Hivi nchi yetu inarejesha mfumo wa zidumu fikra za Mwenyekiti?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,744
2,000
Kwenye ile miaka ya 60 na 70 kutokana na nchi yetu kuwa nchi ya kijamaa na nchi yetu kuwa rafiki mkubwa wa China ambayo nayo ilikuwa inafuataal mfumo wa kijamaa/kikomunisti chini ya Kiongozi wao mkuu Mao Tse Tung, wakawa na kauli mbiu yao ya zidumu fikra za Mwenyekiti, wakiwa na maana Mwenyekiti wao Mao yuko sahihi katika maamuzi yake kwa asilimia 100, kwa maana hiyo walimchukulia Kiongozi wao Mao kama mungu mtu!

Kwa hiyo nchini China ilikuwa ni marufuku kumpinga Mwenyekiti wao wa kikomunisti Mao Tse Tung kwa jambo lolote lile na yeyote aliyejaribu kufanya hivyo alikuwa ni lazima akamatwe na wengi wao wakawa wanafungwa jela na wengine wengi wakapoteza maisha.

Sasa kutokana na nchi yetu wakati huo kupenda kuiga kila kitu wanachofanya wachina, baadhi ya 'wapambe' wa Mwalimu Nyerere nao wakajaribu kuintroduce hiyo slogan ya China ya zidumu fikra za Mwenyekiti.

Hata hivyo aliyekuwa Mwenyekiti wa TANU/CCM wakati huo Mwalimu Nyerere akaipiga 'Stop' slogan hiyo na badala yake akaifanyia ukarabati na kuwaelekeza viongozi wenzake watumie slogan inayosema zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti.

Hii alikuwa akimaanisha zile fikra zake ambazo hazikuwa sahihi hazikupaswa zidumu, kwa maana nyingine zilipaswa kutupiliwa mbali!

Katika vitabu vyote vya dini vinabainisha kuwa hakuna binadamu yeyote ambaye yupo 100% perfect isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Hata hivyo hali ni tofauti kwa awamu hii ya 5 ambapo Kiongozi wetu kwa mfumo anaoendelea nao ni kama anajiona yupo 100% perfect na kutokana na hali hiyo ni kama hayuko tayari kukosolewa kwa maamuzi yake yoyote.

Tumeshuhudia Mkuu wetu akipiga marufuku shughuli zozote za kisiasa za vyama vya upinzani vikipigwa marufuku kufanya shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020.

Wakati yeye kila anapofanya ziara zake kwa 'kofia' ya ziara za kiserikali, anafanya siasa kwa kukipigia debe la nguvu chama chake cha CCM na 'kuvikandia' kwa nguvu zake zote vyama vya upinzani!

Tumeshuhudia pia katika awamu hii ya 5 ikivunja rekodi ya kuweka ndani viongozi wa upinzani na wengine kufungwq jela kuliko kipindi chochote tokea tuanze upya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kwa 'makosa' tu ya kufanya shughuli za kisiasa za vyama vyao!

Tumeshuhudia pia wabunge wa upinzani wakifanya shughuli zao za kibunge kwa kubaguliwa na kuomewa kwa dhahiri kwa kufukuzwa Mara kadhaa bungen humoi mithili ya vibaka wa mitaani.

Cha kushangaza pia tumemsikia Mkulu akitamka hadharani kwa kumpongeza Spika Ndugai kwa namna 'anavyowanyanyasa' wabunge wa upinzani na yeye Mkuu akamhakikishia Spika Ndugai kuwa aendelee na Uzi huo huo wa 'timua timua' wabunge wa upinzani na wakija huku uraiani naye atatumia 'Ukamanda in chifu' wake kuwashughulikia wapinzani!

Tumeshuhudia pia wateule wa Mkulu wakiabuse power zao waziwazi kwa kuweka ndani viongozi wa upinzani bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Kutokana na watendaji hao kutochukuliwa hatua zozote na Mkulu ni wazi hayo mambo wanayofanya, yana all blessings kutoka kwa Mheshimiwa.

Tumeshuhudia pia kwa siku chache mfululizo zilizopita kwa wananchi mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali nchini wakifanya maandamano na mikutano ya hadhara ya kumpongeza Mkuu wa nchi kwa kile wanachokiita ushujaa wake wa kipambana na ufisadi.

Wakati hayo yote yakifanyika, upande wa pili wa kundi la pili la vyama vya upinzani hawaruhisiwi kufanya maandamano na mikutano yoyote ya kisiasa na alishapiga 'mkwara' kuwa kwa yeyote atakayedhubutu kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa unaokinzana na mawazo yake atamshughulika ipasavyo.

Kwa mazingira haya tunayoyaona zipo kila dalili za nchi yetu kurejesha mfumo wa China wa miaka ile ya 60 na 70 ya zidumu fikra za Mwenyekiti!
 
yusuphfrancis

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
434
500
Nyere ndiye katufikisha hapa tulipo, kwa sababu alitengeneza katiba iliowapa mamlaka makubwa viongozi Wa serikari. Sasa wanatusomesha number kwa sababu yake
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,347
2,000
Hili jambo linahuzunisha lakini mtaji wake ni aina ya WaTz kuendekeza unafki, na kutokubali kupigania kile wanachoamini na haki yao ya msingi. Na kwa aina hii ya wananchi CCM wataendelea kuwawanyanyasa WaTz na kuwafanya mtaji wao wa utawala.

Cairo's
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,744
2,000
Nyere ndiye katufikisha hapa tulipo, kwa sababu alitengeneza katiba iliowapa mamlaka makubwa viongozi Wa serikari. Sasa wanatusomesha number kwa sababu yake
Kivipi Mkuu wakati tulimsikia Mkulu akitamka kuwa kwake yeye kipaumbele chake siyo Katiba ya nchi?

Bali priority no 1 kwake ni kuinyoosha nchi?
 
mgoloko

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
4,806
2,000
Kwenye ile miaka ya 60 na 70 kutokana na nchi yetu kuwa nchi ya kijamaa na nchi yetu kuwa rafiki mkubwa wa China ambayo nayo ilikuwa inafuataal mfumo wa kijamaa/kikomunisti chini ya Kiongozi wao mkuu Mao Tse Tung, wakawa na kauli mbiu yao ya zidumu fikra za Mwenyekiti, wakiwa na maana Mwenyekiti wao Mao yuko sahihi katika maamuzi yake kwa asilimia 100, kwa maana hiyo walimchukulia Kiongozi wao Mao kama mungu mtu!

Kwa hiyo nchini China ilikuwa ni marufuku kumpinga Mwenyekiti wao wa kikomunisti Mao Tse Tung kwa jambo lolote lile na yeyote aliyejaribu kufanya hivyo alikuwa ni lazima akamatwe na wengi wao wakawa wanafungwa jela na wengine wanapoteza maisha.

Sasa kutokana na nchi yetu wakati huo kupenda kuiga kila kitu wanachofanya wachina, baadhi ya 'wapambe' wa Mwalimu Nyerere nao wakajaribu kuintroduce hiyo slogan ya China ya zidumu fikra za Mwenyekiti.

Hata hivyo aliyekuwa Mwenyekiti wa TANU/CCM wakati huo Mwalimu Nyerere akaipiga 'Stop' slogan hiyo na badala yake akaifanyia ukarabati na kuwaelekeza viongozi wenzake watumie slogan inayosema zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti.

Hii alikuwa akimaanisha zile fikra zake ambazo hazikuwa sahihi hazikupaswa zidumu, kwa maana nyingine zilipaswa kutupiliwa mbali!

Katika vitabu vyote vya dini vinabainisha kuwa hakuna binadamu yeyote yeyote ambaye yupo 100% perfect isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Hata hivyo hali ni tofauti kwa awamu hii ya 5 ambapo Kiongozi wetu kwa mfumo anaoendelea nao ni kama anajiona yupo 100% perfect na kutokana na hali hiyo ni kama hayuko tayari kukosolewa kwa maamuzi yake yoyote.

Tumeshuhudia Mkuu wetu akipiga marufuku shughuli zozote za kisiasa za vyama vya upinzani vikipigwa marufuku kufanya shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020.

Wakati yeye kila anapofanya ziara zake kwa 'kofia' ya ziara za kiserikali, anafanya siasa kwa kukipigia debe la nguvu chama chake cha CCM na 'kuvikandia' kwa nguvu zake zote vyama vya upinzani!

Tumeshuhudia pia katika awamu hii ya 5 ikivunja rekodi ya kuweka ndani viongozi wa upinzani na wengine kufungwq jela kuliko kipindi chochote tokea tuanze upya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kwa 'makosa' tu ya kufanya shughuli za kisiasa za vyama vyao!

Tumeshuhudia pia wabunge wa upinzani wakifanya shughuli zao za kibunge kwa kubaguliwa na kuomewa kwa dhahiri kwa kufukuzwa Mara kadhaa bungen humoi mithili ya vibaka wa mitaani.

Cha kushangaza pia tumemsikia Mkulu akitamka hadharani kwa kumpongeza Spika Ndugai kwa namna 'anavyowanyanyasa' wabunge wa upinzani na yeye Mkuu akamhakikishia Spika Ndugai kuwa aendelee na Uzi huo huo wa 'timua timua' wabunge wa upinzani na wakija huku uraiani naye atatumia 'Ukamanda in chifu' wake kuwashughulikia wapinzani!

Tumeshuhudia pia wateule wa Mkulu wakiabuse power zao waziwazi kwa kuweka ndani viongozi wa upinzani bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Kutokana na watendaji hao kutochukuliwa hatua zozote na Mkulu ni wazi hayo mambo wanayofanya, yana all blessings kutoka kwa Mheshimiwa.

Tumeshuhudia pia kwa siku chache mfululizo zilizopita kwa wananchi mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali nchini wakifanya maandamano na mikutano ya hadhara ya kumpongeza Mkuu wa nchi kwa kile wanachokiita ushujaa wake wa kipambana na ufisadi.

Wakati hayo yote yakifanyika, upande wa pili wa kundi la pili la vyama vya upinzani hawaruhisiwi kufanya maandamano na mikutano yoyote ya kisiasa na alishapiga 'mkwara' kuwa kwa yeyote atakayedhubutu kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa unaokinzana na mawazo yake atamshughulika ipasavyo.

Kwa mazingira haya tunayoyaona zipo kila dalili za nchi yetu kurejesha mfumo wa China wa miaka ile ya 60 na 70 ya zidumu fikra za Mwenyekiti!
Mwenyekiti Pogba mwenye akili na fikra sahihi kuliko waTz wote
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,744
2,000
Sasa ni 'praise and worship' tu

zidumu fikra za mwenyekiti zote hata za ajabu ajabu?
Kweli Mkuu........

Hii ni awamu ya 'praise & worship'

Kwa yeyote ambaye hatasifu atashughulikiwa ndani na nje ya Bunge na popote pale atakapotoa mawazo yake kinzani na ya Mkulu!

Ndiyo maana hata wale waliokuwa wakiwatetea wadada wanaopata mimba za utotoni kama vile kubakwa, nao 'wameufyata' kwa kuwa Mheshimiwa keshatamka kuwa ndani ya awamu yake hatatokea binti aliyepata mimba hata kama atakuwa kabakwa, hatamruhusu yeyote aendelee na shule baada ya kujifungua!
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,300
2,000
Nyere ndiye katufikisha hapa tulipo, kwa sababu alitengeneza katiba iliowapa mamlaka makubwa viongozi Wa serikari. Sasa wanatusomesha number kwa sababu yake

Tatizo siyo Nyerere, tena mwache Baba wa taifa apumzike kwa AMANI. Huyu baba alikuwa mtetezi wa katiba na sheria hata kama zilikuwa mbovu.
Shida kubwa ni upuuzi wa kizazi cha sasa ambacho hakiwezi kutetea katiba na sheria.
Hata kama kutakuwa na katiba mpya, kwa ugoigoi uliopo, haitaleta ufanisi wowote.
Ni lazima uwe na uwezo wa kuisimamia na kuitetea katiba iliyopo ndipo udai mpya.
 
yusuphfrancis

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
434
500
Kivipi Mkuu wakati tulimsikia Mkulu akitamka kuwa kwake yeye kipaumbele chake siyo Katiba ya nchi?

Bali priority no 1 kwake ni kuinyoosha nchi?
Nilikosea kuandika mwanzo Wa sentensi. Nilitaka kuandika" nyerere ndiyo alitufikisha.......
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,744
2,000
Tatizo siyo Nyerere, tena mwache Baba wa taifa apumzike kwa AMANI. Huyu baba alikuwa mtetezi wa katiba na sheria hata kama zilikuwa mbovu.
Shida kubwa ni upuuzi wa kizazi cha sasa ambacho hakiwezi kutetea katiba na sheria.
Hata kama kutakuwa na katiba mpya, kwa ugoigoi uliopo, haitaleta ufanisi wowote.
Ni lazima uwe na uwezo wa kuisimamia na kuitetea katiba iliyopo ndipo udai mpya.
It is very true ulichosema, kuwa issue siyo Katiba kwa kuwa unaweza kuwa na Katiba nzuri tu, lakini kama watawala wasipotaka kuitii haitakuwa na maana yoyote.

Hebu nitoe mfano mmoja tu, Katiba yetu inaeleza kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi na ibara ya 18 ya Katiba hiyo inatoa ruhusa kwa kila mwananchi kuwa na Uhuru wa kutoa mawazo yake.

Hebu tuangalie je Rais alipata wapi madaraka ya kikatiba ya kukataza vyama vya siasa visifanye mikutano yoyote ya kisiasa na maandamano hadi mwaka 2020?

Mbona yeye kila anapofanya ziara zake anafanya shughuli za kisiasa za kikinadi chama chake cha CCM na kuviponda vyama vya upinzani?

Mbona kwa hii mikutano na maandamano yanayoendelea nchi nzima hatujalisikia Jeshi letu la Polisi likizuia mikutano na maandamano hayo kwa sababu zao zilizozoeleka za mambo ya kiintelejensia?

Hii mbegu ya ubaguzi inayopandwa na CCM ikiongozwa na Mwenyekiti wao itakuja kuliangamiza Taifa letu.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,481
2,000
Tulitaka Rais Kama Nyerere na kapatikana kwny upande wa Ubabe, kutoambilika na kuvuruga Uchumi, nafurahia sana haya Maisha
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,744
2,000
Tulitaka Rais Kama Nyerere na kapatikana kwny upande wa Ubabe, kutoambilika na kuvuruga Uchumi, nafurahia sana haya Maisha
Huwezi mfananisha Magu na Mwalimu Nyerere.....

Kumbuka moja ya hotuba zake muhimu alizotoa, nayo aliitoa mwaka 1995 ambapo alisema watanzania titahitaji kumchagua Rais ambaye ni lazima aitii Katiba aliyoapa nayo wakati anashika madaraka.

Mwalimu alienda mbali zaidi kwa kusema iwapo tutachagua Rais ambaye hatataka kuitii Katiba yetu, Rais wa aina hiyo hatufai.

Mwalimu akabainisha zaidi kuwa Rais wa aina ni bora akatuachia Urais wetu na yeye akaenda kufanya shughuli zake nyingine kama kuchunga ng'ombe!

Cha kushangaza clip za Mwalimu zenye maelekezo hayo muhimu hata TV stations binafsi zinahofia kuzionyesha kwa 'kumgwqya' huyo Bwan
Tatizo siyo Nyerere, tena mwache Baba wa taifa apumzike kwa AMANI. Huyu baba alikuwa mtetezi wa katiba na sheria hata kama zilikuwa mbovu.
Shida kubwa ni upuuzi wa kizazi cha sasa ambacho hakiwezi kutetea katiba na sheria.
Hata kama kutakuwa na katiba mpya, kwa ugoigoi uliopo, haitaleta ufanisi wowote.
Ni lazima uwe na uwezo wa kuisimamia na kuitetea katiba iliyopo ndipo udai mpya.
Umempa jibu zuri sana.

Ni kweli asimsingizie Mwalimu, kwa kuwa yeye alikuwa akisisitiza sana Rais wetu aitii Katiba aliyoapa nayo wakati anaingia madaraka ni.

Nakumbuka moja ya speech zake muhimu sana aliyoitoa mwaka 1995, alipoongea kwa msisitizo mkubwa kuwa watanzania tunapaswa kuchagua Rais atakayeitii Katiba yetu.

Akaendelea kuweka mkazo kuwa Rais ambaye hataki kuitii na kuifuata Katiba yetu hatufai.

Anaendelea kwa kusema kuwa Rais wa aina hiyo ni bora akatuachia Urais wetu na yeye akaenda kufanya shughuli zake nyingine kams za kufuga ng'ombe......

Cha ajabu clip hiyo vyombo vya habari vya TV vinagwaya kuionyesha hiyo clip kwa kumhofia Mheshimiwa kwa kuwa alishavipiga mkwara vyombo vya habari kwamba hawana Uhuru wa kuhabarisha to that extent........
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,481
2,000
Huwezi mfananisha Magu na Mwalimu Nyerere.....

Kumbuka moja ya hotuba zake muhimu alizotoa, nayo aliitoa mwaka 1995 ambapo alisema watanzania titahitaji kumchagua Rais ambaye ni lazima aitii Katiba aliyoapa nayo wakati anashika madaraka.

Mwalimu alienda mbali zaidi kwa kusema iwapo tutachagua Rais ambaye hatataka kuitii Katiba yetu, Rais wa aina hiyo hatufai.

Mwalimu akabainisha zaidi kuwa Rais wa aina ni bora akatuachia Urais wetu na yeye akaenda kufanya shughuli zake nyingine kama kuchunga ng'ombe!

Cha kushangaza clip za Mwalimu zenye maelekezo hayo muhimu hata TV stations binafsi zinahofia kuzionyesha kwa 'kumgwqya' huyo Bwan

Umempa jibu zuri sana.

Ni kweli asimsingizie Mwalimu, kwa kuwa yeye alikuwa akisisitiza sana Rais wetu aitii Katiba aliyoapa nayo wakati anaingia madaraka ni.

Nakumbuka moja ya speech zake muhimu sana aliyoitoa mwaka 1995, alipoongea kwa msisitizo mkubwa kuwa watanzania tunapaswa kuchagua Rais atakayeitii Katiba yetu.

Akaendelea kuweka mkazo kuwa Rais ambaye hataki kuitii na kuifuata Katiba yetu hatufai.

Anaendelea kwa kusema kuwa Rais wa aina hiyo ni bora akatuachia Urais wetu na yeye akaenda kufanya shughuli zake nyingine kams za kufuga ng'ombe......

Cha ajabu clip hiyo vyombo vya habari vya TV vinagwaya kuionyesha hiyo clip kwa kumhofia Mheshimiwa kwa kuwa alishavipiga mkwara vyombo vya habari kwamba hawana Uhuru wa kuhabarisha to that extent........

Wewe ukimzungumza Nyerere unamzungumza wa baada ya kustaafu kwa kusikiliza Hotuba zake, wenzio tunamzungumza Yule Mtu ambae alikuwa hataki kusikia Mtu Ana Mawazo Tofauti na yake akiwa Rais
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,300
2,000
Tatizo siyo Rais, ni watendaji walio chini yake.
Hata hivyo, kiongozi hutegemea walio chini yake na mara nyingi hujisikia raha kama vile unapokuwa na mbwa mkali, utampenda na hutaki apate shida yoyote.
Jamii iliyostaarabika hakuna lawama kama hizi, viongozi wao wana raha kuliko wanaoongoza nchi masikini na zisizo na ustaarabu.
Pamoja na mapungufu binafsi ya kiongozi, kama ana wasaidizi wa kujikomba, hali itakuwa mbaya mno.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom