Hivi nani kaiwekea Tanzania vikwazo vya uchumi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nani kaiwekea Tanzania vikwazo vya uchumi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamayu, Jun 13, 2012.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Siku zinavyosonga mbele ndivyo ugumu wa maisha unaongezeka; mfano mfumuko wa bei umekuwa ukishika kasi kama vile moto kwenye mbuga yenye majani makavu. Kwa sasa mfumuko wa bei ni karibu asilimia 25 (National Bureau of Statistics Tanzania - NBS). Miaka ya 80s mfumuko wa bei ulifikia karibu 30% kwa sababu ya IMF and WB conditions and internal factors especially drought and nincomp**p top government leadership. Mara nyingi nchi zinazowekewa economic sanctions kama Iran ndio zinakuwa na hali mbaya kama ya Tanzania kwa sasa, nani ametuwekea vikwazo vya uchumi Tanzania katika kipindi hiki? Je, ni international community? National community? Mafisadi? Ujinga wa wananchi? current top government leadership?


  Je, nini kifanyike kupunguza huu mfumuko wa bei bila kuuza nchi?
   
 2. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Yaani Mkuu umenifurahisha kweli leo. Unauliza swali wakati jibu lipo wazi kabisa? Viongozi wenu mliojichagulia ndio wanawawekea vikwazo vya uchumi. Hata Marehemu Ng'walimu alisema sana. Wanaolilia Ikulu wanaenda kufanya biashara. Ili biashara yao ifane ni lazima wajue somo la COMPETITION. In the competition of the rivalry, the Five forces in the principales of Michael Porter must apply. power of wananchi (consumers), power of walanchi (suppliers), Threat of wapinzani (New Entry), central is the Ikulu of course which controls every means of the uchumi, that is where raivalry is focusing with corruptions of different colors - Richmond, BoT, IPTL, Madini, UDA, ATC, TRC, ....etc, at the expence of poor public services etc. There is possibility of substitutes too and the cost of switching (Democrasia ya vyama vingi danganya toto). Sijui nisemeje. Unaweza kuandika kitabu kikubwa sana.

  Kwa hiyo tusisingizie IMF na WB, ni viongozi wetu walioziba masikio na wamefumba macho kutoona uchumi mbovu ila wanamaximize kwa perceptions za sisi ni masikini wakati sio hivyo. Tanzania ingebebwa na kuwa Israel ungeshangaa katika mwezi mmoja tunashindana na Marekani kwa utajiri, sababu Israel pamoja na ujangwa walio nao wanaexport nje matunda na chakula na bidhaa kibao. Tusisingizie kuwa ni Taifa barikiwa, hata sisi Mungu katubariki ila tumeipenda njia ya shetani kwa utajiri wa haraka na ubinafsi na kutojali madhara kwa Taifa. Japan wana madini gani, mashamba gani hata tunanunua machines na vyakula kutoka kwao? Viongozi legelege huongoza Taifa legelege. Acha sera zitungwe kwa ajili ya wamachinga barabarani lakini tuwaache wazungu wachimbe madini na kutuachia mashimo na kutuulia ndugu zetu majirani kama paka ambaye unampa mfupa lakini ukimsogelea yuko radhi kukuchanachana kwa makucha yake. Mitanzania ndivyo tulivyo. We think too much of today with selfishness and none of tomorrow and on others. Ngoja ninyamaze mie. Nadhani kiduchu nimekujibu ni nani anatupiga miti watanzania. Ni viongozi wetu tuliojichagulia wenyewe.

  Oh! Nilisahau swali la pili tufanye nini. In fwact ukijua chanzo cha ugonjwa ni rahisi sana kutibu kwa dawa sahihi. Tuamke na kutafuta viongozi wa kweli bila kujali katoka chama gani cha siasa, ambao hawajiwekei shield wajilinde katika ufisadi wao. Tunawabana kwa katiba mpya tunayotakiwa kuwa waangalifu kuiwekea vizuizi na mifagio ya kuondoa uchafu mara moja kila mahali. Na mitanzania nayo iache uvivu wa kufikiri na kufanya mambo. Anayejaribu kuwa initiative asaidiwe pasi kinyongo na aenziwe. Ubunifu ni muhimu na uachiwe wazi. Nyumbu kiwanda cha magari kiko wapi na kimefanya nini mpaka sasa? Tutengeneze viwanda vyetu na kuexport sana, tunadanganyana na kilimo kwanza kwa jembe ati uti wa ngongo. Inawezekana kama tukiamua mmojammoja pasi vizuizi na ili tuendelee tunahitaji vitu vine: Watu, Ardhi, SIasa safi na Viongozi bora (Hapo ndipo hasa penye utata).
   
 3. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Vikwazo vya kiuchumi vimewekwa na uongozi mbovu uliopo madarakani. Mfumuko wa bei ni matokeo ya kudorora kwa uchumi wa nchi. Kila siku tunaambiwa uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia fulani lakini cha ajabu hali ya Mtanzania ni mbaya kila siku.

  Mafisadi wanaishi maisha mazuri na Watanzania walio wengi wanaishi kwa mlo mmoja per day.

  Hivyo vikwazo vipo kwa uongozi.  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...