Hivi Mwigulu anajua asasi za Kiraia zimeajiri watu wangapi? Aziomba hela za NGO's kutoka USAID

Huku sasa ni kujisahau ?

Yaani kama taifa ni ombaomba...., Pili hao wanaotoa hizo pesa baada ya mtu kutoa maandiko fulani si ni kwamba wanapima na kuona kama hilo linalofanyika linafaa ? (Kwani si wangeona Serikali inafanya zaidi si wangepeleka huko, vilevile kwani ni kiasi gani wanapewa au wanataka kutuaminisha kwamba hawapewi)?

Hii nchi itabidi nianze mfumo wa media blockout ili nisisikie huu upuuzi.., yaani mtu unaweza ukapata stress bure kwa kusikiliza haya maneno, ukizingatia pesa za kununulia dawa nikiugua zote wameshazichukua kwenye Tozo...
 
Mh Waziri ajaribu kuangalia hizo fedha za USAmsaada zita ajiri watanzania wangapi na wanufaika wangapi? Jana Mh Rais kasema serikali haita ajiri kwa sababu imebusti ajira.

Waziri wake anakuja kwa mkono mwengine kutaka kunyanganya ajira zitazotokana na USAID. Tafuteni namna nyengine ya kupata huo uchafu wa Tanesco. Kuja na tarakimu ni kitu kimoja na kuraise hiyo fund ni shughuli nyingine pevu. Acheni kucheza na maisha ya watu kabisa.
 
HELA ZA TETEMEKO BUKOBA.
wajitahidi wawe wavumilivu hela ya maendeleo watakayopewa serikali wenzao wataiheshimu,na wao wenzao wakipewa hela za maendeleo INATAKIWA serikali IHESHIMU .
Sio nipe Mimi, nipe Mimi,
kwani hao wafadhili hawajui kuwa kuna serikali?
Magufuli alikuwa haombi fedha nje kiasi hicho bali alikuwa anabana walipa kodi wa ndani.
 
Hakuna msaada unaweza kutolewa kwenye mipango ya kimkakati inayolenga kujenga nchi hiyo ndo tabia ya mabepari...hizo fedha zote zitaishia kwenye Taulo za kike ...ujenzi wa Choo...haki za binadamu...nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Mwigulu anajua asasi za Kiraia zimeajiri watu wangapi?

Vijana wanateseka hawana ajira lakini hata wale walioajiriwa na asasi za kiraia Mwigulu anataka kuwanyang'anya hela ili hao vijana wakose ajira ilihali serikali nayo haina ajira. Mwigulu hapa umepotoka na naona ni kati ya watu ambao hawana huruma na vijana wa Taifa hili na una ndoto za kuwa Rais.

Kuna siku utapendekezwa vijana wote tupewe sumu tufe maana hutupendi hata kidogo. Hata hao USAID wamekuona kiumbe wa ajabu sana maana serikali mmeshidwa kukusanya kodi sasa mnataka na hela za NGO. Shame!

Pia, soma=> Waziri Nchemba, ameiomba USAID, kuelekeza msaada wa dola bilioni 1.3, kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita

View attachment 2165778
Safiii hiyo
 
Back
Top Bottom