kuwa yeye ni dhaifu sasa anawaletea bulldozer. Hii maana yake slijishusha na kukubali kuwa yeye ni kiumbe dhaifu.

Press conference aliyofanya Spika wa bunge Juzi, ambayoa alitoa maneno yenye utata na hata kufikia hatua kumfananisha CAG na " mbwa" anayelishwa, hii inaonesha jinsi Ndugai alivyo dhaifu. Hii maana yake ameonesha hana sifa, uwezo au nguvu ya kuvumilia maneno yanayoweza kuwa ya kweli au uzushi. Mpaka akaona atumie pesa za umma kuitisha press conference ili tu amfananishe CAG na mbwa. Huu nao ni udhaifu wa kutumia madaraka na pesaa za umma ovyo.

Ukimya wa CAG baada ya press conference umeonesha kuwa CAG sio dhaifu kama Ndugai ingawa na yeye kama binadamu ana udhaifu wake. Angekuwa na udhaifu wa kama Ndugai na yeye angeitisha press conference na kumjibu kwa jazba kama Ndugai alivyofanya.

CAG hakuonesha udhaifu wake toka mwanzo wa sakata hili pale Ndugai alivyoitisha press conference mara mbili huku akimtishia CAG aje kwenye kamati ya maadili ya bunge. CAG hakujibu lolote. Alisubiri siku ikafika akawasili kwenye kamati ya maadili na akatoa hoja yake na kusimamia msimamo wake kuwa kweli bunge ni dhaifu na ataendelea kutumia neno dhaifu katika report yake.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
T

The Elephant

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Messages
3,232
Points
2,000
T

The Elephant

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2014
3,232 2,000
Mbwa mwoga huwa ana kelele nyingi sana mpaka mwenye nyumba anashindwa kulala
 
B

Blac kid

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
4,012
Points
2,000
Age
30
B

Blac kid

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
4,012 2,000
hakika nakwambia haka kajamaa kalivyo jeuri na hasira kali, kama kangekuwa ka mwanafunzi ka yesu halafu atamke yale maneno na dhaifu likiwemo. hakika yesu siku hiyo angekufa kwa kutandikwa gogo kichwani na haka kajamaa.
 
B

Blac kid

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
4,012
Points
2,000
Age
30
B

Blac kid

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
4,012 2,000
hakika nakwambia haka kajamaa kalivyo jeuri na hasira kali, kama kangekuwa ka mwanafunzi ka yesu halafu atamke yale maneno na dhaifu likiwemo. hakika yesu siku hiyo angekufa kwa kutandikwa gogo kichwani na haka kajamaa.
 

Forum statistics

Threads 1,285,939
Members 494,834
Posts 30,879,777
Top