Hivi mtu unawekaje namba yako ya simu huku eti watafuta mchumba?

jf user

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
777
622
Mimi huchukulia mitandao kama pori ambalo lina kila aina ya wanyama, wakuliwa, wasio wa kuliwa na wanyama hatari.
Ubaya Zaidi hizo namba mnazoweka humu mitandaoni huwa hazifutiki kwani hubaki milele.
Chakusangaza humu watoto, ndugu na watu wa kila aina wanapita humu wanaona uchafu humu. Hivi hujui kama wajidhalilisha ni kwa namna gani ulivyo mchafu unatafuta watu mitandaoni na kuacha namba zako bila soni?

Swala la usalama hulizingatii hujui kwamba kuna maharamia humu? ukibakwa au kufanyiwa vitendo vya kinyama utadhubutu kuja kulia shida zako hapa?

Watu mnafikiria kwa kutumia nini hivi? You are stupid kind of people i ever saw! Ubaya Zaidi mnachepuka na hamjui wake au waume zenu wapo wanawachora tuu. Mungu akianza kulipa maovu yenu mnalalamika mmesalitiwa mmefanywa nini kumbe ni malipo ya dhambi zenu!

Mjirekebishe na mjifunze mwanaume au mwanamke wa kweli haweki namba zake ovyo mitandaoni au popote pale.
Shame upon you.
 
sijakuelewa mkuu, wanabakwa mtandaoni au?? 😕😕😕
Mazungumzo si yanaanzia humu halafu huko wanakokwenda kukutana ndio hayo mabalaa yanafanyika?
By the way mkuu una umri gani?
 
Mimi huchukulia mitandao kama pori ambalo lina kila aina ya wanyama, wakuliwa, wasio wa kuliwa na wanyama hatari.
kweli nimeamin mitandao ni pori na leo nimekutana na nyani anaetafuta matunda porini. anyway I'll back soon ukipata unachokitaka huku kwenye hili pori.
 
Mawasiliano sio siri kama unavyofikiria,acha fikra za kizamani,kuna rais mmoja alishawahi kuweka namba zake za simu,hata gavana wa jiji moja hapa bongo anae aliweka namba zake za simu,
makamanda wa polisi wa mikoa yote namba zao za simu ziko mitandaoni,wewe tu ndio waona dili sana namba za simu,chukua yangu basi 0717 422222 kama dili sana
 
Pole sana ndugu kwama unashindwa kutofautisha namba za ofisi na namba binafsi una safari kubwa sana.
 
Labda aweke Pm sio Public. labda Ndo mana ya mtoa mada .ushauri wake sio mbaya sana
 
Mtoa maada anaonyesha jinsi alivyo makini ndio inavyotakiwa wasiwasi ndo akili.nataka mwanamke wa hivihivi Kama mtoa maada
 
Back
Top Bottom