Hivi Mwanaume kuzidiwa Umri na Mpenzi/Mwanamke wake ni miaka Mingapi wastani?

JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
2,573
2,000
Ila bana haya mambo ya umri hapana..aah Mimi hapana Yani mwanaume nikupite umri..aahh

Kila la kheri mkuu
Umuhimu wa umri upime kwa kuangalia uwezo wa mtu kutatua mambo na kiwango cha busara na sio miaka mtu aliyoishi duniani.

Sema mara nyingi umri mkubwa huambatana na uzoefu wa maisha na busara lakini si lazima iwe hivyo wakati wote.

Kuna vijana wana 30's wana uwezo mkubwa wa kulea familia na kutunza mke kuliko wababa wenye 50's
 
and 100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
1,769
2,000
Na unakuta kijana anakwambia hajawahi kuwa na furaha maishani kama anayopewa na mama yake
Mama ni mama tu, huwezi linganisha mwanamke yeyote duniani na mama yako kisa ni agemate, mama ana nafasi yake kama mzazi uliyekaa tumboni mwake for 9 mnths, akakunyonyesha, akakulea mpaka unakua, ukiachilia mbali yote hayo wewe kama mtoto ni damu yake, I mean kwenye damu yako kuna damu yake, how comes uje umfananishe huyo mwanamke na mwanamke mwingine..?

Hakuna mahala kitabu kimekataza kuoa mwanamke aliyekuzidi umri..

Kama gender equality ipo na unaiamini basi mwanaume naye ana haki kuoa mwenza mwenye umri kumzidi kama mwanaume mwenye miaka 40 anavyooa binti wa miaka 20, hivyo hivyo na mwanaume wa miaka 20 asionekane anamuoa mama yake kisa ana miaka 40.. mbona hawasemi kaolewa na baba yake kama mwanaume anamzidi mwanamke miaka 20πŸ˜‚

Mwisho kabisa kwa wenzetu Muslim mtume Muhammad (S.A.W) alioa mwanamke wa miaka 40 wakati yeye ana miaka 25..

Kama mapenzi hayachagui dini, kabila, rangi, basi mapenzi pia yasichague umri..

Thanks...
 
JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
2,573
2,000
Angeoa bila kuuliza, hadi kaja kuuliza bado haijampendeza yupo 50/50
Wakati mwingine kuuliza ni njia ya kupima unachoenda kukutana nacho mbeleni ili kujiandaa, haimaanishi kuwa haupo tayari na maamuzi ila unataka kujua unachoenda kukumbana nacho kwa maamuzi uliyoamua.
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
4,311
2,000
Jiulize kwanza aya
πŸ‘‰Unampenda kweli na yeye anakupenda kweli?
πŸ‘‰Moyo wako umeridhika kuwa nae?
πŸ‘‰Unafuraha kuwa nae? Ana furahia kuwa na wewe?
πŸ‘‰Anatimiza majukumu yake ipasavyo(ya kama mke na kama mama wa familia)?
πŸ‘‰Ana kuheshimu na ww una mheshim?

Kama majibu ni ndio bas Umri sio kigezo cha kuwatenganisha. View attachment 1986695
Tatizo mnafikiria urafiki ni sawa na ndoa. Ndoa ni kitu tofauti maana kuna mabonde na milima.
 
Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
55,229
2,000
Wakati mwingine kuuliza ni njia ya kupima unachoenda kukutana nacho mbeleni ili kujiandaa, haimaanishi kuwa haupo tayari na maamuzi ila unataka kujua unachoenda kukumbana nacho kwa maamuzi uliyoamua.
Tukimwambia matokeo hasi? Kama nlivoandika mimi? Ataacha? Bado hajapendezwa 😁
 
THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
436
1,000
Hamna shida ila jua wanawake twawahi kuzeeka na kuchakaa Sasa akikuzidi mtihani na menopause hyo hamu ukata utafanyaje hapo, ndio maana mwanaume akimzidi mwanamke miaka like 10 years wanakuja kuzeeka pamoja bila gap kuonekana
Ndoa yangu tarajiwa anakufa kabisa hivhivi...naona mpaka saiv watu wakupinga kumuoa alienizidi munaupiga Mwingi!πŸ˜‚πŸ˜‚
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,612
2,000
Malengo yako ni nini katika ndoa/mahusiano?
Kwa mfano, unataka huyo mwanamke akuzalie watoto?
Je, umri wa huyo mwanamke unaruhusu kuzaa? #menopause
Vipi jamii yako au ndugu zako unahisi watapokeaje?
Kumbuka ukioa unaunganisha undugu. Binafsi itaniwia vigumu sana kukubaliana na kijana wangu (I really hope sio wewe mleta mada......joke!) akiniletea mchumba mwenye umri kunizidi mimi baba yake au mama yake. Hainiingii akilini kuanza kumpa shakamoo "mkamwana" wangu! Kwangu mimi mwanamke akikuzidi miaka 1 mpaka 3 hivi sio mbaya sana....nahisi ni himilivu socially.

Lakini kubwa kuliko yote ni wewe kufurahia uhusiano wako. Haina maana sana kwako kuoa mwanamke uliyemzidi umri lakini humfurahii.
 
Nakushukuru karibu kwenye Ndoa soonπŸ™πŸ™πŸ˜‚πŸ˜‚
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom