Hivi Mwanaume Unakuwaje Boya Unayeshinda Umelala
Wakuu, kuna muda inabidi tuongee lugha ya machinjioni kwa sababu hawa viumbe wanaojiita wanaume wa kizazi hiki wamezvywa mno na umama.
Inakuwaje mwanaume mzima, una ndevu kidevuni, una sauti ya besi kama honi ya lori la mkaa lakini huna fani yoyote, huna kazi, na huna hata mia mbili ya dharura mfukoni mwako
Upo upo tu mjini kama tambala la deki lililotelekezwa chooni.
Kazi yako kubwa ni kushinda umejilaza kitandani, unakodoa macho kwenye screen ya simu huku ukiwaza shemeji yako au dada yako atakurushia saangapi buku mbili ya kula ugali.
Hivi wewe ni mwanaume kweli au ni demu aliyesahau kuvaa sketi
Inakuwaje mwanaume unafikisha miaka 30 lakini mikono yako haina ujuzi hata mmoja wa kueleweka Hujui ufundi wa pikipiki, hujui kompyuta, hujui kushona, hujui hata kushika jembe ukalime vishamba vya pembezoni mwa mji.
Umekaa tu kizembe umepishana mikono kifuani kama binti aliyekataliwa ukweni.
Nikuambie ukweli unaoukwepa, Huu ujinga wa kushinda unajipaka mafuta mwilini, unanyoa viduku vya ajabuajabu na kuvaa pensi fupi mtaani ukiwa huna mia mbili, haukufanyi uwe mjanja. Unajiona handsome boy wa mjini
Siku shemeji yako akichoka kukulisha ugali, atakufungia mlango mchana kweupe na utarudi kwenu kijijini ukiwa umeshika nguo mbili kwenye mfuko wa sandarusi.
Amka wewe Futa hayo makamasi ya usingizi uelewe jambo moja, Dunia haijawahi na haitawahi kumhurumia mwanaume, Ukiona unatafuta huruma na dezo kama dada yako, jiandae kisaikolojia kulipia gharama yake kwa dharau kubwa zaidi Mjini hapa hakuna mtu atakayekulisha bure bila kukutumia kama tambala la deki
Usipojiongeza sasa hivi ukaingia barabarani kutafuta fani na hela yako mwenyewe, hawa watu unaowaomba mteremko watakufanya vitu ambavyo vitakufanya ujute kwanini ulizaliwa mwanaume
Kama huna fani wala kazi lakini unataka kuvaa nguo za gharama, kumiliki simu kali na kunywa bia, mjini kuna wazee ambao wanasubiri wavulana wapenda dezo kama wewe
Mwisho
Lakini nakuahidi, kitakachokupata mbeleni hakitahitaji mkalimani utakuwa mfano bora kwa wengine.