Hivi muda wa MWANAMUME kurudi nyumbani ni saa ngapi?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Jana jirani yangu wamebwatizana na mkewe kisa jamaa karudi nyumbani saa Nne usiku wakati kawaida yake saa mbili huwa anakuwa sebuleni anaangalia TV.

Nikajiuliza kwani ni haki kwa mwanaume kupangiwa na mke wake muda wa kurudi nyumbani? Muda wa mwanaume kurudi nyumbani ni upi?
 
Mwanaume anatakiwa afike nyumbani muda wowote. Hakuna muda muafaka wa mwanaume kuja nyumbani.
 
Aisee mtatusaidia sana ikiwa swali hili litajibiwa vema..

Hallo ni source ya bifu hata kwangu...(nadhani hata kwa wengine)

Ukitoka tu swali utarudi saa ngapi?? sasa weka muda uone ngoma yake..

natega sikio..
 
sio vizuri kuchelewa nyumbani! mwanaume unatakiwa kuwahi saa kumi na moja asubuhi kabla watu hawajaamka! ukichelewa zaidi ya hapo kwa kweli si vizuri kwani majirani na watoto watakuwa wameamka
 
Mzee vita yako na TAMWA hatutaiingilia.
 
Mimi kwangu sina muda maarumu,mara 11 jioni,mara saa 2,mara saa 5,sometime saa 8 na ukiona mkeo anakupigia kelele ooooh sijui nini, toka nae na siku hiyo uhakikishe mnarudi alfajiri ili ajionee asinzie mezani aliwe na mbu akisema baba watoto twende we unamwambia subiri kidogo tu mpenzi tunaondoka sasa hivi,uone kama atarudia tena ukimwambia tena twende atakataa ila atakwambi usirudi alfajiri.
 
Hapo kazi ipo.
 
Jana jirani yangu wamebwatizana na mkewe kisa jamaa karudi nyumbani saa Nne usiku wakati kawaida yake saa mbili huwa anakuwa sebuleni anaangalia TV.

Nikajiuliza kwani ni haki kwa mwanaume kupangiwa na mke wake muda wa kurudi nyumbani? Muda wa mwanaume kurudi nyumbani ni
upi?

Kusema kweli masuala ya ndoa yanahitaji HESHIMA tu na si kitu kingine. Bahati nzuri siku hizi kuna mawasiliano ya kutosha na hivyo mwenza wako kama kweli unamjali na una sababu iliyokuzuia mpaka muda fulani usifike nyumbani, basi bila shaka anaweza kujua mapema\...Ingawa wengine wanatumia mawasiliano haya vibaya.
Hakuna ulazima wa kupangiana muda wa kurudi nyumbani na mwenzako kama mnaaminiana na kuheshimiana katika ndoa yenu.
Nafikiri mpaka watu wanaamua kuishi pamoja, kama mume na mke, watakuwa wanajuana vizuri na hata kuamianiana pia.
Kwa hiyo hili suala la kupangiana muda wa kurudi nyumbani si dalili ya mapenzi ya dhati na mwenza wako.
 
Hakuna muda maalum, ni pale atakapojisikia kurudi nyumbani la msingi asilale nje ya nyumba.
 
Kama una family na watoto ni vizuri kuhakikisha unawahi then kama kuna safari ndio utoke, au hata ukipitiliza happy hour ukumbuke kuna watu home wanakusubiria, kuna siku zingine inaeleweka unapitiliza lakini isiwe mazoea ya kurudi manane kila siku
 
Kusema kweli masuala ya ndoa yanahitaji HESHIMA tu na si kitu kingine. Bahati nzuri siku hizi kuna mawasiliano ya kutosha na hivyo mwenza wako kama kweli unamjali na una sababu iliyokuzuia mpaka muda fulani usifike nyumbani, basi bila shaka anaweza kujua mapema\...Ingawa wengine wanatumia mawasiliano haya vibaya.<br />
Hakuna ulazima wa kupangiana muda wa kurudi nyumbani na mwenzako kama mnaaminiana na kuheshimiana katika ndoa yenu.<br />
Nafikiri mpaka watu wanaamua kuishi pamoja, kama mume na mke, watakuwa wanajuana vizuri na hata kuamianiana pia.<br />
Kwa hiyo hili suala la kupangiana muda wa kurudi nyumbani si dalili ya mapenzi ya dhati na mwenza wako.
big up Zak,nimekuaminia mkuu?
 
Mimi napata wakati mgumu sana kujibu hili jambo maana sidhani kama kuna muda maalumu wakurudi nyumbani. Mimi nadhani muda wowote mwanaume akitoka ofisini arudi nyumbani na si mambo ya kupita sijui happy hours, sijui bar au club...hii tabia ni ya wapi lakini watanzania? Kama tunatoka kwenda kupata nyama choma au beer mbili tutoke na familia zetu baada ya kufika nyumbani kuongea na familia kuhusu siku ilivyokuwa ndo kuelekea sasa kwa kinywaji au mlo wa jioni na familia either mke na watoto au kama hakuna watoto na mkeo au mumeo baada ya hapo kurudi nyumbani na kupumzika kwa ajili ya siku inayofuata. Hii tabia ya kutoka kazini kukaa bar mpaka saa 6 au 7 ndo inatufanya tunakuwa maskini maana muda mwingi tunatumia kulewa na kuumwa hangover siku inayofuata. Halafu tunalalamika maisha magumu kila siku. Kwanini tusiwe tunaishi kwa mipango. Na badala ya kujisifia kwa kukaa bar au kukesha usiku kucha basi tujisifie kwa kufanya kazi na kutengeneza pesa nyingi. Tuseme mwanaume kufanya kazi masaa mangapi kwa siku, au mwanaume kipato kiasi gani kwa mwezi...? Tuwe na sifa kwa mambo ya maana. Mwanaume hasifiwi kula ila kazi...! TUBADILIKE
 
Are u serious mkuu?
 
Mimi kwangu sina muda maarumu,mara 11 jioni,mara saa 2,mara saa 5,sometime saa 8 na ukiona mkeo anakupigia kelele ooooh sijui nini, toka nae na siku hiyo uhakikishe mnarudi alfajiri ili ajionee asinzie mezani aliwe na mbu akisema baba watoto twende we unamwambia subiri kidogo tu mpenzi tunaondoka sasa hivi,uone kama atarudia tena ukimwambia tena twende atakataa ila atakwambi usirudi alfajiri.

nimeipenda ndg.
 
Siwezi kupangiwa muda wa kurudi lakini ni muhimu kupita home baada ya kazi kama una mke na watoto na kama una la muhimu toka na usichelewe sana.Pia ni muhimu kutoka siku mojamoja na mkeo awajue rafiki zako na viwanja vyako hii hujenga uaminifu.Ikibidi huwezi pita home baada ya kazi piga simu mjulishe mwenzako ni kitu kidogo lakini muhimu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom