ludoking
Senior Member
- Oct 5, 2008
- 124
- 71
Nimefuatilia hatua zote tangu upigaji kura hadi utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mku kwa upande wa Zanzibar lakini mpaka muda huu najiuliza hivi nani alishinda nafasi ya urais Zanzibar..ni CUF au CCM? Kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi Zanzibar, ilimtangaza mgombea kupitia CCM, Mh Shein kuwa mshindi kwa 50.1% akifuatiwa na maalimu Seif wa CUF kwa 49.1%. Hoja yangu naijenga kwa mazingira makuu mawili; moja ni hali walizoonyesha wagombea hao wawili baada ya kutangazwa matokeo na pili ni tofauti ya kura kati ya wagombea urais upande wa Mungano-Dkt JK na Prof. Lipumba. Japo Seif aliyakubali matokeo lakini ilionesha kuwa moyoni kuna siri nzito iliyokuwa imejificha ambayo iliashiria kwa vyovyote vile matokeo yalipindishwa. Na kama ni hivyo, je alikubali matokeo kuonyesha uzalendo kwa manufaa ya wazanzibari maana tofauti na hapo ingetokea vurugu ambayo hatujawahi kuishuhudia au ni alikubali kwa kuwa alijua lazima aingie madarakani? Kwa upande wa Mh Shein hakuonyesha haiba ya kufurahia ushindi wake "wa halali" wakati akitoa shukrani. Naye alionyesha kuwa kuna siri nzito ndani ya moyo wake iliyopelekea yeye kutangazwa kuwa mshindi. Na ukiangali matokeo ya kura za uraisi wa muungano, Lipumba alipata takribani 60% ya kura akimuacha mbali Mh JK. Ninavyo fahamu mimi kwa wazanzibari wa sasa..Zanzibar huwa kwanza then muungano unafuata. Iweje Maalimu apate 49.1% na Lipumba apate 60%? Kama kulikuwa na uchakachuaji basi waliochakachua siyo professionals kwani wali concentrate kuweka sawa kura za Urasi Zanzibar wakasahau za Muungano ndiyo maana bomu linafumuka. Haiingii akilini wazanzibari wampende Lipumba kuliko maalimu Seif. Kama ni hivi sidhani kwa sasa kuna haja ya kupiga kura mpaka hapo nguvu ya umma itakapoamua vinginevyo. Na hapo ndipo nakumbuka kauli mbiu ya CCM wakati wa kampeni kuwa "Kwa CCM, Ushindi ni 'lazima' "