HIVI MWISHO WA KUFUNGULIA MUZIKI KWA SAUTI KUBWA KATIKA MABAA(sehemx za starehe) NI SAA NGAPI?

Saskatchewan

Senior Member
Oct 16, 2011
148
21
Nashindwa kuelewa ktk haya maeneo ya starehe kwa mfano ktk mabaa, grocery, hotel nk. kupiga muziki kwa sauti kubwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wanaozunguka maeneo hayo. Wakati wa usiku wanafungulia muziki mpaka usiku wa manane matokeo yake tunashindwa kupata usingizi! Sie tunaokaa uswahilini tunapata shida sana!
 
Mwisho ni pale mwenye baa anapofilisika hawezi kuhonga polisi tena.
 
Nakumbuka kuna wakati nilikuwa naishi Chang'ombe,(jirani na TTC club),siku wanayopiga twanga nilikuwa napata shida sana ya kupata usingizi!
 
Hii nchi sijui tumelaaniwa. Matatizo chungu nzima hata kupanga miji hatuwezi. Polisi nao njaa tupu unakuta kituo cha polisi kipo karibu kabisa na bar halafu muziki mkubwa bado unafunguliwa! Matokeo yake tunarudi kwenye kauli ile ile kwamba we are not living but just surviving!
 
Nashindwa kuelewa ktk haya maeneo ya starehe kwa mfano ktk mabaa, grocery, hotel nk. kupiga muziki kwa sauti kubwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wanaozunguka maeneo hayo. Wakati wa usiku wanafungulia muziki mpaka usiku wa manane matokeo yake tunashindwa kupata usingizi! Sie tunaokaa uswahilini tunapata shida sana!
Mkuu kisheria kwenye mabaa mwisho ni saa tano usiku. Hotel nafikiri wanaweza kuwa na vibali tofauti vya kuuza pombe mpaka usiku wa manane. Kuna jirani yangu juzi alikuwa na shughuli kwake,nilikuwa nasikia kama P square wako humu chumbani aisee. Hili suala la "Noise pollution" inabidi liangaliwe kwa ukaribu zaidi.
 
hii ni headache jamani, hapa nilipo uswazi kwangu hatua kadhaa kuna ukumbi, jumamosi ya wiki iliyopita kulikuwa na sendoff, i see nilihudhuria sendoff ile nikiwa ndani kwangu, nilikosa msosi tu, kwa jinsi makelele yalivyokuwa makubwa....
 
mamlaka husika wanakaa tu ofisini! Wanaendelea kufanya kazi kwa mazoea!
 
hii ni headache jamani, hapa nilipo uswazi kwangu hatua kadhaa kuna ukumbi, jumamosi ya wiki iliyopita kulikuwa na sendoff, i see nilihudhuria sendoff ile nikiwa ndani kwangu, nilikosa msosi tu, kwa jinsi makelele yalivyokuwa makubwa....

inabidi tuanze kufanya mazoezi ya kulala hata kama kuna makelele! Manake kuna wengine wanapata usingizi bila wasiwasi hata kama kuna makelele!
 
Miji yetu imejaa kelele kuanzia miziki ktk bar,grocery,kumbi za starehe,nyumba za ibada na biashara!
 
na hivi vigodoro huku uswazi kuna vile vigodoro bwana weee utakoma mwenyewe
loh nachukia sana haya mambo pale kwetu ms nilienda kujifungua nikashangaa
mamlaka husika ziko wapi kuna kanisa limeanzishwa katikati ya nyuma za mtaani kwetu limegeuka kuwa kero
maana mda wote wanafungulia manyimbo yao na na spoka wamezipandisha jii ua mlingoti
kwahiyo ni kelele mpaka ukome ilinibidi nirudi haraka sana dar
maana mtoto angewehuka ndo nimemleta tu duniani hapa anakutana na makelele hayo
tena hapo jirani yetu kuna garage vijana wakavizia wakakata waya wa spika,huyo mtumishi wa mungu
akamleta nduguye mwanajeshi akafunga mtaa na kupiga watu hovyo loh
 
Back
Top Bottom