Hivi nchi hii tunakwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nchi hii tunakwenda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Oct 21, 2008.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  _IGP2299 i.jpg

  Jamani hivi nchi hii tutafika wapi?
  Huyu mtoto alipata adha ya kuungua ndani ya nyumba siku nne zilizopita na kuletwa hospitali ya mkoa wa Kagera pale Bukoba mjini. Na hata sasa bado yupo hospitali.
  Lakini mama wa mtoto analia kabisa maana hajapata matibabu yoyote kwa mwanae mbali ya kupewa asprin tu kila siku.
  Kidonda cha huyu mtoto kinaonyesha kuwa huyu mtoto kichwa kinaweza hata kuoza kwa jinsi kidonda kilivyo hoi. Huwezi kuvumilia kumuangalia mtoto huyu kwa hata dakika tano kwa hali aliyonayo.
  Mama wa mtoto anasema hata hali ya chakula anachokipata kwa ajili ya kulisha mwanae ni ugali tu na maharage yasiyo na chumvi.
  Hivi hii ndiyo kikwete amekuwa akijisifia kuwa afya imeboreshwa nchini?
  Nenda uangalie na uchafu ulivyosheheni hospitali pale hapo utaelewa ni nini kinaendelea.
  Jamani mtoto huyu asaidiwe. Yeye ni kama watoto wengine wa mafisadi. anahitaji dawa. Anahitaji msaada wa kila aina. Na hapo ndipo tusimame kuwaambia watanzania, afya imeboreshwa. La sivyo huu ni utapeli wa kisiasa kwa watanzania.
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  What a cute boy! Looks like boy. Sidhani kama hospitali ya hapo Bukoba yaweza msaidia huyu mtoto kwa jinsi alivyoungua. Yahitaji apelekwe Bugando haraka sana.

  Serikali imesisitiza kuwa maisha bora yapo vijijini na hali ndio hii??? Hata dawa za dharula hakuna!!!

  Mchukia fisadi kama upo Bukoba.... unadhani mtoto atafikaje Mwanza kwa matibabu?
   
  Last edited: Oct 21, 2008
 3. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ingekuwa vizuri kama tungepata jinsi ya kumsaidia.

  let us save a life.... au mnasemaje?
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ni aibu na Mungu anaweza kuilaani nchi yetu ikiwa tutaendlea kuachia damu zisizo na hati kupotea bila sababu za msingi.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mundu,
  Huyu mtoto anaweza kufika Mwanza kwa taarifa niliyonayo ni kwamba mama yake hana uwezo hata wa kujilisha pale hospital sijui kama anaweza kumudu gharama hizo.
  Hata hivyo basi si hospitali wangemwambia kwamba hawawezi kumuhudumia na kwamba anahitaji kuwa refered kwenye hospital kubwa ingekwa bora ili atafute njia ya kumsaidia mtoto wake huyu?
  Inasikitisha kweli.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mrembo lakini tumsaidieje? mtoto hayuko na hali nzuri kichwani. Isitoshe pale hospital hana lishe nzuri ya kumsaidia kupona kidonda haraka!
  Hali si nzuri kwa kweli
   
 7. M

  Mjasiliamali Member

  #7
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si' dhani kama hao madaktari wanaweza kumsaidia mpaka wa simamiwe na wananchi wenye hasira kwani si kwelikama hospital yote haina dawa za kumtibu japo yeye. hivyo ina hitajika pia nguvu ya wananchi katika kusimamia suala hilo.
   
 8. M

  Mjasiliamali Member

  #8
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika pitapita yagu nilikuwa nikizunguka katika makapuni ya wawekezaji wa kigeni hapa nchini, lakini chakushangaza ukiangalia kipato cha huyo anaye tumikishwa kwa kiwango cha kimataifa, utatamani kulia, kwani mzalishaji ni Mtanzania, ambaye Serekaliyake ndiyo ime idhinisha alipwe kiwango hicho,lakini atumikishwe kama treni yamizigo. na cha kusikitisha zaidi,pindi ajapo mgeni ambaye anaelimu sawa na mtanzania, atalipwa mara20 ya huyo mlalahoi, wa kibongo na kilakitu atapewa, nakubuka kuna waziri mzima asiye na haya wala kujua kuwa wananchi ndio walio mpa kiti kile, ali simama bungeni akasema kuwa kilamtu atalipwa kwa kiwango cha elimu aliyonayo sasa maswali ya fuatayo....Kipi bora kumlipa msomi anaye iba kama karamagi anaye danganywa katika vijimgahawa na kusaini mikataba vibaya au kuajiri mtumwenye elimu anaye weza kuitumia elimu? je na je mwananchi akilipwa vizuri ni serekali inafaidika au ni makosa? je kuna aja yakuwa na viongozi wasio watendaji? je kwanini wabunge wanapitisha haraka miswaada yao haraka kuliko umeme, hasa ile ya kuongezewa posho na marupurupu? KWANINI...WAWEKEZAJI WANAO WATUMIA WA TANZANIA KUZALISHA KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA WASI WALIPE WATANZANIA HAO KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA?
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mjasiliamali ni kweli yote unayoyasema. Je mtoto huyu afe kwa ajili ya mafisadi wachache wanaodhani neema ni yao peke yao katika nchi hii?
  Nahurumia kitoto hiki kisicho na hatia. Kinafaa kisaidiwe jamani, hivi tutajibu nni mbele za Mungu tunayeapa kwa jina lake kuwasaidia wananchi wa Tanzania?.
   
 10. M

  Mama JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Mchukia Ufisadi, upo hapo Bukoba kwa sasa?

  hebu jaribu kupitisha mchango wa sha sha kwa watu walio karibu yako wanaoweza kusaidia. Ukipata laki moja hapo huyu mama atafika Mwanza. Vinginevyo mama afunguliwe account, but this is an emmergency case. Mtoto anahitaji matibabu immediately!!! Ohh my poor boy.....
   
Loading...