Hivi nchi yetu ilishawahi kunufaika na Chama chochote cha Upinzani?

Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyohoji, napenda kuenda moja kwa moja kwenye mada kama direct kick kwenye football.

Tangu hii nchi iingie kwenye mfumo wa vyama vingi, hivi tulishapata manufaaa yoyote kwa hawa wanaojiita wapinzani? CUF, ACT wazalendo, NCCR Mageuzi na CHADEMA walishaleta matokeo chanya kwa Wananchi?

Walishatupigania Watanzania tuwe na maendeleo? Au ni vyama vilivyogeuzwa kuwa makampuni binafsi ya watu? Nimeleta hili bandiko kama swali ili wenye akili timamu tukipata majibu tujue ukweli upo wapi.

Mfano Chadema walipata Kick kwa kuonekana wanapinga ufisadi, Je, nani aliwapa sapoti mpaka wakina Dk Slaa wakati huo wakawa mashujaa wa kisiasa? Ni wapinzani?

Leo hii Watanzania wanahitaji maendeleo, je hii Chadema iliyojaa nongwa ya kukosa ruzuku itawaaidia Watanzania? Kama hata huko nyuma walipata kick kupitia mgongo wa wanaCCM wenye uchungu na hili taifa sasa hivi ndio watakuwa na machungu ya kuwapigania Watanzania?

Tujitafakari kwa kina tujue ukweli juu ya nani ambae ana nia thabiti ya kuwasaidia Watanzania, maana kama chama cha upinzani kinaendekeza njaa na kutojali maslahi ya taifa kiuchumi na kisiasa, sababu tu viongozi wamekosa mustakabali wa kisiasa, tutambue ni tatizo kwa jamii yetu.
Wewe imewahi kunufaika nini toka kwa mkeo na watoto wako wasiofanyakazi.
Kumbuka kwenye kila jambo kuna manufaa hasi na chanya, manufaa ya mojakwamoja na yasiyo ya mojakwamoja.
Hakuna chama chochote cha upinzani duniani ambacho huendesha nchi, hilo ni jukumu la chama kilichopo madarakani ambacho hukusanya kodi toka kwa wananchi na kuzitumia kwa wananchi hao, hata hivyo wewe na mimi hatujawahi kunufaika na CCM zaidi ya serikali.
 
Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyohoji, napenda kuenda moja kwa moja kwenye mada kama direct kick kwenye football.

Tangu hii nchi iingie kwenye mfumo wa vyama vingi, hivi tulishapata manufaaa yoyote kwa hawa wanaojiita wapinzani? CUF, ACT wazalendo, NCCR Mageuzi na CHADEMA walishaleta matokeo chanya kwa Wananchi?

Walishatupigania Watanzania tuwe na maendeleo? Au ni vyama vilivyogeuzwa kuwa makampuni binafsi ya watu? Nimeleta hili bandiko kama swali ili wenye akili timamu tukipata majibu tujue ukweli upo wapi.

Mfano Chadema walipata Kick kwa kuonekana wanapinga ufisadi, Je, nani aliwapa sapoti mpaka wakina Dk Slaa wakati huo wakawa mashujaa wa kisiasa? Ni wapinzani?

Leo hii Watanzania wanahitaji maendeleo, je hii Chadema iliyojaa nongwa ya kukosa ruzuku itawaaidia Watanzania? Kama hata huko nyuma walipata kick kupitia mgongo wa wanaCCM wenye uchungu na hili taifa sasa hivi ndio watakuwa na machungu ya kuwapigania Watanzania?

Tujitafakari kwa kina tujue ukweli juu ya nani ambae ana nia thabiti ya kuwasaidia Watanzania, maana kama chama cha upinzani kinaendekeza njaa na kutojali maslahi ya taifa kiuchumi na kisiasa, sababu tu viongozi wamekosa mustakabali wa kisiasa, tutambue ni tatizo kwa jamii yetu.
Amini usiamini chadema isingekuwepo:
1. CCM isingemchagua Dkt Magufuli awe mgombea mwaka 2015. Wangemchagua mwingine aliyekuwa anafahamika kuliko Magufuli. Maana bila chadema hakuna Rais Dkt John.

2. Sera za chadema. Kuna mambo ambayo CCM inayatekeleza leo yanayotokana na ilani ya chadema. Mfano, elimu bure.

3. Kasi ya ccm kutimiza ilani yake inatokana na kwamba kando yake kuna chama kikubwa cha upinzani kinachokubalika pia ambacho kinaweza kushinda uchaguzi kama vigezo na masharti vikizingatiwa.

4. Uteuzi wa wagombea wa CCM. Wagombea wa CCM wanachaguliwa ndani ya chama kwa umakini ili wawe na sifa za kushindana na wale wa upinzani.

5. Vyama vya upinzani vimekalia kiti cha baba wa taifa, Mwl Nyerere katika kuikosoa serikali na viongozi wake. Maana baada ya baba wa taifa kufa hakukujitokeza mtu mwingine kama baba wa taifa. Wazee waliosalia ni waoga wanaosukumwa na maslahi yao binafsi na familia zao. Hivyo kukemea ingeshindikana kwao.

Hivyo vyama ni muhimu sana kwenye taifa. Sasa hivi haviko bungeni subiri uone kitakachotupata wote. Just wait and see
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom