Hivi mwanamke kuwa na nyumba ndogo ni dhambi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mwanamke kuwa na nyumba ndogo ni dhambi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Baikal Aguido, Jul 14, 2009.

 1. B

  Baikal Aguido Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni swali hususan kwa kaka zetu.

  Hivi sasa inaonekana ni hali ya kawaida na ni kama haki ya msingi kwa mume au wachumba jinsia ya kiume kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

  Wakati huohuo, binti au mke anapokuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya mpenzi'ye au mumewe huwa anaonekana kama doa katika jamii.

  Swali langu ni hivi, je tatizo liko wapi katika hili?
   
 2. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hamana tatizo kwa Mwanamke kuwa na nyumba ndogo iwapo kama Mr. anayo. Tena haina haja yakukasirikiana na kuwa na jazba eti kuona Mr. anayo then na wewe uende kwa maasira kutafuta ya kwako. Cha msingi a woman should just be patient watakuja tuu kwa wingi kumtongoza na kumuomba huo urafiki. Nasema hivi unajua pale mapenzi yanapopungua au kutoweka kabisa...kuna chemistry fulani hutokea kwa mwanamke na automatically wanaume huanza kumtongoza hapa na pale. Sasa ni juu yake kukubaliana nao au kukataa.
   
 3. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  GOD forbide!!!!!!!!!!!!!!!!! this does not wash,society is losing its bearings
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Penny nimecheka mh jibu lako uko fasta mamii.

  Mtazamo wangu ni kuwa kijamii mwanamme akiwa na wanawake wengi huonekana kijogoo ila sivyo kwa mwanamke (yeye ataonekana ni ma..... of which ni sifa mbaya). So kwa mtazamo wangu, kuna vitu ambavyo wanawake lazima tukubali kuwa katu hatuwezijilinganisha na mwanaume na kimoja wapo ni hiki cha na sisi kuwa na nyumba ndogo! Kwa nini nasema hivi
  1. Kimaadili hili si jambo zuri hata kwa mwanaume mwenyewe (ingawa wanalishabikia)
  2. Kibinaadam -just think of that process ya kuwa pamoja (kitendo) ni aibu kumfanyia yale mtu mwingine ambaye siye mwandani wako_ kwa kweli mwanamke tumeumbwa na haya za kike babu ah na ndo mana wenzetu kwao sawa tu hata akisimama pembeni ya barabara na kujisaidia haja ndogo hakuna ataemmaka ila kwetu lol. Sipati picha
  3. Wanawake tuna staha kuliko hao so hatujiweki low to that extent lol (mnitupie mawe sasa!!)

  Kuna mengi ya maendeleo ambayo tunaweza kujilinganisha nao lakini kwa hili hapana!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Penny naungana nawe katika hilo la chemistry jamani mie wakati napendwa yaani sikuwa na hata wa kunipa dada hujambo yaani hata nizunguke mjini siku nzima......... Sasa yalivyopungua lol yaani hadi kwero- Hivi kwa nini Penny lol
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  "Jino kwa Jino" or to put it in a better wording "akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia"
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Baba Enock mie nlikuwa najua hizi zina maana tofauti
  Jino kwa jino ni kama akikupiga la kushoto we mpige la kulia no?
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  hujajibu swali
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ni wapi imeandikwa mwanaume anaruhusiwa kuwa na nyumba ndogo?basi huko pia pameandikwa mwanamke pia ana ruhusiwa kuwa nayo.
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160

  Mwanajamii1,

  Kupendwa kuna maana nyingi sana!

  "Ulipokuwa unapendwa":-

  1. ulitumia muda mwingi kufikiria "mpenzi" wako
  2. ulitumia "resources" nyingi kumridhisha "mpenzi" wako
  3. ulifanya mambo yote kwa umakini sana usimkwaze "mpenzi" wako
  4. e.t.c

  In the process of doing 1,2,3 ... above unakuwa exhausted, stressful, ... and ultimately ule "uzuri" wako unapungua exponentially halafu una-tend kuwa "serious" and "reserved" kwa watu wa jinsia tofauti.

  Sasa pale inapotokea "kupendwa" kunaanza kupungua, na wewe automatically unaaza ku-react in different way kwenye 1,2,3.... na matokeo yake unaanza "kupendenza"....

  Haya jameni... by the way nyumba ndogo siku hizi ni "fasheni", either kwa mwanamume au kwa mwanamke.

  Weekend hii nilikuwa baa moja napata "kili baridi" maeneo ya sinza, wanywaji wote waliookuwa "coupled" hawakuwa mtu na mke wa ndoa, ingawaje wote walikuwa wameoa au wameolewa!
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Maana yake ni sawa ukitaka ku-justify "unyumba ndogo"!
   
 12. B

  Baikal Aguido Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakweli mambo ni matamu....
  Hasa tunapoonfelea feelings, wacha kabisa.
  Tetesi zinasema "mke wa mtu au mpenzi wa mtu anapokuwa nyumbandogo" ni raha ilioje upande wa jinsia 'ke'....
  Na hapo ndipo amani inapoanza kurudi kwa house hasa kama alikua anaonekana karaha ya nyumba.
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante Baba_Enock- Umenielewesha.
   
 14. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Ni suala la mila zaidi.Wanaume toka zamani ilikuwa sio tatizo kuoa na kutembea na wanawake zaidi ya mmoja. Isipokuwa leo hii hata kama mtazamo uko hivyo, mbona sioni tofauti kati ya wanaume na wanawake kwenye suala la nyumba ndogo?Wanawake nao wameamua ati kuingia katika fani.Kwa yale ninayoyaona, mimi hata nikitembea nimeweka % fulani kwamba mke wangu pia ana nyumba ndogo. Vinginevyo ntajakufa na pressure buree na mambo yanayoendelea ulimwengu wa leo.Lol
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unadhani hili limeanza sasa hivi? Kwa maoni yangu hili lilikuwepo tangia zamani. Nilikuwa najaribu kutizama maisha ya ndoa ya wanaume wa rika ya baba yangu (about 65 yrs). Naweza kuthubutu kusema, kati ya wazee hawa kumi basi karibu saba wana watoto wa nje ya ndoa! Kwa jamii nyingi ambazo zinaruhusu ndoa za mitala, hili la mwanaume kuwa na nyumba ndogo halitizamwi kama ni tatizo.
  Ni kweli kwa jamii nyingi za kitanzania, mwanamke hawezi kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ukweli huu unafanya hata swala la mwanamke kuwa na hiyo unayoiita 'nyumba ndogo' (wengine wanaita 'kidumu'!) kutokubalika kijamii.

  Zaidi ni kwa sababu ya athari za mfumo dume, lakini pia hata kibaolojia ni vigumu zaidi kwa mwanamke kuolewa na wanaume wengi kwa wakati mmoja.

  Si katika mapenzi hata katika mambo mengine jamii inatend kuwa na mategemeo ya kitabia tofauti kutoka kwa mwanamke. Unajisikiaje ukiona mwanamke (kwa hapa Tanzania) anavuta sigara au mlevi?
   
  Last edited: Jul 14, 2009
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiyo ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja hata wanawake inakuaga hivyo. Siyo kitu cha kushangaza kusikia mwanamke ana more than one boyfriend.

  Hilo la kuwa ndani ya ndoa hata wanawake wana mabwana wa nje. The big question is "DO two wrongs make a right?"

  Hakuna anayepaswa kuwa na nyumba ndogo au mwanaume au mwanamke. Who ever does it is wrong regardless of the gender.
   
 17. B

  Bunduki Member

  #17
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unauliza jibu? Nadhani wewe unastahili kuelezwa maana ya neno dhambi. Dhambi, ni uasi, ni tendo lililo kinyume na maadili au linaloasi sheria ya Kimungu (divine law) Na katika sheria ya Kimungu, kuna mke na mume tu, the rest ni kujinyima upepo. Labda ungetumia neno ni halali au sio halali, lakini kwa case ya kuwa dhambi, it's very obvious
   
 18. M

  Mintanga New Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyumba ndogo sio nzuri kwa wote iwe mume au mke.itaweletea matatizo kaeni chini muangalie tatizo lipo wapi.
  Mintanga
   
 19. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mambo dear, pole nilikuwa nimesafiri kidogo...nashukuru kwa kunielewa nadhani hiki kipengele ndicho nilichokuwa nakazia katika mada hii na jibu nililotoa hapo juu...sio kwamba eti tujilinganishe na wanaume hapana...kwanza ni kitu kisichowezekana. Kwa kweli hiki kitu cha chemistry hata mimi kimeshanitokea sana tuu. Nadhani kuna signs fulani mwanamke hutoa ambazo humjulisha mwanaume kuwa umpweke wa mapenzi...huo ndio mtazamo wangu dear.
   
 20. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kha! umepikiwa, umepakuliwa sasa mpaka ulishwe! haya basi jibu ni si dhambi kabisa endapo mwenzake hamtekelezei...
   
Loading...