Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Wife zamani akiniiuliza nilikuwa namjibu pika chochote,, nilivoona anaendelea siku moja nikamwambia pika mchemsho, akatabasam akasepa,, alivorudia siku nyingine nikamwambia pika nyama choma na ugali.

Siku hizi haniulizi tena.
Na huwa tunauliza vile we care about you tupike mpendacho ukiona huulizwi kakuchukulia poa Bora liende
 
Hapo ndipo unapata nafasi ya kusema hutaki dagaa. Usipikiwe.

Bila nafasi hiyo unaweza kupikiwa dagaa, kitu ambacho hupendi.
A4172207-22CD-45D5-A59F-0361DA261CCB.jpeg
This is my shiet😋
 
Mie nakula chochote uzuri sie tumefunzwa kula chochote kinachopikwa in the day toka utotoni!

Katika vitu ambavyo niligundua sipendi ni dagaa kauzu, kabichi, mchicha, magimbi na ndizi! Yani ukipika chakula nje ya hivyo ntakula tu sina tatizo.
Usizitaje ndizi basi unazionea!ila hapo kwenye dagaa na jamii yake ndo umeongea mimi hupenda kuwambia watu kwamba dagaa sio mboga
 
Spendi hili swali na nilishamwambia wife mara kibao lakini hataki kuacha kuniuliza uliza sijui nifanyeje mimi!
yaani hata nikiwa job unanipigia simu kuniuliza hivyo! Hivi kwani huewezi pika tu chakula nikakuta kimepikwa yaani mpaka nitoke job ninajua kwamba home kuna wali maharage leo! daah inabia sana!
 
Na mimi nimesema hivyo. Baba yangu hakuwa mpenzi wa nyama, labda za aina chache sana na sio mchuzi, na usithubutu kumpikia ugali usiku unless amekwambia. Na wanaume wengi wenye asili ya Mbeya; kumpikia ugali usiku ni ugomvi
Kinachokera ugali wa usiku ni ile njaa unaamka nayo asubuhi aisee
 
kuna upuuzi mwingine wa kutakiwa kurudi na vyakula ukitoka job. wakati umewaachia hela ya mwezi mzima. nilipohoji nikaambiwa mbona baba jirani huwa analeta. Majibu ilikuwa simple tu,kaolewe naye
Matunda hilo halina shida sababu misimu inabadilika badilika unaweza beba kafuko ka matunda daily ila sio eti ubebe mavitu ya kupika kila siku huo sio uungwana ikiwa mama umempa hela ya shopping ya vitu mwezi mzima.
 
Jamaa anaonekana wa ajabu sana. Yani anachukia ugali hao ndio wale daddy im going!

Ukiwa huna hobby ya kupika ni kazi ngumu kweli! Ila if you are creative there are a million dishes yani! Na vitu ni vile vile tu ila unatwist kidogo tu unapata new dish. Unaongeza kidogo inakuwa kitu amazing.

Nunua vijarida vya mapishi vitakusaidia kuto run out of ideas! Mie sijui tatizo nina dada anapenda mapishi yani nikifikaga kwa shemeji yangu namuonea wivu anavyopikiwa vitu vizuri vizuri yani kama yuko 5 star hotel
Hahaha kimoyomoyo unasema sasa mbn cmpat kama huyu dada angu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kweli maisha yanatofautiana sana,maana nina miaka 17 ya uchumba sugu ila sijawahi kuulizwa swali hilo,ngoja nitafute hela maana ndio sababu ya kutoulizwa na % kubwa nahisi hatuulizwi kabisa,maana najua siku nikikuta ugali nyama ni kama suprise,tumezoea mwendo wa harage ugali na tembele tu
tafuta hela
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Mwambie mpange ratiba ya juma inasaidia kubajeti na kuounguza hayo maseali.
Jua kwamba na yeye anakanganyikiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom