Hivi nchi yetu ilishawahi kunufaika na Chama chochote cha Upinzani?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyohoji, napenda kuenda moja kwa moja kwenye mada kama direct kick kwenye football.

Tangu hii nchi iingie kwenye mfumo wa vyama vingi, hivi tulishapata manufaaa yoyote kwa hawa wanaojiita wapinzani? CUF, ACT wazalendo, NCCR Mageuzi na CHADEMA walishaleta matokeo chanya kwa Wananchi?

Walishatupigania Watanzania tuwe na maendeleo? Au ni vyama vilivyogeuzwa kuwa makampuni binafsi ya watu? Nimeleta hili bandiko kama swali ili wenye akili timamu tukipata majibu tujue ukweli upo wapi.

Mfano Chadema walipata Kick kwa kuonekana wanapinga ufisadi, Je, nani aliwapa sapoti mpaka wakina Dk Slaa wakati huo wakawa mashujaa wa kisiasa? Ni wapinzani?

Leo hii Watanzania wanahitaji maendeleo, je hii Chadema iliyojaa nongwa ya kukosa ruzuku itawaaidia Watanzania? Kama hata huko nyuma walipata kick kupitia mgongo wa wanaCCM wenye uchungu na hili taifa sasa hivi ndio watakuwa na machungu ya kuwapigania Watanzania?

Tujitafakari kwa kina tujue ukweli juu ya nani ambae ana nia thabiti ya kuwasaidia Watanzania, maana kama chama cha upinzani kinaendekeza njaa na kutojali maslahi ya taifa kiuchumi na kisiasa, sababu tu viongozi wamekosa mustakabali wa kisiasa, tutambue ni tatizo kwa jamii yetu.
 
Kamanda bandiko wazi mbona haujaibu kama tumenufaika?
Wapinzani watanufaisha vipi na nyie CCM mnawazuia kwa nguvu za dola wasionyeshe leadership? You don't give them opportunity to lead. Mnaua, all sosrts of intimidation.

Lisu risasi 38 mmemwaga, 17 zimempata bado mnataka kujua nchi inanufaikaje, are you kidding? Go and rant somewhere else.
 
Vyama vya upinzani ni vizuriiii saanaaa na vina Sera ambayao inaweza kuwa mbadala wa CCM hapo baadae, tatizo lao niviongozi wao ndo hawafai kuviongoza. Mfano kwenye uchaguzi wa mwaka huuu, hakunachama cha upinzani kilicholeta mgombea anayekidhi wadhifa wa kuwa raisi wa taifa hili ilikuleta ushindani thabiti dhidi ya chama tawalaa.
 
Wapinzani watanufaisha vipi na nyie CCM mnawazuia kwa nguvu za dola wasionyeshe leadership? You don't give them opportunity to lead. Mnaua, all sosrts of intimidation.

Lisu risasi 38 mmemwaga, 17 zimempata bado mnataka kujua nchi inanufaikaje, are you kidding? Go and rant somewhere else
Kumbe alipigwa risasi zote hizo?
 
Ufisadi mkubwa uliowahi kuibuliwa nchi hii ulitokana na wabunge wa upinzani, Richmond - Kafulila kipindi akiwa NCCR, speaker Marehemu Samuel Sitta pamoja na mapungufu yake lakini walau alikuwa anaheshimu katiba kwa kiasi flani, Sasa hivi speaker badala ya kuongoza bunge kuhoji serikali, analiongoza kuilinda serikali kwa lolote, ingekuwa enzi za Sitta, tungejua 1.5 tillion zilipotelea wapi.

Unataka wapinzani wakupe maendeleo gani, wakujengee barabara kwani wao ndiyo wanaokusanya kodi? Maendeleo wanayokupa ni kukuonyehsa ubovu na makosa ya serikali, japo serikali chini ya chama tawala watapinga lakini chini ya kapeti kuna wanayorekebisha baada ya upinzani kupiga kelele. Hata kuna mambo mengine serikali ya CCM ilichukua kutoka kwenye ilani za vyama vya upinzani.

Ukisema nani ana nia thabiti ya kuwasaidia watanzania una maana gani? Maana kwa miaka zaidi ya 50 watanzania wanaongozwa na chama kile kile sasa kama mpaka sasa wanahitaji msaada, hata wewe unakubali kuwa wanahitaji kusaidiwa, ni kichekesho kusema CCM wako serious! Miaka 50 madawati hayatoshi, miaka 50, bado tunapigana na ujinga. Wakati tuna madini, samaki, mbuga, gas asilia, misitu na ardhi kubwa yenye rutuba. Kuna vinchi vinazalisha miwa tu na utalii ila wananchi wana maisha mazuri tu. Funny
 
Malunde hii mada yako ya kitoto kweli, wapinzani zaidi ya kusema bungeni unataka wakasemee wapi kwingine? na kama kila wakisema bungeni hawasikilizwi Spika anailinda serikali na chama chake CCM ulitaka hao wapinzani wakasemee wapi kwingine ili wasikilizwe?

Au unataka wapinzani wachangie ujenzi wa SGR na Stiglers Gorge?

Siku nyingine ukiamka usingizini jipe muda wa kutafakari mambo, sio unakurupuka tu kuanzisha mada zisizo na kichwa wala miguu.
 
Unao uhakika kuwa skendo zote ufisadi ziliibuliwa na wapinzani? Hujui kuwa ni wana CCM ndio waliziibua?
 
Malunde hii mada yako ya kitoto kweli, wapinzani zaidi ya kusema bungeni unataka wakasemee wapi kwingine? na kama kila wakisema bungeni hawasikilizwi Spika anailinda serikali na chama chake CCM ulitaka hao wapinzani wakasemee wapi kwingine ili wasikilizwe?

Au unataka wapinzani wachangie ujenzi wa SGR na Stiglers Gorge?

Siku nyingine ukiamka usingizini jipe muda wa kutafakari mambo, sio unakurupuka tu kuanzisha mada zisizo na kichwa wala miguu.
Sio mada ya kitoto kamanda, kwani mpaka uingie bungeni ndio uwe na hoja zenye mashiko?
 
Unao uhakika kuwa skendo zote ufisadi ziliibuliwa na wapinzani? Hujui kuwa ni wanaCcm ndio waliziibua?
Umejuaje ni wana CCM wakati wapinzani ndio waliozipeleka bungeni, weka ushahidi hapa tuuone wacha kutupigia kelele asubuhi.
 
Unao uhakika kuwa skendo zote ufisadi ziliibuliwa na wapinzani? Hujui kuwa ni wanaCcm ndio waliziibua?
Ndiyo zote kubwa, ikiongozwa na richmond hadi kafulila alifikia kuitwa tumbili, halafu wana CCM walipambana sana kuwalinda wahusika, hadi kuna mbunge wa CCM ambaye Asumpta Mshana alifikia hadi kuwalaumu wanaoungana na wapinzani kuwakaanga wahusika kuwwa siyo wana CCM, inaelekea wana CCM hulindana kwenye ufisadi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom