Hivi mwongozo wa Wizara ya Elimu kuhusu watoto kukariri darasa umekaaje?

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,137
809
Wanabodi,
Naombeni msaada nahitaji anaejua hili.
Kuna wakati nakumbuka wizara ya elimu ilitoa mwongozo kwa shule zote hasa shule binafsi kwa vile mtindo huu ulikuwa shule binafsi zaidi. Ya kuwa mtoto akishavuka kidato cha pili asikaririshwe darasa maana mtihani wa mchujo unahusu watoto wa kidato cha pili.
Majuzi nmekutana na rafiki yangu kanieleza mtoto wake kalazimika kukariri kidato cha tatu kwa vile hakupata wastani unaotakiwa na shule anayosoma hivyo hawezi kuingia kidato cha nne.
Nilimuuliza mtihani wa kidato cha pili alipata daraja gani? Akanijibu alipata daraja la kwanza na hajawahi kuelezwa kuhusu mtoto wake kushuka kitaaluma!
Mzazi alifunga safari toka Dar es salaam mpaka Geita, kuongea na mwalimu wa taalum huku akihoji, inakuwaje mtoto aliepata daraja la kwanza mtihani wa kidato cha pili leo kuingia kidato cha nne mnamrudisha? Ndiyo yawezakuwa kweli kateleza na akashindwa jupata wastani wenu mlioupanga, lakini kwa nini msiangalie back ground yake? Mwalimu wa taaluma alimjibu kwa mkato kuwa " Huo ndio msimamo wa shule".
Ibidi mzazi arudi zake Dar es salaam huku mtoto akikariri darasa.
Nikabaki na maswali, sasa kama ndo mzazi unalipa zaidi ya milioni mbili kwa mwaka, walimu hawakuiti kama mtoto kadrop au anaenda vizuri, mtoto kama alikuwa mzuri kichwani toka kidato cha kwanza mpaka cha tatu mwanzoni, kwa nini tusiwalaumu sasa hao waalimu kuwa wao ndo wamemharibu? Kwa nini wasimpe special program ili kumpandisha kama mwanzo na amalize kidato cha nne?
Hivi hii ni biashara au ni mkakati wa kutangaza shule kuwa wanaomaliza wote wanakuwa na division one?
Mwisho wa mwaka mmiliki wa shule anaita watu wa media huku akitamba kwamba shule yake inafanya vizuri na kuwazawadia watoto magari?
Hivi kama shule inakuwa na mtihani wa kuingia kidato cha kwanza na mtoto anafaulu, kunakuwa na mtihani wa mchujo wa kidato cha pili na mtoto anafaulu tena ufaulu wa juu, inakuwaje kidato cha tatu ashindwe kuingia kidato cha nne?
Wizara,hivi mnatuma wakaguzi kwenye hizi shule kufuatilia haya mambo?
Mkoa wa Geita hauna Afisa elimu? Hana taarifa kuwa watoto wanakaririshwa madarasa? N ahivi wizara inawaruhusu vipi kufanya mitihani wakati majina yao yalitakiwa yafanye mitihani mwaka unaokuwa umepita?
Hivi ikifuatiliwa,hakuna taarifa za ugonjwa kwa watoto ambao hawaumwi kuwa ulipelekea kurudia au kuahirisha mitihani?
Nahisi JPM ana kazi na safari ndefu, yaweza kuwa yeye ana vision tofauti na watenda kazi wake. Wizara inatoa mwongozo usiofuatwa, watendaji wapo na hawatolei maelekezo tukisema wanapewa hongo na wenye shule tutakuwa tuankosea?
 
Back
Top Bottom