Hivi nani mjinga, kati ya trrafic(polisi) na abiria/dereva wa basi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nani mjinga, kati ya trrafic(polisi) na abiria/dereva wa basi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by djochuku, Apr 11, 2012.

 1. d

  djochuku Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nasafiri siku moja kutoka Dar kwenda mbeya kwa Basi la Kampuni moja hivi.(Naomba nisitaje hiyo Kampuni).Kutoka kituo kikuu cha Mabasi Ubungo mwendo ulikuwa mzuri kabisa. Nasema mzuri kwa sababu ulikuwa ndani ya Kilometa 80 kwa saa.
  Nilifurahi sana kwa sababu mimi ni muoga sana wa mwendo mkali. lakini baadae nilona kuwa kadiri tulivyokuwa tunapunguza urefu wa safari yetu na mwendo ulizidi kuongezeka na kuwa mkali.Nilivumilia hadi Mikumi. Baada ya Mikumi,kwa wale wenyeji wa njia ya Dar -Mbeya,kuna eneo linaitwa IYOVI, kuna kona kali sana na kwa umbali mrefu hadi eneo la RUAHA MBUYUNI. Dereva alikuwa anakata kona bila kupunguza mwendo.
  nilimuuliza jirani yangu "mwendo huu vipi?" akanijibu "hii ndio ........ (Akataja jina la Kampuni) mpaka saa 11:00 tupo Mbeya." Nikamuuliza tena, "na huu mwendo kwenye kona?" akaniangalia kwa mshangao na kujibu, " Kwani wewe mgeni na gari hili?,humu kawaida Dereva anakata na zote( Yaani speed kali)" kwangu mimi niliona kama ana maana kuwa anakata na roho zetu zote.
  Nilipoona kwangu nimeshindwa nilimuita Kondakta nikamnong'oneza," Kaka huu mwendo mbona Mkali?" akanijibu tena kwa sauti,"Kamuulize dereva." yakaniishia kwani alikuwa sahihi. jirani yangu akaendelea kunipa somo,"Wafanya biashara wote huwa wanapanda basi hili kwa kuwa wanawahi kufika na kupumizika" Nikawaza, ni kweli wanawahi kufika.Lakini ikitokea bahati mbaya hata kwa mungu wanawahi kufika na kupumzika.
  Nije kwenye hoja yangu sasa,nilichogundua njiani ni kwamba, Madereva wa mabasi njiani wanawashiana taa kama ishara kuwa mbele kuna Traffic ana Tochi , yaani kifaa cha kugundua mwendo kasi wa gari,hapo utaona kuwa mwenda unapungua na pengine chini ya hata kilometa 80 kwa saa. Traffic atapanda ndani ya gari na kuuliza kama kuna tatizo. wote wanajibu hakuna.Basi likiondoka tu na kuhakikisha kuwa Traffic yupo mbali, mwenda ni ule ule, Dereva anakata kona na roho zetu zote. mbele tena anapunguza mwendo,Traffic anapanda na kuuliza maswalli yale yale na majibu ni yale yale. sasa:-

  • Tukianza na huyu Traffic,hivi hajiulizi kwamba,kama kweli Basi hili lingekuwa linatembea mwenda uliopo kwenye hiyo tochi yake( KM 80 kwa saa) lingekuwa eneo hilo muda huo?
  • Sisi abiria tunaulizwa kuna tatizo tunasema hakuna.
  • Dereva akienda mwendo wa kawaida, abiria tunamtukana na kumwambia tutakuwa hatupandi mabasi ya kampuni hiyo.inakuwaje?
  • Uzoefu unaonyesha kuwa,ikitokea ajali abiria wanalalamika kuwa Dereva alikuwa anakimbia sana.Lakini mbona, Traffic walikuwa wanauliza njiani na wanapewa majibu kuwa kila kitu ni sawa?
  Sasa hapa nani mjinga,Abiria/Dereva au Traffic au wote?
   
 2. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mi naona wote ni wajinga
   
 3. m

  mgadafi Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wote watatu wajinga
   
 4. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kumbe na wewe ulikuwamo humo humo wakati Traffic akiuliza kama kuna tatizo, umenyamaza na kuja kuulizia hapa kama ni ujinga au lah. Mimi naona mjinga ni wewe
   
 5. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,451
  Likes Received: 4,733
  Trophy Points: 280
  Great thinker alijisahau hapa
   
 6. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  si ufunguke tu mkuu kuwa hilo basi ni ama
  Nganga
  Happy Nation
  au Budget
  maana hayo ndio mabasi yanayokimbia km kina Lewis Hamilton na Jesse Button.
  kwa hiyo kama ni muoga wa mwendo panda zako Sumry linalofika saa 2 mbeya hakikisha una helmet la sivyo jiandae kupigwa nondo
   
 7. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Piga,ua,galagaza,hilo basi ni Happynation.
   
Loading...