Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,481
- 30,152
Kwenye ile miaka ya 60 na 70 kutokana na nchi yetu kuwa nchi ya kijamaa na nchi yetu kuwa rafiki mkubwa wa China ambayo nayo ilikuwa inafuataal mfumo wa kijamaa/kikomunisti chini ya Kiongozi wao mkuu Mao Tse Tung, wakawa na kauli mbiu yao ya zidumu fikra za Mwenyekiti, wakiwa na maana Mwenyekiti wao Mao yuko sahihi katika maamuzi yake kwa asilimia 100, kwa maana hiyo walimchukulia Kiongozi wao Mao kama mungu mtu!
Kwa hiyo nchini China ilikuwa ni marufuku kumpinga Mwenyekiti wao wa kikomunisti Mao Tse Tung kwa jambo lolote lile na yeyote aliyejaribu kufanya hivyo alikuwa ni lazima akamatwe na wengi wao wakawa wanafungwa jela na wengine wengi wakapoteza maisha.
Sasa kutokana na nchi yetu wakati huo kupenda kuiga kila kitu wanachofanya wachina, baadhi ya 'wapambe' wa Mwalimu Nyerere nao wakajaribu kuintroduce hiyo slogan ya China ya zidumu fikra za Mwenyekiti.
Hata hivyo aliyekuwa Mwenyekiti wa TANU/CCM wakati huo Mwalimu Nyerere akaipiga 'Stop' slogan hiyo na badala yake akaifanyia ukarabati na kuwaelekeza viongozi wenzake watumie slogan inayosema zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti.
Hii alikuwa akimaanisha zile fikra zake ambazo hazikuwa sahihi hazikupaswa zidumu, kwa maana nyingine zilipaswa kutupiliwa mbali!
Katika vitabu vyote vya dini vinabainisha kuwa hakuna binadamu yeyote ambaye yupo 100% perfect isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Hata hivyo hali ni tofauti kwa awamu hii ya 5 ambapo Kiongozi wetu kwa mfumo anaoendelea nao ni kama anajiona yupo 100% perfect na kutokana na hali hiyo ni kama hayuko tayari kukosolewa kwa maamuzi yake yoyote.
Tumeshuhudia Mkuu wetu akipiga marufuku shughuli zozote za kisiasa za vyama vya upinzani vikipigwa marufuku kufanya shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020.
Wakati yeye kila anapofanya ziara zake kwa 'kofia' ya ziara za kiserikali, anafanya siasa kwa kukipigia debe la nguvu chama chake cha CCM na 'kuvikandia' kwa nguvu zake zote vyama vya upinzani!
Tumeshuhudia pia katika awamu hii ya 5 ikivunja rekodi ya kuweka ndani viongozi wa upinzani na wengine kufungwq jela kuliko kipindi chochote tokea tuanze upya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kwa 'makosa' tu ya kufanya shughuli za kisiasa za vyama vyao!
Tumeshuhudia pia wabunge wa upinzani wakifanya shughuli zao za kibunge kwa kubaguliwa na kuomewa kwa dhahiri kwa kufukuzwa Mara kadhaa bungen humoi mithili ya vibaka wa mitaani.
Cha kushangaza pia tumemsikia Mkulu akitamka hadharani kwa kumpongeza Spika Ndugai kwa namna 'anavyowanyanyasa' wabunge wa upinzani na yeye Mkuu akamhakikishia Spika Ndugai kuwa aendelee na Uzi huo huo wa 'timua timua' wabunge wa upinzani na wakija huku uraiani naye atatumia 'Ukamanda in chifu' wake kuwashughulikia wapinzani!
Tumeshuhudia pia wateule wa Mkulu wakiabuse power zao waziwazi kwa kuweka ndani viongozi wa upinzani bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Kutokana na watendaji hao kutochukuliwa hatua zozote na Mkulu ni wazi hayo mambo wanayofanya, yana all blessings kutoka kwa Mheshimiwa.
Tumeshuhudia pia kwa siku chache mfululizo zilizopita kwa wananchi mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali nchini wakifanya maandamano na mikutano ya hadhara ya kumpongeza Mkuu wa nchi kwa kile wanachokiita ushujaa wake wa kipambana na ufisadi.
Wakati hayo yote yakifanyika, upande wa pili wa kundi la pili la vyama vya upinzani hawaruhisiwi kufanya maandamano na mikutano yoyote ya kisiasa na alishapiga 'mkwara' kuwa kwa yeyote atakayedhubutu kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa unaokinzana na mawazo yake atamshughulika ipasavyo.
Kwa mazingira haya tunayoyaona zipo kila dalili za nchi yetu kurejesha mfumo wa China wa miaka ile ya 60 na 70 ya zidumu fikra za Mwenyekiti!