Hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kusema kuwa unatafuta mwenzi mcha Mungu?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,115
Vijana wengi wakike na wakiume wanapotafuta mke/mume huandika kuwa wanamtaka mcha Mungu.

Hivi ni nani atakuambia kuwa mimi simchi Mungu? Kumcha Mungu (kumwogopa Mungu) ni jambo la ndani ya moyo. Hata jambazi hutaka mcha Mungu. Hata mafisadi hutaka mcha Mungu

Hata wanaokwenda kwa waganga wa kienyej hutaka mcha Mungu. Mungu anasema atakupa wa kufanana na wewe. Mke au mume haji kwako kwa bahati mbaya. Utampata mwenye kicho sawa na wewe.

Niliapa tangu zamani kuwa pamoja na ulokole wangu sitapiga goti kuomba mke. Mke ni zao la maisha yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom