Hivi nani competent kati ya Tundu Lissu Vs Peter Kibatala?


britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
11,040
Points
2,000
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
11,040 2,000
Hawa ni wanasheria nguli wote wanatetea upinzani,

Mi nawapima wanasheria kwa kuangalia yafuatayo
1.Idadi ya kesi alizoshinda
2.Idadi ya maamuzi Tata ya utafasiri wa sheria ambayo kayatatua yakawa mwongozo kwa wengine,
3.Idadi ya wateja reputable aliwatetea kwa crucial cases na kawashinda
4.idadi ya complicated cases ambazo amelegeza kwa kupangua vifungu mpaka zikawa za kawaida

Je kati ya hao wawili nani mkali sana?

Britannica
 
Stanley Mitchell

Stanley Mitchell

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2014
Messages
4,626
Points
2,000
Stanley Mitchell

Stanley Mitchell

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2014
4,626 2,000
Mimi ni wakili nimepata fursa ya kufuatilia hawa mawakili wawili kwa karibu sana. Ninachoweza kusema ni kwamba kumlinganisha Tundu Lissu na Peter Kibatala ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu, Lissu ni mlima na Kibatala ni kichuguu. Kibatala is very ordinary lawyer sema tu anajua kujitangaza vizuri sana (good marketing strategies). Kwa wale waliokuwepo mahakama kuu mbele ya majaji 3 kwenye kesi ya Mitaa 200 mwaka 2015 mliona siku jinsi naibu mwanasheria mkuu wa wakati huo Dr. Tulia Akson Mwansasu alivyomtoa jasho Kibatala ambaye alipoteza network kabisa hakawa kama vile hakujiandaa kabisa wakati Dr. Tulia sio legal practitioner bali ni academician lakini alimdhibiti Kibatala kikamilifu. Kibata alishindwa kesi ya Mita 200, Lissu hajawahi kushindwa kesi yoyote ambayo serikali ni mshitaki au mshitakiwa, kila mtu anajua jinsi Lissu alivyoigalagaza Serikali mahakamani kwenye kesi ya ugaidi dhidi ya Lwakatare na Ludovick Rwezaura au kwenye kesi ya uchaguzi ya Lema katika mahakama ya rufaa. Pia kesi Wasira dhidi ya Esther Bulaya kila mtu aliona jinsi Lissu alivyomfanyia kitu kibaya Wasira, Lissu kampiga Wasira mahakama kuu mara mbili na kampiga tena mahakama ya rufaa mpaka Wasira akaamua kustaafu siasa. Tundu Lissu hiyo ni habari nyingine, inaweza kuichukua nchi hii miaka 200 kupata mwanasheria bora kama Lissu. Unaposema top class lawyers wa Tanzania utawataja mawakili kama Lissu, Prof. Kabudi, Prof. Luoga, Magafu, Dr. Kilangi, Masumbuko Lamwai, Dr. Tenga na wengine wachache lakini sio bwana mdogo Peter Kibatala.

Kuna vitu sitaki kuongea kuhusu udhaifu wa Kibatala kwenye tasnia ya sheria maana staki nimvunjie heshima yake.
Very good objective analysis....

Mkuu Hata mimi nilishangaa sana mtu kama Tulia Ackson kushinda ile case ya mita 200...

Kibatala kapoteza kesi nyingi sana mfano ile ya Sugu Mbeya akapigwa miezi 5, kuna ile ya Lulu akapigwa miaka 2.......
 
Justice Cardozo

Justice Cardozo

New Member
Joined
Jan 13, 2019
Messages
2
Points
45
Justice Cardozo

Justice Cardozo

New Member
Joined Jan 13, 2019
2 45
Wajibu mkubwa wa mwanasheria akiwa kama ofisa wa mahakama,ni kuiongoza mahakama kufikia maamuzi sahihi, ima iwe kwa mteja kushinda kesi au kupoteza, mawakili hawaendi mahakamani kushindisha wateja wao, hivyo kupima ubora wa wakili kwa kipimo cha idadi ya kesi alizoshinda ni kinyume na maadili ya kazi ya uanasheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kelevra

Kelevra

Senior Member
Joined
Nov 23, 2018
Messages
111
Points
250
Kelevra

Kelevra

Senior Member
Joined Nov 23, 2018
111 250
Hawa ni wanasheria nguli wote wanatetea upinzani,

Mi nawapima wanasheria kwa kuangalia yafuatayo
1.Idadi ya kesi alizoshinda
2.Idadi ya maamuzi Tata ya utafasiri wa sheria ambayo kayatatua yakawa mwongozo kwa wengine,
3.Idadi ya wateja reputable aliwatetea kwa crucial cases na kawashinda
4.idadi ya complicated cases ambazo amelegeza kwa kupangua vifungu mpaka zikawa za kawaida

Je kati ya hao wawili nani mkali sana?

Britannica
Data zao sina ila nakuunga mkono kwenye namba 2 na namba 4...Japo impact yake ni moja tu ana create Landmark cases kupitia akili aliyojaaliwa....na kusababisha hata new rules kutengenezwa.
Idadi ya kesi na Idadi ya wateja kuna challenge nyingi mfano Rushwa huwezi jua network ya Lawyer kushinda kesi nyingi...
 

Forum statistics

Threads 1,295,907
Members 498,472
Posts 31,227,666
Top