Hivi na mwaka huu uchaguzi mkuu kura itakuwa ya wazi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi na mwaka huu uchaguzi mkuu kura itakuwa ya wazi!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bright, Apr 20, 2010.

 1. Bright

  Bright Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 sikupiga kura kwani uchaguzi ulikuwa wa wazi. CUF na DP waliongelea hili mara moja tu na kukaa kimya pengine baada ya kupewa nakala ya daftari la wapiga kura. Katiba yetu inasema kura ni ya siri lakini upigaji kura unakuwa wa wazi. Je huku sio kuvunja au kuisigina kabisa katiba ambayo wengi wa viongozi wa juu akiwemo M/kiti wa tume ya uchaguzi waliapa kuilinda huku wakiomba Mungu awasaidie? Mimi nafikiri kimoyo moyo wanaomba Shetani awaongoze kwa kutokana na wanayotenda! Mtikila mbona hujapeleka hili mahakama kuu?

  Muda mfupi kabla ya uchaguzi, nilikutana na mwandishi wa gazeti moja na kumwambia kwa nini hawajaliandikia hili wakati Mtikila na Hamad walishaongelea suala hili; alijibu na kuwa muwazi kuwa labda wananchi wapitishe 'petitions' lakini vinginevyo alikiri kuwa wataingia matatani!
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Unaposema upigani kura wa wazi unamaanishe uwe wa kunyoosha vidole?
   
 3. Bright

  Bright Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama utakumbuka karatasi ya kupigia kura ilikuwa na sehemu ya kujaza namba yako ya mpiga kura ambayo iko kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Hivyo ni rahisi kujua nani amempigia kura kiongozi gani. Namna hii ya kupiga kura waliiifanya CCM illi wabanane wao kwa wao na matajiri. Wapinzani walipiga kelele mara moja tu na mara wakapewa nakala ya daftari hilo nao kunyamaza kwani waliona ni vema nao kubanana wao kwa wao.

  Kwani kura ya siri ina maana gani? Mimi nafikiri ni kutokufahamu kabisa kwa mtu yoyote na chombo chochote cha serikali ikiwemo tume ya uchaguzi kuwa Mr. X amemchagua Ms. Y kwa namna yoyote ile.

  Cha ajabu tume haikusema matumizi ya hizo namba kwenye karatasi ya kupigia kura; kama ingekuwa kuhakiki waliopiga kura mbona majina ubandikwa pale nje ya kituo na mpiga kuara kabla hajapewa karatasi ya kupigia kura anaonesha kitambulisho chake na kuhakikishwa kwenye daftari halafu anapiga kura; hiyo namba ya nini sasa? Walichofanya wasimamizi wakawa wanawaandikia namba wapiga kura ili wasiache wazi au wasibadilishe namba - nilikwisha dhamiria kubadilisha namba kama mpiga kura angekuwa anaandika mwenyewe.

  Mimi naona hii ni kura ya wazi si lazima msimame nyuma ya mgombea, kunyoosha kidole au kupayuka/ kupiga mayowe kama vile Bungeni. Uoanishe namba ya kupigia kura na namba ya usajili wa gari; gari likitumika vibaya unachukua namba zake za usajili halafu mwenye gari anapatikana mara moja kupitia TRA labda namba ziwe 'fake'; vivyo kwenye uchaguzi kupitia tume ya uchaguzi utamjua nani kampigia nani!
   
Loading...