Hivi ndevu huota baada ya muda gani?

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
19,730
10,057
Habari zenu wanaJF,

Mwenzenu natatizika kidogo hapa! Inaweza inaonekana kama suala la kijinga lakini ni bora tuliongee hapa!

Mimi ni kijana mtu mzima tu, umri wangu ni 23, na niko higher learning second year!

Mpaka sasa sina hata chembe ya ndevu kwenye kidevu changu compared to my fellows, nikiangalia umbo langu nilivyo mrefu, natatizika!

To some extent, ndevu zinaleta heshima kidogo!!!! Sasa mie mbona sina hata kidogo? Nimechoka kutaniwa taniwa na kuitwa mtoto!

Jamani sorry kama kuna ntakae muudhi!
 
pole sana zingekuwa zinabadilishana ninge kupa japo za tumboni kwangu kidogo zinanikera,
 
Usihadaike ukubwa,ona ng'ombe mkubwa hana ndefu ila beberu la mbuzi dogo lina ndevu.

Ndevu ni shani tu toka kwa muumba.
 
Dah! kaka kweli kwenye miti hakuna wahunzi...jinsi ninavyotaabika na hizi ndevu kila siku asubuhi lazima nizinyoe imekua ni sehemu ya maisha kama vile kupiga mswaki. ingewezekana kubadirishana ningekupatia aisee.
 
Hapo ndo hazioti tena nakumbuka mimi zilianza kutoka nikiwa na miaka 17 sasa hivi nazinyoa style yoyote niitakayo vp zivu unalo au?
 
Pole sana hata mimi nimemaliza elimu yangu ya juu bila ndevu ba hapa nilipo sina na wala sina pressure maana najua zinakuja tu.....
 
Pole sana hata mimi nimemaliza elimu yangu ya juu bila ndevu ba hapa nilipo sina na wala sina pressure maana najua zinakuja tu.....

mkuu kuna vijamaa vilikuwa chini kabisa ya age yangu by that time nikiwa form 2. vyenyewe vina vindevu lakini mimi wapi!
 
Ndevu huanza kuota mtu anapoanza kubalehe lakini wengine huota ndevu hata baada ya miaka 25 hivi pia inategemea na ulivyorithi.

ahsante mkuu!

ila hapo kweny kurithi, naomba uelezee kidogo inakuwaje!

nini hasa kinachorithiwa!
 
Hapo ndo hazioti tena nakumbuka mimi zilianza kutoka nikiwa na miaka 17 sasa hivi nazinyoa style yoyote niitakayo vp zivu unalo au?

mkuu hapa sasa unanitisha!! zisiote kabisa?

kuhusu zivu, hilo ninalo mpaka kero!

nalikwanguaga kila baada ya nusu mwezi!
 
Dah! kaka kweli kwenye miti hakuna wahunzi...jinsi ninavyotaabika na hizi ndevu kila siku asubuhi lazima nizinyoe imekua ni sehemu ya maisha kama vile kupiga mswaki. ingewezekana kubadirishana ningekupatia aisee.

mi aisee naboreka!!

kwanza by structure mi ni mrefu kama hasheem th. sasa kwa kipimo hicho ukiwa huna kimzuzu unaonekana kinda sana!!

yani nikiingia kula lecture lazima niitwe dogo! kisa tu kidevu smooth!
 
Usihadaike ukubwa,ona ng'ombe mkubwa hana ndefu ila beberu la mbuzi dogo lina ndevu.

Ndevu ni shani tu toka kwa muumba.

hahaaaa!! asante! but ndevu nazo zina heshima yake ujue!
 
Kwangua kidevu kwa wembe kutoa vinyweleo....baada ya muda zitajaa.....
 
Dah! kaka kweli kwenye miti hakuna wahunzi...jinsi ninavyotaabika na hizi ndevu kila siku asubuhi lazima nizinyoe imekua ni sehemu ya maisha kama vile kupiga mswaki. ingewezekana kubadirishana ningekupatia aisee.

Hahahaaa nimecheka sana, yaani ndevu uinaboa sasa mim kwenye ndevu kuna mvi kibao hadi naboreka siyo siri
 
Dogo hebu tulia kwanza!ndevu kama huna kitu zinakuwa kama fagio la chooni...piga kitabu ukipata hela zinamea zenye afya
 
Back
Top Bottom